TANZANIA BADO INAIDAI UGANDA FIDIA YA VITA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inategemea kulipwa na serikali ya Uganda kiasi cha dola za Marekani  milioni nane laki nane na alfu 24, ikiwa ni fedha za fidia ya vita ambayo Tanzania ilipigana nchini Uganda Miaka ya 1977/78.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania Shamsi Vuai Nahodha alisema hayo alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Mbinga mjini Dodoma John Komba aliyetaka kufahamu iwapo serikali ya Tanzania inafanya lolote juu ya madai ya fidia ya fedha za kupigana vita nchini Uganda.

Waziri Nahodha amesema kuwa, nusu ya fedha yote iliyokuwa ikidaiwa ilikwishakulipwa na kubakia kiasi hicho cha fedha ambacho bado hakijalipwa.


EmoticonEmoticon