Baraza la sanaa Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la hatimiliki nchini zimejipanga kuzuia mauzo ya CD za wasanii wa bongo ambazo hazina chata ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), ili kuongeza kipato cha wasanii na Taifa kwa ujumla.
Wakiongea na Blog hii leo Dar es salaam, Kaimu katibu mtendaji wa BASATA bwana Godfrey Lebejo na Mtaalamu wa Tehama kutoka COSOTA wamesema zoezi hilo litaanza rasmi July 1 mwaka huu.
Kwa muda sasa wasanii wa bongo wamekuwa wakilalamika kuibiwa kazi zao, hivyo mamlaka hizi zimeamua kutumia mbinu mpya ya kudhibiti kazi hizo kwa lengo la kuinua maslahi ya wasanii.