Nchi ya Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa mataifa yanayoshamiri kwa biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa ajili ya utumwa wa ngono duniani.
Hayo yamelezwa leo jijini Dar es Salaam na Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya kuzuia na kupambana na biashara haramu ya bianadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Bw. Separatus Fella alipokuwa akiongea katika mkutano uliondaliwa na shirka la kimataifa la msaada wa sheria (NOLA) kwa lengo la kutoa elimu juu ya mdahara ya kusafirisha watoto.
"Tanzania ni kusudio,mkondo na chanzo cha usafirishaji wa wanawake na watoto wanaopelekwa kwenye biashara ya utumwa wa ngono katika mataifa mengine, na hii ni kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa nchini Marekani"
Bw. Fella amesema wasafirishaji binadamu wamekuwa wakitumia Tanzania kama chanzo cha kupitisha na kupata watoto wanawake wakufanya biashara hiyo na kuwa serikali itaandaa takwimu za watu walioathirika na usafirishaji huo.