WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Prof. Joyce Ndalichako amesema kwa mwaka huu wa fedha, wamejipanga
kuhakikisha wanafufua karakana zilizopo na kuhakikisha zinaendana na
matakwa ya serikali ya Viwanda.
Akizungumza wakati alipotembelea katika banda la VETA,
Ndalichako alisema pamoja na kufufua karakana zilizopo Veta pia
wataongeza wigo wa kuhakikisha zinakuwa nyingi na kuboreshwa.
Alisema kazi inayofanywa na VETA ni kubwa ila tatizo lipo kwenye kujitangaza ili kuweza kuuza bidhaa zao.
"Kazi wanayofanya Veta ni kubwa, lakini changamoto ipo
kwenye kujitangaza, bado hawajajitangaza katika kutoa huduma zao. Hivyo
tutashirikiana na Costech ili kuendeleza VETA na kupunguza kuagiza vitu
kutoka nje ya Nchi," alisema.
Ndalichako alisema tatizo linalosababisha la Veta kuwa
chache ni gharama zake kwani jengo moja linagharimu bil. 9, hivyo
wameshawaagiza Veta kupitia upya gharama kwa viwango tofauti tofauti ili
kupata Veta nyingi.
Aidha Ndalichako aliwapongeza Veta kwa tuzo waliyoipata na
kusema kwamba walistahili kupata tuzo hiyo kutokana na ubunifu
walioufanya kwa vitu mbalimbali ikiwamo pampu ya kamba, bustani ya
kuhama na jiko la kukaushia mboga.
EmoticonEmoticon