WASHINDI WA FAIDIKA NA AMANA BANK WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO



KATIKA kuadhimisha kilele cha kampeni ya faidika na amana bank, benki hiyo imewazawadia wateja wake waliobahatika kushinda zawadi mbalimbali kutokana na kujiwekea akiba zao  katika benki ya amana ambapo makabidhiano hayo yamefanyika leo Jijini Dare s salaam kwenye maonesho ya viwanja vya sabasaba ndani ya banda la benki hiyo.




Kampeni hiyo iliyojumuisha wateja wa akaunti binafsi kujiwekea akiba katika akaunti zao kuanzia kiasi cha shilingi laki tano na kundelea kwa muda wa miezi mitatu na kuweza kupata nafasi ya kujishindia zawadi za vifaa vya matumizi a nyumbani kama luninga, jokofu na nyinginezo.





Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi hizo mkurugenzi wa benki ya amana Dokta Muhsin Masoud amesema kuwa zawadi zilizotolewa leo kwa wateja zimegharimu kiai cha shilingi milioni tano na kuongeza kuwa benki itaendelea kuwafikia wateja wake kila siku na kuwapatia watanzania wote huduma bora zenye ubunifu na zenye tija kufuatana na mahitaji yao ili kuwapa faida iliyohalali na kuwaondoa katika mzigo wa riba.

Nao baadhi ya washindi waliojishindia zawadi wameipongeza benki ya amana kwa kuw karibu na wateja wake na kuiomba iendelee kuonesha ushirikiano huo mzuri kwa watumiaji wote wa benki hiyo.


EmoticonEmoticon