SHARO MILIONEA AZIKWA LEO

Mamia ya watu wakiwemo wasanii, leo wamefurika ilikumzika msanii wa Vichekesho, Maigizo na Muziki mareemu Husein Mkiety aka Sharo Milionea, mkoani kwa Tanga wilaya ya Muheza


Sharo Milionea alifikwa na umauti baada ya kupata ajali ya Gari yenye namba za usajili T478 BVR, akiwanjiani kuelekea Tanga akitokea Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumanne ya taree 26/11/2012, tarifa zinasema gari hilo lilipasuka tairi kisha kuacha njia na kupinduka marakadhaa kitu kilicho pelekea Sharo Milionea kufikwa na umauti.


Mareemu sharo Milionea, alizaliwa mwaka 1985, nakupoteza maisha mwaka huu 2012, akiwa na umri wa miaka 27. Mareemu Sharo Milionea atakumbukwa kwa ucheshi na ubunifu wake katika sanaa ya maigizo.


Baadhi ya mashabiki wa Bongo Movie na Bongo Fleva kwa ujumla wametoa pole na masikitiko yao, walipokuwa wakifanya mahojiano na Blog hii, Hance Mley wa Ubungo anasema, "Bongo kuna wasanii wengi ila Muonekano na Upeo wa kuwa mbunifu alikuwa na Mareemu Sharobaro...kwaujumla nimesikitishwa sana.


Watuwengi waliofanya mahojiano na Blogu hii wamelilia kushindwa kufika katika mazishi ya Msanii huyo wakitamani msiba huo Ungekuwa jijini Dar es Salaam iliwaweze kumuaga Mpendwa wao Sharo Milionea.


EmoticonEmoticon