WATUHUMIWA WA UHAMSHO WA PUNGUZIWA DHAMANA


Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo imepunguza masharti ya dhamana kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar, wanaokabiliwa na mashtaka ya kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu wa mali.

 Afisa habari mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Mohamed Mhina, amesema kuwa uamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe.Ame Pinja, baada ya kukubali maombi ya Mawakili wa Watuhumiwa walioomba kupunguzwa kwa masharti hayo. kesi hiyo itatajwa tena Desemba 4, mwaka huu


Mnamo Octoba 12 mwaka huu, vurugu zilivuka katika baadhi ya mikoa nchini hasa Zanzibar na Dar es Salaam, baada ya mtoto momja kukojolea Msaafu. Miongoni mwa Vurugu za Zanzibar zilipelekea viongozi wa Uhamsho kuchukuliwa hatua kwakile kilicho daiwa na mahakama ni kuchochea Vurugu zilizo pelekea uharibifu wa mali


EmoticonEmoticon