NASIKIA KUITWA- ALBUM MPYA YA NJIMBO ZA INJILI IKO MADUKANI


 

huu  ni muonekano wa albam cover ya peter banzi inayokwenda kwa jina la NASIKIA KUITWA
WAWEKA PINGAMIZI WAGONGA MWAMBA TFF

WAWEKA PINGAMIZI WAGONGA MWAMBA TFF



Release No. 143
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 28, 2013


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeshindwa kusikiliza pingamizi mbili zilizowasilishwa mbele yake dhidi ya waombaji uongozi wawili baada ya kukosa sifa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF.
MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF

MAANDALIZI MKUTANO WA UCHAGUZI TFF



Release No. 142
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 27, 2013


Sekretarieti ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inaendelea na maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Uchaguzi utakaofanyika Oktoba 26 na 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

WABUNGE WATAKA UWAZI SUALA LA MADWA YA KULEVYA, LUKUVI YEYE ASISITIZA SERIKALI ITACHUKUA HATUA MPAKA IJIRIDHISHE


BUNGE la 10 mkutano wa 12 kikao cha kwanza imeanza hii leo jijini Dodoma, katika kikao hicho ambapo hoja mbalimbali zilisomwa na maswali kadhaa yaliulizwa huku suala la Madawa ya kulevya yakiwa yameshika kasi mjengoni hapo
UTAFITI WA KUPIMA UMAHIRI WA WATOTO KATIKA KUSOMA NA KUANDIKA WAJA

UTAFITI WA KUPIMA UMAHIRI WA WATOTO KATIKA KUSOMA NA KUANDIKA WAJA

Watafiti wa kujitolea elfu nane kutathmini watoto Tanzania Bara
Utafiti umelenga kupima umahiri wa watoto katika stadi za kusoma na kuhesabu

21 Agosti 2013, Dar es Salaam: Jumla ya watafiti wa kujitolea 7,980 wanashiriki katika Tathmini ya Uwezo katika wilaya 133 za Tanzania Bara. Utafiti huu unalenga kujua uwezo wa watoto katika kusoma Kiswahili, Kiingereza na kufanya hesabu. Tathmini hii ni jitahada za Uwezo kila mwaka kukagua ubora wa msingi wa elimu kwa watoto.
NSSF YALIA NA UNIVERSAL PENSION, WAWATAKA WADAU KUJIRIDHISHA KABLA YA KUIPITISHA, SASA KUJITOSA KUKOMESHA MALERIA

NSSF YALIA NA UNIVERSAL PENSION, WAWATAKA WADAU KUJIRIDHISHA KABLA YA KUIPITISHA, SASA KUJITOSA KUKOMESHA MALERIA

Shirika la taifa la hifadhi ya jamii NSSF imewatahadharisha waajiri wasiowasilisha michango ya kila mwezi ya wafanyakazi ambao wamejiunga katika mfuko huo, na kuahidi kuwachukuliw hatua za kisheria pamoja na kulipa faini ya kipindi chote ambacho hawakuwasilisha fedha hizo.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam Meneja kiongozi wa uhusiano na huduma kwa wateja Bi Eunice Chiume amesema waajiri wanatakiwa kuwasilisha michango ya wanachama wao kwa wakati na kuongeza kuwa asiye fanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria
58 WAJITOSA UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI

58 WAJITOSA UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI


Jumla ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne Nyamlani,Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace Karia.
WAHAMIAJI HARAMU WATAKIWA KUONDOKA NCHINI, WANAO WALINDA KUKIONA

WAHAMIAJI HARAMU WATAKIWA KUONDOKA NCHINI, WANAO WALINDA KUKIONA

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi Tanzania imetangaza kuanza rasmi kwa zoezi la kuwaondoa wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiingia na kuishi nchini kinyume cha sheria.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Dkt Emmanuel Nchimbi wakati akiongea na waandishi wa habari, ambapo Waziri huyo amesema kutekelezwa kwa zoezi hilo kunatokana na maelekezo kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete.
U20 WANAWAKE KUANZIA RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA DUNIA

U20 WANAWAKE KUANZIA RAUNDI YA KWANZA KOMBE LA DUNIA

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20 inaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza Kanda ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Canada.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana (Agosti 18 mwaka huu) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania imepangiwa kucheza na Msumbiji ambapo mechi ya kwanza itachezwa Dar es Salaam kati ya Oktoba 25, 26 au 27 mwaka huu.

TAMKO LA JUMUIYA YA TAASISI ZA KIISLAM JUU YA SHEIKH PONDA KUCHUKULIWA NA POLISI


GOROFA LAANZA KUPOROMOKA HUKU LIKIENDELEA KUJENGWA DAR, AANGUKIA NYUMBA,MAJIRANI WAOFIA USALAMA WAO


Sehemu ya Nyumba ya mama mmoja mkazi wa Kinondoni karibu na Hospitali ya Dr. Mvungi jijini Dar es salaam ilioangukiwa na gorofa linaloendelea kujengwa jirani na nyumba hiyo
KAMATI YAPITIA USAJILI, NGASA KUCHEZEA YANGA

KAMATI YAPITIA USAJILI, NGASA KUCHEZEA YANGA

Release No. 133
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 16, 2013

KAMATI YAPITIA USAJILI, NGASA KUCHEZEA YANGA

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepitia usajili wa wachezaji wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na kumuidhinisha Mrisho Ngasa kuchezea timu ya Yanga baada ya kukamilisha usajili wake.

Hata hivyo, Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Alex Mgongolwa imebaini kuwa Ngasa alisaini mkataba mwingine Simba (katika kipindi ambacho alikuwa na mkataba na Azam) ambapo anatakiwa kurejesha fedha alizopokea (sh. milioni 30) pamoja na fidia ya asilimia 50 (sh. milioni 15) ya fedha hizo kwa Simba.

Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha hizo.

Vilevile Kamati imepitia pingamizi zote zilizowasilishwa kuhusu usajili wa wachezaji, kukatiza mikataba ya wachezaji na kuzitaka klabu husika ziwe zimetatua masuala hayo hadi Alhamisi (Agosti 22 mwaka huu).

Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC) pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).

Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.

UCHAGUZI TFF SASA KUFANYIKA OKTOBA 27

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.

Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.

Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa  mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.

Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI KUU KUFANYIKA OKTOBA 20, NAFASI ZAWEKWA WAZI KWA WAGOMBEA

UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI KUU KUFANYIKA OKTOBA 20, NAFASI ZAWEKWA WAZI KWA WAGOMBEA



Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

NAPE AWARUDISHA MADIWANI WANNE WA CCM WALIOTIMULIWA BUKOBA



Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.
KAMATI KUTANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF LEO

KAMATI KUTANGAZA MCHAKATO WA UCHAGUZI TFF LEO


Mchakato wa uchaguzi wa kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unatarajiwa kutangazwa hii leo (Agosti 13 mwaka huu).

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Hamidu Mbwezeleni atakutana na Waaandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF saa 6 kamili mchana ambapo mbali ya mchakato utakavyokuwa anatarajia kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi huo ambao awali ulitarajiwa kufanyika Septemba 29 mwaka huu.
MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA

MAKOCHA 32 KUSHIRIKI KOZI YA FIFA COPA COCA-COLA


Makocha 32 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wanashiriki kozi ya Copa Coca-Cola inayoanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Mkufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA).

Kozi hiyo itakayomalizika Agosti 17 mwaka huu itafunguliwa saa 3 kamili asubuhi kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre na washiriki wote tayari wameshawasili Dar es Salaam. Mkufunzi wa kozi hiyo ni Govinder Thondoo kutoka Mauritius.

Washiriki wa kozi hiyo ni Ahazi Ibrahim Kasegese (Mbeya), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Asuri Msakamali (Simiyu), Bakari Khamis Kilambo (Kaskazini Pemba), Chacha Sambulo (Mara), Charles Rwezaura (Kagera), Daniel Sambala (Njombe), Dudu Haruni (Iringa) na Emmanuel Kapurata (Rukwa).

Faki Makame Haji (Kaskazini Unguja), Fatawi Khamis Sheha (Kusini Pemba), Hamisi Omary Mabo (Kigoma), Hussein Maulid (Morogoro), Issa Lugaza (Kilimanjaro), James Gaspar (Shinyanga), James Wambura (Arusha), Jomo Jackson Puccey (Lindi), Joseph Sihaba (Dodoma), Kelvin Haule (Ruvuma) na Kessy Juma Abdallah (Tanga).

Kessy Mziray (Mwanza), Menswi Mchwampaka (Kinondoni), Mohamed Abdallah Kweka (Singida), Nurdin Gogola (Temeke),  Pius Kamande (Rukwa), Ramadhan Abrahman Ramadhan (Mjini Magharibi), Ramadhan Salum Mnyoti (Manyara), Raphael Ngeleja (Geita), Samuel Edgar Maokola (Ilala), Shaweji Nawanda (Mtwara) na Vuai Abdul Haji (Kusini Unguja).

Fainali za U15 Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa zitafanyika Septemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

      SEMINA YA MAKAMISHNA YAANZA DAR, MWANZA

Semina kwa ajili ya makamishna wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) pamoja na mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa  waamuzi wote wa daraja la kwanza (Class I) wanaotaka kuchezesha VPL msimu wa 2013/2014 vinaanza kesho (Agosti 12 mwaka huu) katika vituo vya Dar es Salaam na Mwanza.

Mafunzo hayo yatakayomalizika Agosti 14 mwaka huu yatakuwa chini ya wakufunzi Leslie Liunda, Joan Minja na Riziki Majara kwa kituo cha Dar es Salaam wakati kituo cha Mwanza kitakuwa na Alfred Rwiza na Omari Kasinde.

Kwa Dar es Salaam mafunzo yatafanyika Uwanja wa Taifa wakati Mwanza itakuwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Kituo cha Mwanza kitakuwa na makamishna na waamuzi kutoka mikoa ya Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Kituo cha Dar es Salaam kitahusisha waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.

Washiriki wote wanakumbushwa kuwa ni lazima wafuate utaratibu huo wa vituo, na si vinginevyo.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA CHUMBA CHA MTIHANI, TARATIBU CHACHE SANA LAKINI HUFELISHA WENGI .....ZINGATIA HAPA


Watu wengi hufeli kwasababu ya kutofuata taratibu na sheria za mitihani, hapa baraza la mitihani limekupa mambo ya kufanya na mambo ambayo hupaswi kufanya unapokuwa katika chumba cha mtihani
 WATANZANIA WAHAMASIHWA KUCHANGIA ELIMU, UJENZI WA MABWENI 30 KWA SHULE ELFU 1500

WATANZANIA WAHAMASIHWA KUCHANGIA ELIMU, UJENZI WA MABWENI 30 KWA SHULE ELFU 1500

http://www.ibn-tv.com/wp-content/uploads/2013/07/TEA.jpg
  
Wanafunzi wanaoishi katika Geto au nyumba za kupanga hawapati nafasi ya kusoma kutokana na mazingira ambayo wanakumbana nayo katika nyumba hizo hali ambayo inapelekea wanafunzi wengi kufeli, kubeba mimba au kuacha shule.

Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa ukuzaji rasilimali wa taasisi ya elimu TEA Bi Sylivia Lupembe wakati akipokea msaada wa shilingi Millioni 5 kutoka kwa kampuni ya mafuta ya GAPCO.

“Tumetembea seemu tofauti tofauti hapa nchini tumeona, mazingira nimagumu kwani mwanafunzi analazimika kupika, kuchota maji na wakati mwingine hakuna hata umeme wakujisomea, maitaji nayo yanakuwa shida kuyapata kiasi kwamba mwanafunzi anachoka na kuacha shule” Alisema Sylvia

Bi.Sylvia liongeza kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanao ishi katika nyumba hizo ni wale wanaotoka katika familia duni, kwani kwa mwaka jana wanafunzi elfu 16 waliacha shule kwa matatizo mbalimbali kama ujauzito na umbali mrefu.

Mchango ulipokelewa leo na mamlaka hiyo utaelekezwa katika ujenzi wa mabweni 30 katika shule 1500 hapa nchini ili kuweza kuwawezesha watoto wakike kupata elimu bila vikwazo, kwani tayari wameanza na ujenzi wa bweni katika shule ya kibaigwa. 

Mamlaka ya elimu pia imewataka watanzania kuwekeza katika usafiri kwa wanafunzi ikiwa ninjia moja wapo ya kuchangia katika swala la kuendeleza elimu hapa nchini.
                                   ********************************

MKUTANO WA 31 WA SHIRIKISHO LA MABARAZA YA UPIMAJI NA TATHMINI YA ELIMU AFRIKA KUFANYIKA ARUSHA AUG. 12-16 MWAKA HUU

Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa shirikisho la mabaraza ya upimaji na tathmini ya Elimu Barani Afrika, kwa lengo la kujadili kuwepo kwa elimu ya uvumbuzi pamoja na kuinua kiwango cha walimu barani Afrika.

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini dar es salaam, Naibu Katibu Mtendaji wa baraza la Mitihani nchini Tanzania Dkt. Charles E Msonde amesema mkutano huo utafunguliwa na makamu wa pili wa Rais wa zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi huko mkoani Arusha

Mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 16 Augost mwaka huu ambapo washiriki zaidi ya 400 watahudhuria mkutano huo kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Asia na marekani.
KAULI YA PIGA TU YA MFIKISHA PINDA MAHAKAMANI NI BAADA YA KUKATAA KUFUTA KAULI HIYO

KAULI YA PIGA TU YA MFIKISHA PINDA MAHAKAMANI NI BAADA YA KUKATAA KUFUTA KAULI HIYO

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania LHRC kwa kushirikiana na wanasheria wa Tanganyika leo wamefungua kesi katika mahakama kuu ya Tanzania dhidi ya waziri mkuu Mizengo Pinda kwa madai ya kutoa kauli bungeni akiamrisha vyombo vya dola viwapige watuhumiwa wa makosa mbali mbali ambao watakuwa wakikaidi amri.

Photo: HATI YA MASHITAKA YAFIKISHWA mahakama kuu na LHRC na TLC dhidi ya waziri mkuuna mwanaheria mkuu wa serikali na wanasubiri kupangiwa jaji wa kusikiliza shauri hili na kupinga kauli ya waziri mkuu aliyoitoa bungeni kuhusu atakayekaidi amri za vyombo vya dola apigwe

Akizungumza mara baada ya kufungua kesi hiyo ya dahawa namba 24 ya mwaka 2013; mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Hellen Kijjo-Bisima amesema hatua ya wao kufungua kesi inatokana na waziri mkuu kutofuta kauli hiyo wanayodai kuwa imevunja katiba na kukiuka kinga aliyopewa na katiba hiyo.


Kwa upande wake, mkurugenzi wa taasisi ya kiraia inayojishughulisha na kufuatilia mwenendo wa bunge ya Citizens Parliament Watch Bw. Albani Markosy, amesema wanaunga mkono hatua ya LHRC na kwamba taasisi hiyo pia inakusudia kumshitaki waziri mkuu kwa madai kuwa siku hiyohiyo alitoa kauli kuwa serikali imechoka.

Shitaka hilo lenye no. 24 la mwaka 2013 dhidi ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo na Mwanasheria Mkuu wa serikali Mhe. Jaji Werema, ikifuatia kauli ya waziri huyo aliyo itoa Bungeni Dodoma katika kikao cha Tarehe 20 mwezi wa 6 2013 ambapo Waziri mkuu aliwaamuru Polisi kuwapiga wale wote watakao kaidi amri kupigwa tu.



MALERIA IMEPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 18 MPAKA ASILIMIA 10 HIVI SASA : WAZIRI WA AFYA ASEMA

MALERIA IMEPUNGUA KUTOKA ASILIMIA 18 MPAKA ASILIMIA 10 HIVI SASA : WAZIRI WA AFYA ASEMA



Hali ya maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini imepungua kutoka asilimia 18 mwaka 2007 hadi mwaka 2008 mpaka kufikia asilimia 10 kwa mwaka 2012 na 2013.

Takwimu hizo zimetolewa hii leo Jijini Dare es salaam wakati wa makabidhiano ya dawa za malaria zenye thamani ya shilingi Bilion 2 kutoka China,



Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr Hussein Mwinyi amewataka wazazi kuhakikisha familia nzima inatumia vyandarua vilivyowekwa dawa ili kupambana na ugonjwa huo, hayo ameyasema wakati akipokea msaada huo


Pia amewataka watanzania kufuata maelekezo wanayopewa na wataalam wa afya na kuongeza kuwa hali ya upatikanaji wa dawa za Malaria nchini ni nzuri lakini changamoto ipo katika suala la usambazaji kwenye zahanati zilizo katika maeneo yasiyofikika hasa vijijini

Hatahivyo serikali ya china imeendelea kuisaidia tanzania kwa dawa za maleria tangu mwaka 1968 ikiwa ni miaka 45 sasa, pia Waziri ameishukuru serikali ya china kwa ushirikiano wao ambao unachangia kwa kiasi kikubwa katika kutokomeza ugonjwa huo

MILIKI BIASHARA YAKO NA TIGO- BAJAJI ZA ZIDI KUTOLEWA

Kampuni ya simu za mkononi ya TIGO imeendelea kuwamilikisha
biashara wateja wake kupitia promosheni yake ya Miliki biashara yako ambapo kila mshindi wa Droo hiyo anajinyakulia bajaji

Tayari Bajai 10 zimegawia huku zikibaki bajaji 50 ambazo nazo zitagawia kwa washindi wa shindalo hilo, unachotakiwa kufanya nikuweka kiasi cha shilingi 1000 tu kwenye simu yako ilikuibuka mshindi
 


Hapo jana washindi wa 5 walikabidhiwa Bajaji zao huko Mbagala miongoni mwao walikuwepo wasichana 2 ambao walifurahi sana kumiliki biashara zao, William Mpinga mneja chapa wa Tigo amesema kuwa hawa niwashindi wa wiki ya pili ya shindano hilo

Washindi wa wiki ya pili ni Evelyn Elisalia Massawe mkazi wa Kimara umri miaka 22, pamoja na Usabela Edward Msemo mkazi wa Makumbusho, Khalid Jafari Gomani mkazi wa mabibo
William amesema kuna washindi wawili wapo mikoani hivyo Tigo itawafikia kwaajili ya kuwa kabidhi zawadi zao za Bajaj lengo ikiwa ni kuwawezesha wateja wao kumiliki biashara zaio na TIGO.



Kategori

Kategori