HONGERA KENYA KWA MIAKA 50 YA UHURU

Rais Uhuru Kenyatta jana amewaongoza wananchi wa Kenya kusherehekea miaka 50 ya uhuru, na kuwataka kudumisha umoja na moyo wa uzalendo ulionyeshwa na wapigania uhuru wa Kenya, kwa kudumisha amani na mshikamano katika taifa hilo.

Akihutubia taifa la Kenya katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kasarani ameelezea mafanikio kadhaa yaliyofikiwa kiuchumi na kimaendeleo, ikiwa ni pamoja na  ujenzi wa barabara, reli na miundombinu mingine itakayochangia kasi ya ukuaji wa uchumi na kutoa ajira kwa wananchi.

Amesema kuwa Kenya imefanikiwa katika elimu ambapo hadi kufikia sasa asilimia 90 wananchi wanajua kusoma na kuandika, ambapo kwa upande wa afya wamefanikiwa kujenga vituo vingi vya afya karibu na wananchi.

Sherehe hizo zimehudhuriwa pia na wakuu wa nchi wapatao 19 wakiwemo rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Museveni wa Uganda, Goodluck Jonathan  wa Nigeria pamoja na Dk. Joyce Banda wa Malawi ambao walipata nafasi ya kuwapongeza na wananchi wa Kenya.


EmoticonEmoticon