KATIKA
kuadhimisha kilele cha kampeni ya faidika na amana bank, benki hiyo
imewazawadia wateja wake waliobahatika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na
kujiwekea akiba zao katika benki ya
amana ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo Jijini Dare s salaam kwenye
maonesho ya viwanja vya sabasaba ndani ya banda la benki hiyo.
Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti binafsi
kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi laki tano na
kundelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi
za vifaa vya matumizi a nyumbani kama luninga, jokofu na nyinginezo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kukabidhi zawadi hizo mkurugenzi wa benki ya amana Dokta Muhsin Masoud amesema
kuwa zawadi zilizotolewa leo kwa wateja zimegharimu kiai cha shilingi milioni
tano na kuongeza kuwa benki itaendelea kuwafikia wateja wake kila siku na
kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na
mahitaji yao ili kuwapa faida iliyohalali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.
Nao baadhi ya washindi waliojishindia zawadi
wameipongeza benki ya amana kwa kuw karibu na wateja wake na kuiomba iendelee
kuonesha ushirikiano huo mzuri kwa watumiaji wote wa benki hiyo.
EmoticonEmoticon