TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI

VIJANA wameaswa kuachana na tabia ambazo zinapelekea kusambaza ugonjwa wa ukimwi ili kuweza kujiepusha na maambukizi mapya ya Ukimwi,
Hayo yamekuja kutokana na Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo uadhimishwa taree 1 ya mwezi wa 12 kila mwaka na kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika Mkoani Lindi. ambapo Raisi Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.



Tabia ambazo vijana wameaswa kuachana na nazo nizile tabia hatarishi ambazo zinapelekea maambukizi mapya, kama kutotumia Condom, Kushindwa kusubiri na Uaminifu, nanjia zingine kama Matumizi ya Sindano hasa katika makundi ya vijana wanao Tumia madawa ya kulevya na ulevi kupindukia


Kaulimbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni Tanzania bila maambukizi mapya,bila vifo vitokanavyo na Ukimwi,na bila unyanyapaa inawezekana. 


Hatahivyo Msemaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania yani TACAIDS Bi.Gloria Mziray ameelezea malengo ya Tumehiyo ni kuakikisha kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kinakuwa chini sana ifikapo 2016.






EmoticonEmoticon