TANZANIA BILA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI

VIJANA wameaswa kuachana na tabia ambazo zinapelekea kusambaza ugonjwa wa ukimwi ili kuweza kujiepusha na maambukizi mapya ya Ukimwi,
Hayo yamekuja kutokana na Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambayo uadhimishwa taree 1 ya mwezi wa 12 kila mwaka na kitaifa maadhimisho hayo yatafanyika Mkoani Lindi. ambapo Raisi Jakaya Kikwete atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.



Tabia ambazo vijana wameaswa kuachana na nazo nizile tabia hatarishi ambazo zinapelekea maambukizi mapya, kama kutotumia Condom, Kushindwa kusubiri na Uaminifu, nanjia zingine kama Matumizi ya Sindano hasa katika makundi ya vijana wanao Tumia madawa ya kulevya na ulevi kupindukia


Kaulimbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni Tanzania bila maambukizi mapya,bila vifo vitokanavyo na Ukimwi,na bila unyanyapaa inawezekana. 


Hatahivyo Msemaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania yani TACAIDS Bi.Gloria Mziray ameelezea malengo ya Tumehiyo ni kuakikisha kiwango cha maambukizi ya Ukimwi kinakuwa chini sana ifikapo 2016.





 UGANDA KUSHUGULIKIA MAKAMPUNI YA SIMU
Serikali ya Uganda imetangaza kuyatoza faini makampuni ya simu yatakayo kuwa na matatizo katika mawasiliano

Tume ya mawasiliano ya nchi hiyo, imesema tayari imeunda chombo maalum chenye mfumo wa computer utakayo fuatilia mitandao itakayo kuwa na matatizo kama vile simu kukata mawasiliano, kukatika, makampuni kutoza viwango zaidi ya zile inavyotangaza.

kwa mujibu wa mkurugenzi wa mawasiliano ya kisheria wa Tume ya Mawasiliano nchini humo UCC Susan Wegoye, amesema faini hizo zitakuwa zikiangalia nikiasi gani cha hasara ambacho kampuni husika imesababisha kwa watumiaji wake kwa muda wa mwaka mzima

pia amesema faini azitatozwa endapo tu,matatizo hayo ya kimtandao yatakuwa yamesababishwa na majanga yasiyo weza kuzuilika kama vile mafuriko,dhoruba na vita.

 WAMILIKI WA MABASI DAR WATAKIWA KIJIPANGA KIBIASHARA

Chama cha wamiliki wa Mabasi jijini Dar es Salaam, kime waasa wamiliki wa mabasi kuwa tayari kwaajili ya changa moto za kibiashara zitakazo letwa na mradi wa mabasi yaendayo kasi


M/Kiti wa chama hicho Bwana Sabri Mbabruk amesema biashara za Mabasi azitaendeshwa tena na mtu mmoja mmoja na badala yake kutakuwa na kampuni mbili tu kwaajili ya kufanya biashara hiyo

Aidha amesema kuwa ilikupunguza msongamano wa magari jijini, serikali imeamua kubadili mfumo wa uendeshaji magari jijini na kuazimia kuanzisha mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.

kwa upande mwingine, mamlaka ua udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA, itasitisha utoaji leseni kwa wamiliki wa daladala, na kusitisha swala la kurudia leseni ifikapo juni mwakani.Nakuwa taka wamiliki wa barabara ya Kilwa na Alhassan Mwinyi kuanza kuunda makundi yao.

       VIJANA WAASWA KUMILIKI NYUMBA

Vijana nchini wametakiwa kumiliki nyumba kupia utaratibu nafuu wa nyumba za mikopo na kuachana na mtindo wa sasa ambapo kila kijana anataka kumiliki nyumba kwa kununua ardhi na kusimamia ujenzi yeye mwenyewe


hayo yamesemwa na Waziri wa Ardhi, Nyumna na Maendeleo ya Makazi Mhe. Pfor. Anna Tibaijuka wakati akizindua nyumba za kisasa zinazojengwa na shirika la nyumba la Taifa NHC, mtaa wa Ilala Mchikichini jijini Dar es SALAAM


Prof.Anna Tibaijuka, amesema Vijana wameshindwa kumiliki nyumba wenyewe kutokana na kasumba ya kutaka kununua kiwanja, Vifaa vya ujenzi na kusimamia ujenzi hatua ambayo Waziri huyo ametaja kuwa niya garama


                      UCHIMBAJI WA URENIUM 
                WAZIDI KUPINGWA

SIKU chache baada ya kituo cha haki za binadamu LHRC, kutoa msimamo wake wa kupinga mpango wa serikali kuchimba madini aina ya URENIUM, mbunge wa Ubungo ambaye pia ni Waziri kimvuli wa Nishati na Madini, amejitokeza na kupinga uchimbaji wa madini hayo
Mnyika amesema, uchimbaji wa madini ya Urenium utasababisha nchi kuingia vitani, kwani nchi zote zinazo chimba madini hayo zina mogogoro ya kizita. na kusisitiza kuwa serikali aina budi kutilia mkazo swala hilo
Aidha Mnyika amesema, nchi kama Congo inazongwa na migogoro ya Kivita kutokana na kuwepo kwa madini hayo ambayo nigali sana Duniani na Utumika kutengenezea Chemicali na Silaha za Kivita kama Nuclear

                                           SHARO MILIONEA AZIKWA LEO

Mamia ya watu wakiwemo wasanii, leo wamefurika ilikumzika msanii wa Vichekesho, Maigizo na Muziki mareemu Husein Mkiety aka Sharo Milionea, mkoani kwa Tanga wilaya ya Muheza


Sharo Milionea alifikwa na umauti baada ya kupata ajali ya Gari yenye namba za usajili T478 BVR, akiwanjiani kuelekea Tanga akitokea Jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumanne ya taree 26/11/2012, tarifa zinasema gari hilo lilipasuka tairi kisha kuacha njia na kupinduka marakadhaa kitu kilicho pelekea Sharo Milionea kufikwa na umauti.


Mareemu sharo Milionea, alizaliwa mwaka 1985, nakupoteza maisha mwaka huu 2012, akiwa na umri wa miaka 27. Mareemu Sharo Milionea atakumbukwa kwa ucheshi na ubunifu wake katika sanaa ya maigizo.


Baadhi ya mashabiki wa Bongo Movie na Bongo Fleva kwa ujumla wametoa pole na masikitiko yao, walipokuwa wakifanya mahojiano na Blog hii, Hance Mley wa Ubungo anasema, "Bongo kuna wasanii wengi ila Muonekano na Upeo wa kuwa mbunifu alikuwa na Mareemu Sharobaro...kwaujumla nimesikitishwa sana.


Watuwengi waliofanya mahojiano na Blogu hii wamelilia kushindwa kufika katika mazishi ya Msanii huyo wakitamani msiba huo Ungekuwa jijini Dar es Salaam iliwaweze kumuaga Mpendwa wao Sharo Milionea.

                       HUSENI RAMADHANI AKA SHARO MILIONEA
                            AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA GARI

Msani wa Muziki na Maigizo nchini Sharo Milionea aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika eneo la Maguzonizonga, kwaajali ya gari alilokuwa akiendesha kutokea Dar akielekea Tanga, anatarajiwa kuzikwa kesho huko mkoani Tanga


Tarifa toka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga Constatine Masawe amethibitisha kutokea kwa kifo hicho,nakueleza kuwa Marehemu alikuwa kwenye gari no T478 BVR Toyota Harrier, na alikuwa akitokea Dar na alipofika eneola Maguzonizonga Wilaya ya Muheza gari lake liliacha njia nakupinduka mara kadhaa
   



Kamanda Masawe, amesema mwili wa Marehemu umeifadhiwa kwenye Hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza, nakuongeza kuwa mazingira ya eneo la tukio hakuna kona kali wala ubovu wa barabara na kuwa Marehemu alikuwa pekeyake ndani ya gari hilo

         TANZANIA YAONGOZA KUTOA RASIMU YA VIWANGO VYA UBORA

Tanzania yawa ya kwanza kutoa rasimu ya Viwango vya ubora kwa bidhaa zenye jamii ya nafaka na kunde,
miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.ambayo itawawezesha wafanya biashara nchini kuuza hadi soko la kimataifa


Rasimu hiyo ambayo inalenga hasa bidhaa za Bogamboga na Mazao ya Mbegumbegu, itawawezesha watengenezaji na wazalishaji wa bidhaa hizo kuwa na viwango ambavyo vinaidhinisha matumizi salama kwa binadamu


Aidha wafanya biashara wa bidhaa hiyo wamepewa mafunzo na shirika la viwango Tanzania TBS ilikukidhi vigezo na viwango ambavyo vimewekwa na shirika hilo


MPANGO WA DAMU SALAMA WAPUNGUZA V.V.U

     

Mpango wa damu salama nchini, umepunguza kiwango cha virusi vya Ukimwi kutoka asilimia 7% mpaka 1% kwa mwaka huu. Meneja Mradi wa Mpango wa Damu Salama nchini, Dr. Efesper Nkya, amesema mpaka kufikia mwisho wa mwaka huu maambukizi yatafikia chini ya asilimia moja,


Hatahivyo Meneja huyo amewataka vijana kujitokeza kwa wingi na kuchangia damu, kwani Benki ya Damu nchini inaupungufu mkubwa wa Damu, na kusisitiza kuwa utoaji damu nijukumu la kilamtu

WATUHUMIWA WA UHAMSHO WA PUNGUZIWA DHAMANA


Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe mjini Zanzibar leo imepunguza masharti ya dhamana kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislamu Zanzibar, wanaokabiliwa na mashtaka ya kusababisha vurugu na kupelekea uharibifu wa mali.

 Afisa habari mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Mohamed Mhina, amesema kuwa uamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe.Ame Pinja, baada ya kukubali maombi ya Mawakili wa Watuhumiwa walioomba kupunguzwa kwa masharti hayo. kesi hiyo itatajwa tena Desemba 4, mwaka huu


Mnamo Octoba 12 mwaka huu, vurugu zilivuka katika baadhi ya mikoa nchini hasa Zanzibar na Dar es Salaam, baada ya mtoto momja kukojolea Msaafu. Miongoni mwa Vurugu za Zanzibar zilipelekea viongozi wa Uhamsho kuchukuliwa hatua kwakile kilicho daiwa na mahakama ni kuchochea Vurugu zilizo pelekea uharibifu wa mali

       Waziri wa US,Hillary Clinton kuanza Mazungumzo ya Amani kati ya Israel na Palestina


Waziri wa Mambo ya Mambo ya Nnje ya Marekani Bi.Hillary Clinton leo atatembelea Israeli, Ramallah ilikuendeleza mazungumzo ya amani kutokana na masambulizi ya Gaza yaliyo fanywa na Israel
 

Jeshi la Israeli, limeuwa takribani watu 110 wengi wao wakiwa ni watoto na wanawake, huku watu 900 wakiwa wame jeruhiwa vibaya.Majeshi ya Israeli yaliongeza kuwa walituma nguvu nyingi katika uvamizi huo



Hawa ni baadhi ya watoto ambao wamefichwa kutokana na mashambulio hayo ya Israeli didhi ya Wapalestina waishio maeneo ya Gaza




 Ripoti ya Ngwilizi yayeyuka, ushadidi wakosekana

Hakuna ushahidi uliobainika wakuweza kuwatia hatia wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini iliyo vunjwa na spika wa Bunge bi. Anne Makinda kwa tuhuma za rushwa baada ya walalamikaji kushindwa kutoa ushahidi wa tuhuma hizo.


Akiongea Bungeni leo alipokuwa akifunga vikao vya Bunge la Miswada, Spika Makinda amesema katibu Mkuu wa Nishati na Madini Mhe. Eliakimu Maswi amelidhalilisha Bunge kwa kutoa tuhuma zilizo shindwa kudhibitika kisheria, nakumtaka kuomba radhi

Aidha Spika, alimtaka Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof, Sospiter Muhongo kuwa makini nakauli anazozitoa Bungeni.


Tuhuma za Rushwa ziliiandama Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, daada ya kuwepo kwa madai kuwa Wajumbe wake waliongwa fedha na Wafanya biashara wa mafuta ilikufanikisha kupitisha bajeti ya Fedha ya Mwaka 2012/2013.


Kinacho acha Maswali nikwanini Spika haja weka wazi kama kamati ile itaundwa upya au itaendelea na kazi yake

Fainali za Epiq Bongo Star Search leo Diamond Jubilee



Leo ndio siku ya fainali ya mashiondano ya EPIQ BONGO STAR SEARCH, ambayo yatafanyika usiku waleo katika ukumbi wa Diamond Jubilee. Mshindi atapewa kiasi cha Milioni 50 taslim


haya nimashindano ya sita tangu kuanzishwa na yamekuwa chachu ya kukuza muziki nchini, kwa kuwapa nafasi wale ambao hawana uwezo wakusimama wenyewe kimuziki pamoja na kuwapa kipato kama vijana.

Kategori

Kategori