HUSENI RAMADHANI AKA SHARO MILIONEA
                            AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI

Msani wa Muziki na Maigizo nchini Sharo Milionea aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika eneo la Maguzonizonga, kwaajali ya gari alilokuwa akiendesha kutokea Dar akielekea Tanga, anatarajiwa kuzikwa kesho huko mkoani Tanga


Tarifa toka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga Constatine Masawe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho,nakueleza kuwa Marehemu alikuwa kwenye gari no T478 BVR Toyota Harrier, na alikuwa akitokea Dar na alipofika eneola Maguzonizonga Wilaya ya Muheza gari lake liliacha njia nakupinduka mara kadhaa
   



Kamanda Masawe, amesema mwili wa Marehemu umeifadhiwa kwenye Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, nakuongeza kuwa mazingira ya eneo la tukio hakuna kona kali wala ubovu wa barabara na kuwa Marehemu alikuwa pekeyake ndani ya gari hilo


EmoticonEmoticon