UNYAMA NCHINI: KWA MUDA WA MIEZI 6 VITENDO VYA UBAKAJI VIMEFIKIA ELFU 2965, WATOTO 394 WAMELAWITIWA HUKU WATOTO 127 NAO WAKITUPWA
Picha ya mtoto aliye zikwa akiwa hai mbeya na baba yake, hapo ni baada ya kufukuliwa na polisi |
Haki ya kuishi kwa
watanzania imeendelea kukiukwa katika kipindi cha miezi sita
iliyopita kupitia matukio mbalimbali yaliyo kinyume na haki za
binadamu ikiwa ni pamoja na Polisi kuua raia, polisi kuuawa mikononi
mwa raia, mauaji ya alibino, mauaji ya vikongwe kwa imani za
kishirikina, wananchi kuvamia vituo vya polisi, vitendo vya ubakaji.
Hayo yameelezwa katika
taarifa ya hali ya haki za binadamu nchini katika kipindi cha kuanzia
January hadi June mwaka huu iliyotolewa leo na kituo
cha sheria na haki za binadamu ambayo pia inaonesha kuongezeka kwa
vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vitendo ambavyo vinatokana
na wananchi kujichukulia sheria mkononi.
Mtafiti kutoka kituo
hicho Bwana Pasience Mlowe ndiye aliyesoma taarifa hiyo mbele
ya waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam ambapo amesema
kuwa elimu ya kutosha juu ya haki za binadamu itolewe kwa wananchi
ili kuzuia vifo visivyo vya lazima hapa nchini
Katika kipindi cha
January hadi june mwaka huu Jumla ya askari polisi 8 wameuawa
na wananchi, raia 22 wameuawa chini ya vyombo vya ulinzi,
watoto 127 wametupwa, watoto 394 wamelatiwa, vifo 597
vimetokana na raia kujichukulia sheria mkononi, vifo 303
vimetokana na imani ya kishirikina na vitendo 2965 vya
ubakaji vimeripotiwa.
Katika matukio ya kubakwa
huko ukerewe mwanza mwanaume wa miaka 40 aliyejulikana kwa jina la
Emanuel Halala alimbaka mara mbili mtoto wa miaka 8, huku mtoto wa
miaka 3 aliye bakwa na mwanaume wa miaka 30 huko mkoani Mbeya matukio
ambayo yanazidi kila ripo zinavyo zidi kutolewa
Aidha kuna mtoto aliye
zikwa akiwa hai na baba yake huko Mkoani Mbeya kwa madai ya kuachana
na mama yake mtoto huyo alikuwa wa miaka 4, lakini katika matukio
mengi hakuna hatua zozote za kisheria zilizo chukuliwa didhi ya
wahusiaka wa matukio hayo.
Shirika hili limeitaka serikali kuendesha kampeni juu ya elimu ya haki za binadamu kama ambavyo wamefaulu katika maleria na ukimwi ilikuondoa matendo ya ukatili na unyanyasaji katika jamii ya watanzania.
DR. SLAA SIMTAMBUI TENDWA, ASEMA READ BRIGADE ILIANZA TANGU 2004
Katibu mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema Dr. Wibroad Slaa amesema kuwa chama hicho akimtambui msajili wa vyama vya siasa nchini Gaji John Tendwa na kwamba wamefuta kiasi kwamba hawashirikiani nae katika kazi zao.
Dr. Slaa amezidi kusema kuwa hawata shirikiana na Tendwa mpaka atakapo ondoka madarakani lakini Dr. Slaa alisisitiza kuwa chama chake inaeshimu sana ofisis ya msajili wa vyama vya siasa na kutambua uwepo wake.
"Msajili wa vyama vya siasa anatakiwa kulea vyama vya siasa na sio kukandamiza upande mmoja, yeye hatungi sheria na taratibu zote tumefuata za kusajili chama, labda atuambie nikifungu gani atatumia kukifuta chama" Alisema Dr. Slaa.
Hayo yamekuja baada ya Dr. Slaa kufanya mahojiano na wanahabari alipokuwa kwenye ufunguzi wa kongamano la demokrasia lililo chini ya taasisi ya kimataifa ya inayojishugulisha na mambo ya kidemokrasia inayojulikana kama International Young Democrat Union IYDU.
Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkali kati ya CHADEMA na ofisi ya msajili ambapo ofisi ya msajili ilikitaka chama hicho kuachana na mpango wake wa kuunda vikundi vya ulinzi na endapo kitakaidi atakifutia usajili chama hicho.
Kuusiana na suala la Read Brigade Dr. Slaa amesema kuwa chama chake hakikuanza mwaka huu, tangu mwaka 2004 chama hicho kilikuwa na kikundi hicho hivyo kama kuna sheria inawafunga kufanya hivyo wangependa kudhibitishiwa.
Aidha kuusiana na swala la amani Dr. Slaa amesema kuwa kama serikali ingeweza kutatua matatizo ya ardhi na kuondoa kero hasa za ubadhirifu wa fedha kwa viongozi amesema amani ipo ila nimuhimu kwa serikali kuweka mazingira ambayo yataondoa malalamiko miongoni mwa wananchi.
Hatahivyo Mwenyekiti wa Bavicha Mhe. John Heche amesema mkutano huo wa kuangalia masuala ya Demokrasia katika nchi mbali mbali duniani umeshirikisha nchi zaidi ya 18 ndani ya Afrika na nje ya Afrika.
Heche amesema, yeye ndiye Mjumbe wa bodi ya vijana ya Dunia hivyo wataitumia fursa hii kuleta mabadiliko kwa vijana katika ushirikiano wao kwenye siasa, fursa za ajira pamoja na uwezo wa kuzalisha ili kuweza kujiwezesha kiuchumi.
"Bila vijana kukombolewa taifa halita inuka kikubwa ni kufanya mabadiliko na kuwapa ewezo zaidi vijana na sisi tuna wataka wafanye mabadiliko na washiriki kikamilifu katika kufanya mabadiliko" amesema Heche
Baadhi ya nchi zilizoshiriki katika mkunao huo ni Germany, Italy, Spain, Finland, Kenya, Uganda, Togo na nchi zingine nyingi.
Hatahivyo Heche amesema, chama chake kita wasilisha matatizo yote wanayo kumbana nayo kutoka kwa vyombo vya dola kama kuzuiliwa mikutano yao ya kisiasa, ukatili kutoka kwa polisi dhidi ya raia, vifo katika mikutano yao mfano David Mwangosi na mengine mengi.
Lengo la kuwasilisha hayo nikuuambia ulimwengu yanayojiri hapa nchini. amesema Heche.
KAMPUNI YA PROACTIVE YAJIPANGA KUWAAJIRI WAZAWA KATIKA MIRADI YA GESI LINDI NA MTWARA
Wadau mbali mbali wanao jishugulisha na shuguli za uchimbaji mafuta na gesi katika mkoa wa Lindi na Mtwara, hasa kampuni ya Proactive Solutions ambao wamejipanga kuwapa elimu vijana wa Lindi na Mtwara jinsi ya kufanya kazi katika makampuni ya kuchimba gesi
Shughuli za uchimbaji na uzalishaji wa Gesi na mafuta katika mikoa ya Lindi na Mtwara utagharimu kiasi cha Dola 60 za kimarekani, ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 97 za kitanzania.
Wadau hao wamejadili njia za kutumia ili kuweza kuwahusisha wazawa katika miradi yao na jinsi ya kupata eneo la kufanyia shughuli zao za uchimbaji wa gesi katika mikoa hiyo.
Corporate sales manager bi Jamila Holaki akitoa maelekezo ya bidhaa zao katika mkutano wa wadau wa Gesi na Mafuta |
Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo, Mkurugenzi
Mkuu wa TPDC Bwana Yona Kilaghane amesema kuwa lengo lao
kubwa ni kuwashirikisha wazawa katika shughuli zote za uzalishaji
na kuongeza kuwa gesi itasindikwa katika mikoa hiyo ya Lindi na
Mtwara.
Mkuu wa TPDC Bwana Yona Kilaghane amesema kuwa lengo lao
kubwa ni kuwashirikisha wazawa katika shughuli zote za uzalishaji
na kuongeza kuwa gesi itasindikwa katika mikoa hiyo ya Lindi na
Mtwara.
Mkutano huo ulioanza leo na kumalizika kesho jijini Dar Es Salaam utafungwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo.
BENKI YA NMB YAFADHILI MAAFISA MAENDELEO WA VIJANA NCHI NZIMA
Waziri wa Habari, Vijana, Tamaduni na Michezo Dkt. Fenera Mkandara akiongea katika semina hiyo |
Benki ya NMB imefadhili semina kubwa iliyohusisha maafisa
maendeleo wa vijana kutoka nchi nzima kwa lengo la kujadili maendeleo ya vijana
kuanzia ngazi ya halmashauri ilikuweza kuimarisha utendaji kazi kwa vijana wa
mikoa na Wilaya
Semina hiyo ya siku mbili ilifanyika katika kumbi za uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo
Mhe. Dkt Fenera Mukangara ambaye naye aliishukuu Benki hiyo kwa ufadhili mkubwa
na kujitolea ili kufanikisha semina hiyo.
Meneja mahusiano wa NMB Josephine Kulwa akiongea katika semina hiyo |
JESHI LA POLISI LA KANUSHA KUMLENGA MNYIKA NA BOMU, WAKAMATA KIWANDA CHA SILAHA DAR, NA MAJAMBAZI SUGU 8
Picha hii ahiusiani na habari hii |
Jeshi la Polisi
kanda maalum ya Dar es salaam, hii leo limekanusha tuhuma kuwa Bomu
lililo lipuka katika mkutano wa Chadema uliofanyika kwenye viwanja
vya Sahara Mabibo siku ya Jumamosi tarehe 21/07/2013 halikuwa
limemlenga Mhe. John Mnyika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kama
taarifa za awali zilivyo eleza
Akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi
kanda maalum ya Dar es salaam DCP Ally Mlege amesema taarifa zimekuwa
zikipotoshwa juu ya tukio hilo, lakini ukweli ni kuwa bomu hilo
lililipuka kwa bahati mbaya na hakuna mtu yeyote aliye jeruhiwa
Bomu hilo lililipuka
kwa bahati mbaya baada ya Askari no. E.5340 D/CPL JULIUS ambaye
alikuwa ndani ya gari la Polisi lenye namba PT 1902 alipokuwa
anasogeza Box lenye mabomu ya mamchozi ya kurusha kwa mkono ndipo
Bomu hilo likalipuka.
Hatahivyo Chadema
hawakuruhusiwa kufanya mkutano eneo hilo lakini baadae waliondoka kwa
amani katika eneo hilo bila madhara yeyote kujitokeza na kuamia
katika maeneo ya Ubungo na kumalizia mkutano wao. Amesema DCP Ally
Mlege
KARAKANA
YA KUZALISHA SILAHA MAENEO YA
KAWE MZIMUNI, NA MAJAMBAZI 8 WANASWA NA
RISASI 56
Majambazi 8 wamekamatwa na Polisi wa
kanda maalum ya Dar es salaam, wakiwa na silaha 5 pamoja na kiwanda
cha kienyeji cha kutengenezea silaha na vifaa mbalimbali vya kufanyia
uhalifu maeneo ya Kawe Mzimuni, kiwanda hicho kilikuwa chini ya
Charles Francis Masunzu mkazi wa eneo hilo
wengine ni Matula Rashid dereva
pikipiki mkazi wa mbezi, Omary Hassan kinyozi mkazi wa Mabibo, Mardha
Muhagama mkazi wa Mbezi Kibanda cha mkaa na Mwasiti Maulidi mkazi wa
mbezi msumi, watuhumiwa walikuwa na SMG yenye usajili no.02704 ikiwa
imekatwa kitako na risasi 20 ndani yake.
Bunduki hiyo SGM no.02704 aliporwa
Askari Polisi Wilaya ya Rufiji akiwa anasindikiza magari toka
ikwiriri mkoani pwani mwaka 2007, majambazi hayo wametumia silaha
hiyo kwa takribani miaka 7.
Aidha baada Charles Francis Masunzu
mkazi wa mzimuni baada ya kufanyiwa upekuzi alikutwa na Shortgun
moja no. 2539 double bore, Reffile 3 iliyo sajiliwa kwa no. TZ CAR
42871, Reffile 3 iliyosajiliwa kwa no. CAR83744,Reffile 3 ikiwa
imefutwa namba, Pistol KJW Works, pamoja na mitutu 5, pingu,risasi 36
na maganda 17 ya risasi, mkebe wa Short gun, funguo mbali mbali,
misumeno ya vyuma na vielelezo zingine vingi vinavyo husiana na
uhalifu
Pia katika msako mwingine maeneo ya
Kijitonyama Polisi walikamata Maragi ya wizi 5 Engine 3 za magari,
vipande vya magari yaliyo katwa huku wezi 5 wamagari wakitiwa
nguvuni.
Wahusika katika uhalifu huo ni Godlove
Damasi, Anna Kway, Sharif Ahamad, Salehe Abdala Ally, pamoja na
Nassoro Mohamed
AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA MAMIA KUAGA MIILI YA WANAJESHI 7 WA TANZANIA WALIOUWAWA DARFUR
Rais wa Tanzania Jakaya Kiwete amewaongoza maelfu ya waombolezaji katika kutoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa kwa kushambuliwa na waasi Darfur nchini Sudan walipokuwa wakilinda amani.
“Rais
Kikwete amesema nchi ya Sudana ifanye uchunguzi wa haraka juu ya vifo
vya wanajeshi hao ili kubaini ni kina nani wamehusika katika
shambulio hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa” Alisema Rais Kikwete
na kuongeza kuwa Wanajeshi wetu walienda kuwalinda ili waweze kuwa na
amani katika nchi yao na sivinginevyo. Alisema
Miili ya wanajeshi hao iliwasili jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, na kupokelewa na mamia ya waombolezaji walioongozwa na makamu wa rais Dokta Gharib Bilal, katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya kijeshi ya Lugalo.
Zoezi la kuwaaga wanajeshi hao imefanyika katika uwanja wa makao makuu ya jeshi eneo la Upanga jijini DSM, ambapo wanajeshi wawili kati yao watasafirishwa visiwavi Zanzibar kwa mazishi
Wanajeshi hao ni pamoja na Sajenti Shaibu Shehe, Corporal Oswald Chaulo, Corporal Mohammed Ally, Corporal Mohammed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Fortunatus Msofe na Private Peter Werema.
Rais wa Sudan Omar Al Bashir alimhakikishia Rais Jakaya Kikwete kuwa wote waliohusika katika kuwashambulia wanajeshi hao na kuwaua watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Rais Bashir alitoa ahadi hiyo
wakati wa mazungumzo na Rais Kikwete na kuongeza kuwa anaamini
waliohusika na mauaji hayo walikuwa wahalifu na kuwa lazima wasakwe.
SHOW LOVE “NELSON MANDELA INTERNATIONAL DAY”
Wananchi wa Afrika kusini hii leo wame sherehekea siku ya kuzaliwa kwa Raisi wao wa kwanza bwana Nelson Mandela kwa kufanya shuguli mbalimbali za kijamii.
Siku hii ya mandela ni miongoni mwa siku kuu za kidunia mbayo watu wanahimizwa kutoa kwa kusaida jamii inayo wazunguka na kufanya mema.
Maeneo mbalimbali ya Miji mkubwa nchini Afrika Kusini imepambwa kwa mabango ya picha za raisi huyo kama ishara ya kumuenzi
Wananchi wa Afrika kusini wametumia dadika 65 kwaajili ya kusaida watu mbalimbali
MIILI 7 YA WANAJESHI WALIO UWAWA DARFUR KUWASILI NCHINI HAPO KESHO
Miili ya wanajeshi 7 waliofariki huko nchini Sudan - Darfur huenda ikawasili hapo kesho baada ya kupewa heshima za mwisho na majeshi yanayolinda amani nchini humo hii leo
Habari zilizo andikwa na mtandao wa UNAMID zinasema tayari miili hiyo imeagwa tangu majira ya mchana na kuanza safari ya kuletwa nchini kwa mazishi
Hatahivyo taarifa ambazo hazijathibitishwa na Blog hii kwani jitihada za kuwasiliana na msemaji wa jeshi ziligonga mwamba baada ya kutopewa ushirikiano wa kutosha na simu kuita bila kupokelewa
Taarifa zinasema kati ya wanajeshi 14 waliokuwa mahututi 4 tayari wamefariki Dunia....... Blog hii itakujuza zaidi kadri habari zitakavyo kuwa zinatufikia = Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
Habari zilizo andikwa na mtandao wa UNAMID zinasema tayari miili hiyo imeagwa tangu majira ya mchana na kuanza safari ya kuletwa nchini kwa mazishi
Hatahivyo taarifa ambazo hazijathibitishwa na Blog hii kwani jitihada za kuwasiliana na msemaji wa jeshi ziligonga mwamba baada ya kutopewa ushirikiano wa kutosha na simu kuita bila kupokelewa
Taarifa zinasema kati ya wanajeshi 14 waliokuwa mahututi 4 tayari wamefariki Dunia....... Blog hii itakujuza zaidi kadri habari zitakavyo kuwa zinatufikia = Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
MNYIKA AMJIBU MGIMWA TOZO ZA SIMU, APINGA KUSEMA WABUNGE WALIPITISHA
Alia na wananchi kuongezwa mzigo mkubwa wa kodi, na kutoa hatua 7 ambazo amemtaka waziri wa fedha kutolea ufafanuzi huku akieleza jinsi anavyo hamasisha wananchi kupinga tozo hizo
> Ataka maandamano,
> Sahihi ya wananchi wanao pinga kupandishwa kwa tozo hizo,
> Wabunge waliopitisha sheria hiyo watajwe,
> Wananchi wapewe taarifa kamili ilikuwaje sheria hiyo ikapitishwa.
Habari kamili
KAULI YA WAZIRI WA FEDHA KUHUSU KODI YA LINE ZA SIMU NI KIELELEZO CHA UDHAIFU WA SERIKALI NA UZEMBE WA BUNGE; NIANDIKIE SASA KUHUSU HATUA ZA KUCHUKUA JUU YA SUALA HILI KUPUNGUZA MZIGO WA GHARAMA ZA MAISHA KWA WANANCHI
Katika kipindi cha Hot Mix cha EATV muda mfupi uliopita Waziri wa Fedha amesema kwamba mawazo ya kutoza elfu moja kwa mwezi kwenye kila laini ya simu ni ya wabunge.
Kauli inayokaribiana na hiyo imewahi kuandikwa pia na Naibu Waziri wa Wizara yenye dhamana na sekta mawasiliano kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni. Baadaye alifuata Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na sasa waziri mwenyewe. Mwaka 2012 nilitahadharisha kuhusu udhaifu wa Rais (na Serikali) na uzembe wa Bunge katika masuala yanayohusu maandalizi ya bajeti, hususan kutozingatiwa kwa mpango wa taifa wa maendeleo na ongezeko la mara kwa mara la gharama za maisha kwa wananchi. Kwa kauli hizi za Serikali udhaifu na uzembe huo unaendelea kujihidhirisha.
Kauli hizi za Serikali ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge.
Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Serikali ijitokeze itaje kwa majina na wabunge gani hasa walitoa mawazo hayo. Mimi sijawahi kutoa wazo hilo wala kuliridhia. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwenye Hotuba yake juu ya Muswada wa Sheria ya Fedha ilipinga pendekezo hilo lililokuwepo katika jedwali la marekebisho lililowasilishwa na Wizara ya Fedha. Katika kuhakikisha kwamba kifungu hicho hakipitishwi, niliwasilisha jedwali la marekebisho ya sheria kutaka kifungu hicho kiondolewe katika muswada wa sheria ya fedha na marekebisho yake yaliyowasilishwa na Serikali.
Hata kama ikiwa ni ukweli kwamba wazo hilo ni la baadhi ya Wabunge (ambao ni muhimu wakatajwa kwa majina), Serikali inayokwepa kutetea maamuzi ambayo Serikali yenyewe imeyaunga mkono inadhihirisha kwamba imechoka na imepoteza uhalali kwa kimaadili kwa kushindwa kukubalika mbele ya wananchi wake yenyewe (illegitimate government) .
Mamlaka na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa katiba ibara ya 63 ni kuishauri na kuisimamia Serikali. Katika kutekeleza mamlaka hayo, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi na chenye mamlaka pia ya kutunga sheria na kupitisha bajeti ya nchi. Hata hivyo, ibara ya 99 ya Katiba imeweka mipaka kwa mamlaka hayo ya Bunge inapokuja suala la kutunga sheria ya fedha kama hii iliyoongeza mzigo wa kodi kwa wananchi. Mamlaka hayo yamewekwa kwa kiwango kikubwa mikononi mwa Rais kupitia Waziri wake mwenye dhamana.
SOMA ZAIDI HAPA
KAULI YA WAZIRI WA FEDHA MHE. WILLIUM MGIMWA AMBAYO ANAPINGWA NA MNIKA
KULETWA KWA MIILI YA WANAJESHI 7 WATANZANIA WALIOFIA DARFUR BADO HAIJAJULIKANA
Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limesema linasubiri matokeo ya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa juu ya kikundi kilichohusika pamoja na mazingira ya mashambulizi yaliyosababisha kuuawa kwa wanajeshi 7 wa Tanzania wanaolinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Hot Mix kinachorushwa na EATV, msemaji wa jeshi hilo Kanali Kapambala Mgawe amesema jeshi linasubiri ripoti ya umoja wa mataifa ili kuamua ni lini miili ya marehemu italetwa nchini,
Aidha amekanusha juu ya taarifa zilizo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jeshi hilo limetoa majina ya wale waliofariki katika shambulio hilo
"Kuna baadhi ya majina tume yaona kwenye vyombo vya habari lakini sisi hatukutoa majina ya wale walio uwawa, Jeshi lina utaratibu wake katika matukio kama haya sijui haya majina nani kawatajia, hivyo siwezi kusema ni nani ameuwawa kwani majina bado hayaja wekwa hadharani" amesema
Kanali Kapambala Mgawe amesema, utaratibu wa kijeshi nikuwa mtu anapo uwawa, nilazima ndugu wakaribu waambiwe kwanza na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo nasio kutamka kwenye vyombo vya habari kwani inaweza kusababisha matatizo mengine.
Mtu amefiwa na mtuwake wa karibu wewe unatoa jina lake, je atajiskiaje kusikia kwenye vyomboi vya habari bila kuambiwa kwa utaratibu unao faa, Alihoji na kueleza kuwa kilicho tendeka sio utaratibu mzuri kwani wao ndio walipaswa lutoa taarifa kwa ndugu wa marehemu. Alisema Kanal Kapambala
Jumla ya wanajeshi 875 walikuwa nchini humo tangu mwezi February mwaka huu, kwa maana hiyo walio hai mpaka hivi sasa ni 868 (ukitoa 7 waliofariki) na miongoni mwa hao walio hai 14 walijeruhiwa na wapo katika hali mbaya
.Wanajeshi hao walishambuliwa wakati wakisindikiza msafara wa waangalizi wa amani wa Umoja wa Mataifa, Tangu Tanzania ianze kupeleka majeshi yake mwaka 2007 huko Darfur ni mara ya kwanza kwa Jeshi letu kupoteza watu wake. Pole Tanzania Pole kwa ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.
CCM YA BURUZWA NA CHADEMA ARUSHA, WASHINDA KATA ZOTE VIONGOZI WA DINI NAO WAPONGEZA UTULIVU ULIOPO
Viongozi
wa Madhebu ya Kidini mkoani Arusha wameeleza kuridhishwa na hali ya
amani iliyotawala katika uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata za
Jiji la Arusha na kuzisifu vyombo vya dola pamoja na wananchi kwa
kudumisha amani na kuepuka vurugu zisizo za lazima.
Habari
zilizo ifikia Blog hii toka mkoani humo zinasema, Viongozi wa kidini
Wakizungumzia hali hiyo, kutoka katika madhehebu tofauti wamesema,
amani itaendelea kuwepo kwani utulivu ulioonyeshwa na vyombo vya dola
pamoja na wakazi wa Arusha unapaswa kuendelea katika chaguzi
zijazo.
Naye
Mkurugenzi wa kituo cha Taarifa kwa wananchi Deus Kibamba amesema
watendaji wa serikali wakiweza kusimamia demokrasia kwa kiwango
hicho, hakuna vurugu wala umwagaji wa damu utakaotokea hapa nchini.
Kwa
upande mwingine, Wanachama wa Chama cha Mapindizi wamewataka viongozi
wa Chama
hicho kwa Wilaya ya Arusa kujithamini kutokana na anguko walilolipata
katika Uchaguzi huo, ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo
kimeshinda katika kata zote nne.
Chama
cha Chadema kimethibitisha ushindi wake baada ya kutetea kwa kishindo
kata zake nne kwenye mkoa huo, Uchaguzi huo ulikuwa ukisubiriwa kwa
hamu na ulikuwa unachukuliwa kama kipimo cha siasa komavu mkoani
humo
Chadema
kimeongoza katika vituo vyote136 vya kupigia kura katika Kata za
Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Matokeo
hayo yameonyeshwa kulingana na idadi ya vituo katika kata mbali mbali
ambapo Matokeo ya Uchaguzi katika kata hizo nne na vituo 136 yalikuwa
kama ifuatavyo:
Kata
ya Elerai CHADEMA
kura
2,047 CCM kura
1,471
Kata
ya Themi
CHADEMA
kura 674
CCM
kura 326
Kata
ya Kaloleni CHADEMA
kura
1,470
CCM
kura
330
Kata
ya Kimandolu CHADEMA
kura 2,761
CCM
kura 1,163
Baadhi ya Kata
hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua
wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John
Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni
MAKAMBA AOMBA SERIKALI IAONDOWE VIKWAZO VIJANA
Serikali
imetakiwa kuhakikisha vijana wanapewa ewezo wa kutumia vipaji vyao
kujiajiri na kuajiri wengine kwa kuwaondolea vikwazo vinavyo
wakabili bindi wanapo taka kuanzisha biashara au kupata mkopo katika
mabenki hapa nchini.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mhe. January Makamba wakati wa uzinduzi wa tuzo za vijana chini ya miaka 30, ambapo Mhe. Makamba amesea, kujituma na kutumia fursa kwa vijana inategemeana na vikazo mbavyo kuna muda wanakumbana navyo na kuitaka serikali kuondoa vikwazo hivyo
“kijana
anataka kusajili biashara yake lakini kuna mlolongo mrefu sana ambao
unafanya anakata tamaa, au anahitaji mkopo benki lakini wanahitaji
hati ya nyumba huyu kijana anatoa wapi nyumba? Sasa kama serikali
ikiangalia hivi nadhani vijana wataweza kuonyesha uwezo wao”Alisema
Makamba
Aidha,
alisema Mfumo wa elimu wa nchi yetu nao urekebishwe iwe elimu ambayo
itawapa vijana uwezo wa kutatua matatizo yanayo mkabili, kushirikiana
na wengine na sio elimu tu ambao bado itamfunga kuendana na dunia ya
sasa. Alisema
Mhe.
Makamba amesema katika Bunge lijalo Serikali imeandaa muswada ambao
utawasilishwa juu ya kuwepo kwa Baraza la Vijana kwaajili ya
kushugulikia matatizo ya vijana kama ajira, elimu na baraza hilo
liwepo kisheria ili liweze kuwa na nguvu
“baadhi
yetu tumekuwa tukipenda bara hili lianzishwe haraka kwani litao tao
majibu kwa matatizo ya vijana na serikali imejipanga vyema
kuhakikisha kuwa bunge lijalo tunajadili nini cha kufanya” Alisema
Naye
Mkurugenzi mkuu wa Youth for Africa bwana Awadhi Malasi amesema
Taasisi yake inawakumbuka sana vijana kutokana na mchango wao katika
jamii hivyo tuzo hizo zitawapa motisha vijana wengine kufanya vyema
zaidi. Amesema
Awadhi
amesema hii ni mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kutoa tuzo hizo hapa
nchini lakini kila mwaka kutakuwa na mabadiliko juu ya tuzo hizo
kwani hata mikoani na watapewa fursa ya kushiriki
Kwa
kupata washindi katika tuzo hizo unapiga kura kupitia mtandao wao ambao ni
http://www.youthawards.or.tz au kwa njia ya simu
andika YOA acha nafasi kisha tuma kwenda 15584. Tuzo zitatolewa
tarehe 17/8/2013.
A NEW CAR DESIGNED IN IRINGA TANZANIA
Keneth Mwangoka akiwa ndani ya Gari lake |
Gari hilo lililo lililoundwa na Vyuma chakavu pamoja na mbao na urembo mwingine wakawaida kutengeneza Bodi ya gari hiyo. Akiongea na Blog hii mmiliki wake bwana Keneth amesema kwa mtu yeyote atakaye hitaji kutengenezewa gari kama hiyo wawasiliane kwa simu no. 0754 005004
Gari hiyo imeundwa kwa kutumia Engine ya Toyota, matairi ya kawaida huku spea zingine zikiwa ni za dukani na ameiundwa kwa muda wa miezi 6. Lengo la Keneth ni kuwataka vijana hasa ambao hawana ajira kuwa wabunifu kuliko kukaa tuu mitaani
SHILINGI BILLIONI 160 KUKUSANYWA KWA MWAKA KUPITIA TOZO ZA LAINI YA SIMU YA KILA MWEZI
>TOZO YA LAINI KWA MWEZI WABUNGE NDIO WALIPITISHA
>YADAIWA ITAPATIA NCHI BILIONI 160
>BILIONI 231 NAZO ZATOLEWA NA SEEDEN,
>NA ADB BANK YAIKOPEHA TANZANIA BILIONI 286
Serikali imeendelea kusisitiza
kodi ya Line za simu ambayo itakatwa kila mwezi kwa watumiaji wa simu nchini
Akijibu swali lililo ulizwa na mmoja wawaandishi wa habari katika mkutano
wa kusaini mkataba na nchi ya Sweeden, Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa
amesema serikali ili chukua uamuzi huo baada ya wabunge ambao ni wa wakilishi
wa wananchi Bungeni kukubali kupitisha Bungeni swala hilo
“Wananchi wana lalamika lakini wawakilishi wao ambao ni wabunge
ndio walipitisha aina hii ya tozo hivyo serikali inajipanga kuanza mchakato wa
kupata fedha hizo ili kuweza kuongeza kipato”Alisema
Aidha Dr. Mgimwa amesema kuwa serikali itapokea shilingi
Billioni 160 kwa mwaka kutokana na kukata tozo hizo”Amesema
Akitoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo Dr. Mgimwa amesema
kuwa fedha hizo zitatumika katika kusaidia maitaji ya jamii kama vile
Hospitali, mashule na barabara”Alisema Dr. Mgimwa
Hii inamaana kama kila mwaka mmiliki wa line moja atatozwa
shilingi Elfu 12 hali ni tete kwa wale wanao miliki laini zaidi ya Mbili.
Tozo hiyo itaanza kukatwa rasmi kuanzia Julai 2013 mwezi huu
Wananchi wengi wamezidi kulalamikia tozo hizo huku baadhi ya wabunge nao wakidai kuwa swala la laini za simu aikuwekwa Bungeni kujadiliwa kwa wazi
Tozo hiyo itaanza kukatwa rasmi kuanzia Julai 2013 mwezi huu
Wananchi wengi wamezidi kulalamikia tozo hizo huku baadhi ya wabunge nao wakidai kuwa swala la laini za simu aikuwekwa Bungeni kujadiliwa kwa wazi
BILLIONI 231 KUTOKA SWEEDEN KUENDELEZA MITAMBO YA UMEME NA
UCHUMI
Serikali ya Tanzania imepokea shilingi bilioni 231 kutoka
serikali ya Sweden kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali nchini
Waziri wa Fedha Dr. William
Mgimwa amefafanua kuwa mikataba
miwili iliyotiwa saini leo ni kwa ajili ya matumizi tofauti ambapo mkataba wa
kwanza wa shilingi bilioni 202 unalenga kuongeza nguvu katika kuhamasisha
ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini
Mkataba wa pili wa jumla ya shilingi bilioni 129 utaelekezwa
katika shughuli za ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Hare jijini
Tanga, nakuongeza megawati 21 katika umeme wa taifa
“Hivi sasa hare inazalisha megawati zisizo zidi tisa 9, nakuwa
serikali imeamua kuongeza uzalishaji wake kwani kuna upatikanaji wa maji ya
kutosha katika eneo hilo” amesema.
Dr. Mgimwa amesema, Hii ni sehemu ya jitihada za serikali
kufanyia kazi vipaumbele vya mwaka huu wa fedha 2013/2014 ambapo kipaumbele cha
kwanza ni miundombinu ya Nishati ya umeme na barabara.
Serikali ya Sweden imekuwa
mstari wa mbele miongoni mwa washirika wa maendeleo nchini kusaidia ukuaji wa sekta
ya nishati hususani Umeme hapa nchini
BARABARA YA ARUSHA-HOLILI KUJENGWA AUGUST 2013 MAPAKA DEC 2018
Barabara ya Arusha-Holili mpaka Taveta na Voi nchini Kenya
inatarajiwa kuanza ujenzi wa kupanua barabara hiyo baada ya Tanzania kusaini
mkataba wa mkopo wa shilingi Billioni 286 kutoka Banki ya maendeleo Afrika AFDB
Akiongea na waandishi wa Habari hii leo jijini Dar es salaam,
Waziri wa Fedha Mhe. Willium Mgimwa amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo yenye
urefu wa kilometa 42, utaanza August mwaka huu na kumalizika December 2018.
Aidha, Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo itasaidia usafiri wa
watu zaidi ya Laki 5 na 84 kwa upande wa Tanzania ikiwa pamoja na kurahisisha
usafiri kwa watalii watakao tembelea mkoa wa Arusha na Kilimanjaro
Tanzania itarudisha mkopo huo baada ya Miaka 40 lakini mda wa
kuanza kulipa mkopo huo ni miaka 5 ijayo, katika kurudisha fedha hizo Tanzania
itatoa Asilimia 4.7 huku Kenya ikitoa Asilimia 5.9.
WANAFUNZI EFU 33,683 KUJIUNGA KIDATO CHA TANO2013, 530 WAPELEKWA VYUO VYA UFUNDI, HUKU LAKI 397,437 WAKISOTA MTAANI
Jumla ya wanafunzi 34,213 sawa na asilimia 18.1 ya waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 kwa madaraja ya I – IV wamechaguliwa kuingia kidato cha tano na vyuo vya ufundi pamoja na taasisi ya menejiment ya maendeleo ya maji kwa mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 2,790 sawa na asilimia 8.9 ikilinganishwa na mwaka 2012.
Aidha Jumla ya wanafunzi 33,683 sawa na asilimia 18.1 ya waliofaulu wakiwemo wavulana 23,383 na wasichana 10,300 wamechaguliwa kuingia kidato cha tano kwa mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.15 ikilinganishwa na mwaka 2012.
Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe Philip Mulugo ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini DSM na kusema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu ni wa masomo (Tahasusi) ya Sayansi.
Mhe. Mulugo amesema wanafunzi wa some kwa bidii bila kujali aina ya masomo anayosoma, pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa kike kujiamini kuwa wanaweza masomo yote, Alisema
Idadi ya wanafunzi wote waliojiunga na vyuo vya ufundi imepungua kutoka 564 mwaka 2012 hadi 530 mwaka 2013 ambapo wavulana ni 416 wasichana wakiwa 114 tu. Lakini hilo niongezeko kubwa kwa upande wa wasichana ambao kwa mwaka huu wamechaguliwa 144 tofauti na mwaka jana ambao walikuwa 47 tu.
Kuhusiana na baadhi ya wanafunzi ambao tayari wame kwisha anza masomo ya kidato cha tano katika shule binafsi, Mhe Mulugo ametoa ufafanuzi kuwa shule za serikali hufunguliwa Julai ambapo waliochaguliwa watatakiwa kuripoti tarehe 29 Julai
“Wanafunzi ambao tayari wameanza kusoma masomo ya kidato cha tano katika shule binafsi na wamefauli katika shule za serikali ni uamuzi wao kuamua kama waendelee na shule za binafsi au warudi kujiunga na shule za serikali ila wasiihusishe serikali” Amesema
Matokeo
haya yanaonesha kuwa, shule za serikali zitakumbwa na upungufu wa
wanafuzi takribani 10,097 wengi wao wakiwa ni wa masomo ya sanaa.
Kwa taarifa ya Waziri Jumla ya Wanafunzi Laki 397,437 hawacha chaguliwa kujiunga na masomo ya juu, na kati ya hawa kuna waliopata daraja la IV na 0 ambao ndio wengi kuliko waliochaguliwa
VIJANA WALILIA KUTOPEWA BARAZA LAO, KUJADILI RASIMU YA KATIBA
Vijana wote nchini
wametakiwa kujiunga bila kujali itikadi zao ili kuweza kupigia kelele
kuwepo kwa baraza la taifa la vijana litakalo jadili mambo ya Rasimu
ya kuundwa kwa katiba mpya hapa nchini
Akiongea na
waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, mwenye kiti wa
jukwaa la vijana Tanzania bwana Fahami Matsawilly amesema kuwa tunaomba ibara ya 43 itamke wazi kuwa
kila kijana anao wajibu wa kushiriki shuguli za kijamii na maendeleo
kwa ujumla
“Vijana wote
tunaombwa kuungana bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kidini,
kabila na elimu ili kuweza kutetea changa moto zinazo tukabili hapa
nchini
Hayo yote yamekuja
baada ya JUVITA kubaini kuwa matatizo yanayowakabili vijana kama
Ukosefu wa ajira, makundi kama yale ya Machinga, dereva wa bodaboda
na vijana wanao fanya kazi majumbani na makundi mengine ni lazima
wawe na chombo kitakacho wa wakilisha kwenye vyombo vya maamuzi ya
katiba mpya
Pia amewataka vijana
kupeleka mapendekezo yao kwa wawakilishi wa mabaraza ya katiba ili
ibara ya 43 iweze kufanyiwa marekebisho
“Cha ajabu baraza
la taifa la vijana halimo kwenye rasimu ya katiba mpya, wakati nchi
nyingi zenya mabara za ya taifa ya vijana, kwa nini Tanzania hiyo
nafasio hakuna” Alisema
Baadhi ya nchi
ambazo zina baraza la vijana linaloshigulikia matatizo ya vijana ni
pamoja na Costasica, Slovenia, Rwanda , Uganda pamoja na Kenya na
nchi zingine nyingi
Uundwaji wa Katiba
mpya umefikia katika hatua za mabara ya Rasimu ya katiba mpya ambapo
mabaraza hayo yataanza kukaa kuanzia Ijumaa ya wiki hii tarehe 12.
Subscribe to:
Posts (Atom)