BUNJU SISTERS GROUP INAKARIBISHA WANACHAMA WAPYA


Kikundi cha Bunju Sisters Group kimekuwa kikikutana kila mwisho wa mwezi kwaajili ya kupea taarifa mbalimbali za chama, mapato na matumizi pamoja na mipango ya baadae ya kikundi chetu

Kuanzia kushoto ni Wendy muweka hazina , wapili ni Suzan Nzota Katibu na wamwisho ni Loyce Joseph mwenyekiti wa kikundi
Japo tumekuwa na misukosuko mbalimbali ikiwemo ya misiba ya wanafamili wa wanachama wetu, wengine kutengana na kikundi kuelekea vyuoni kwa masomo pamoja na ubize wa kazi za kila siku lakini Umoja na urafiki bado unadumu kati yetu

Kutoka kushoto ni Bibiana, Suzy na Janeth Jackson

Pole kwa Janeth Jackson aliye mpoteza Mume wake Kipenzi, Pole kwa Rosemery aliye fiwa na baba yake kipenzi kwa upande mwingine Hongera kwa Bibiana aliye mwozesha mdogo wake na Lucy aliye baatika kupata mtoto wa kiume mungu awape maisha marefu sana wana kikundi



Mara nyingi tumekuwa kwenye vikao vya usiku, kutoka out kubadilishana mawazo na mara zingine tunatembeleana ili kuzidisha mshikamano wetu. Tume weza kukopeshana na kusaidia kwenye matatizo mbalimbali kama msiba na harusi na kiuchumi.

Kutoka kushito ni Janeth, Loyce Joseph, Bibiana na Lucy
Mwenyekiti wa Bunju Sisters Group anapenda kuwkaribisha kina dada wote wenye nia ya maendeleo na kusaidana, kupata marafiki katika eneo la Bunju kuwasilina nasi kupitia Simu no. 0659 269416 kwani huu ni muda wa kukaribisha wanachama wapya. Vigezo na masharti nivya kawaida Karibu.

MAFUNZO KWA WALIMU WALIOPO KAZINI MKOANI MWANZA YAFUNGULIWA RASMI NA KATIBU MKUU ELIMU


Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi Prof. Sifuni Mchome amefungua rasmi mafunzo kwaajili ya walimu walioko kazini katika mkoa wa mwanza ambapo ameweza kutembelea baadhi ta vyuo na shule mkoani hapo.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyakurunduma iliyoko jijini Mwanza ambapo alitembelea shule hiyo kuona ujenzi wa miundombinu (maabara, vyooo, ukarabati wa madarasa na tanki la maji)
9 KANEMBWA WATAKIWA KUWASILISHA UTETEZI

9 KANEMBWA WATAKIWA KUWASILISHA UTETEZI

Release No. 020
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Februari 6, 2014

9 KANEMBWA WATAKIWA KUWASILISHA UTETEZI

Wachezaji tisa wa Kanembwa JKT pamoja na timu yao wanaolalamikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kumpiga mwamuzi Peter Mujaya wanatakiwa kujitetea mbele ya Kamati ya Nidhamu itakayokutana Jumapili (Februari 9 mwaka huu).

Utetezi huo unaweza kuwa wa mdomo kwa walalamikiwa kufika wenyewe mbele ya kamati itakayokutana saa 4 kamili asubuhi au kuuwasilisha kwa njia ya maandishi.

TAWLA YAONGEZA JITIHADA ZA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI NCHINI




Chama cha wansheria wanawake nchini Tanzania TAWLA, kimeanzisha utaratibu wa msaada wa namna jamii inavyoweza kupata huduma za kisheria kwa kuanzisha utaratibu wa wanasheria wasaidizi.








Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Aisha Bade amesema wanasheria wasaidizi watakuwa wanaelekeza jamii namna ya kupata huduma za kisheria hasa kwa makundi yenye uhitaji wakiwemo wanawake, watoto, wajane, waathirika wa ubakaji pamoja na matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu.


Kwa mujibu wa Bi. Bade, mpaka sasa TAWLA imeshafundisha na kuandaa wanasheria wasaidizi 412 waliosambazwa maeneo mbali mbali nchini, ambao uwepo wao utapunguza garama ya kupta huduma za kisheria pamoja na pengo la uhaba wa huduma hiyo katika jamii.

MAKAMPUNI YANAYO CHUKU RUSHWA NA KUTOZA FEDHA NYINGI KINYUME NA KIWANGO HUSIKA WAKATI WA KUUNGANISHA UMEME VIJIJINI KUSHUGULIKIWA


Wakala wa nishati vijijini REA, imeanza kufanya uchunguzi kuhusiana na tuhuma kuwa baadhi ya wakandarasi wanaosambaza umeme vijijini wamekuwa wakichukua rushwa kutoka kwa wateja ili kuwaunganishia huduma hiyo.



Mkurugenzi mkuu wa REA Dkt. Lutengano Mwakahesya, amesema hayo katika mahojiano na East Africa TV, ambapo amewataka wananchi kutokubali kutoa rushwa kwa kampuni zinazounganisha huduma hiyo vijijini.

Kwa nini uchukue rushwa kwa mwananchi wa kijijini ambaye maisha yake ni bado yana mahitaji mengi, hili suala sio zuri kabisa na Waziri wetu (Mhe. Sospeter Muhongo) ameshatoa kauli kuwa nikinyume cha taratibu” amesema Lutengano
RAIS KIKWETE: Kampeni za Uraid hazijaanza rasmi, Amtaka Philip Mangula Kuwashugulikia wanao fanya kampeni

RAIS KIKWETE: Kampeni za Uraid hazijaanza rasmi, Amtaka Philip Mangula Kuwashugulikia wanao fanya kampeni

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa kampeni za kugombea kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) hazijaanza rasmi.
 
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa vitendo vya baadhi ya watu kuanza kampeni kabla ya wakati wake ni moja ya mambo yanayosikitisha.

Hata hivyo, Rais Kikwete amesema kuwa suala hilo zima limekabidhiwa kwa Makamu wa Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara) Mzee Philip Mangula ambaye atalisimamia jambo hilo na kulishughulikia.

Kategori

Kategori