ASILIMIA 80 YA WATOTO HUPOTEZA MAISHA KWA SARATANI YA JICHO NCHINI TANZANIA




Asilimia 80  ya watoto wenye umri kati ya mwaka 1 hadi 5 wanaougua saratani ya jicho nchini Tanzania hupoteza maisha kila mwaka kutokana na kuchelewa kupata matibabu ya ugonjwa huo..


Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Daktari bingwa wa saratani kutoka hosptali ya taifa Muhimbili Dr. Anna Sanyiwa amesema, bado jamii na wauguzi wa afya ngazi ya mkoa na zahanati awana ufahamu juu ya ugonjwa huo suala ambalo linapeleka waathirika wa ugonjwa huo kuchelewa kupata matibabu na baadae kuwa na upofu au kupoteza maisha..

"Takribani watoto 150 kwa mwaka hupatikana na tatizo hili, asilimia 70 hadi 80 kati yao hupoteza maisha kwa kuchelewa kupata uduma kutokana na uelewa mdogo wa ugonjwa huo" amesema Dr. Sanyiwa

Saratani ya jicho  hutokea kwenye macho yote mawili au kijo moja, ambapo dalili za awali za ugonjwa huo nikuwepo kwa weupe kwenye mboni ya jicho na kwamba ni rahisi kwa familia moja kuwa na watoto wenye ugonjwa huo kwani saratani ya jicho ni miongoni mwa magonjwa yanayo tokana na hitilafu kwenye vinasaba..


Dr. ameitaka jamii kujenga tabia ya kufanya uchungizi mapema kwani ugonjwa huo unatibika pale wanapo baini mtoto anadalili za macho kuwaka kama ya paka nyakati za usiku, kengeza, weupe kwenye kioo cha jicho, jicho kuivilia damu, kubadilika rangi au kuuma, kuwa kubwa na kuvimba.. 

Aidha, Dr. Sanyiwa amesema, ili kutoa elimu kwa umma kuelewa zaidi juu ya ugonjwa huo kutakuwa na wiki ya kimataifa ya kueleimisha na kuhamasisha jamii juu ya saratani ya jicho kwa watoto , kitaalamu ugonjwa huo ujulikana kama Retinobastoma..



EmoticonEmoticon