TECHNO YAJA NA SMARTPHONE YA CAMON 9, WATEJA 100 WA MWANZO WAZIGOMBANIA

 Kampuni ya simu ya Tecno yazindua Smartphone ya Camon 9 nchini Tanzania 

• Ina kamera yenye uwezo wa mega pixel 13 

•Yaja na  ofa ya GB 10 kutoka kampuni ya simu ya Vodacom kwa muda wa mwezi moja.


Meneja wa mauzo wa TECHNO Bw Fred Kadilana akielezea ubora wa CAMON c9




Kampuni ya simu ya TECNO leo imezindua rasmi nchini Tanzania smartphone mpya aina ya Camon C9 yenye uwezo mkubwa na sifa mbalimbali. Toleo hili jipya la Camon 9 linafuatia mafanikio makubwa yaliyotokana na toleo la Camon  8 lililozinduliwa mwaka jana.

Bw Fred Kadilana pia alibainisha kuwa Camon C9 ina kamera yenye uwezo wa kupiga picha 
aina ya ‘Selfie‘kwa watu wengi kwa pamoja pia kulenga kitu kilichopo kwenye mwendo kwa sekunde 0.1 na kukitoa vizuri bila ukungu .


'Tunawaletea toleo jipya la simu lenye mtazamo mpya wa kamera inayoweza kugeuka ndani na nje vilevile na pembeni ‘Alisema Bw Fred Kadilana  .




EmoticonEmoticon