Serikali inatarajia
kuendesha zoezi la uhakiki wa Watumishi wa umma kote nchini kwa siku
14 kwa kutumia mfumo wa kielektroniki ili kuondoa watumishi hewa na
wenye utambulisho danganyifu.
Akiongea na waandishi wa
habari hii leo jijini Dar es salaam, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais
menejmenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. Angela Kairuki
amesema zoezi hilo litahusisha uchukuwaji wa alama za vidole, vyeti
vya elimu, cheti cha kuzaliwa na hati ya malipo ya mshahara, Hati ya
kusafiria, kadi ya mpiga kura na Kitambulisho cha Kazi.
Mhe. Kairuki amesema lengo
nikuuimarisha mifumo ya usimamizi wa raslimaliwatu na mishahara
kwakutumia kanzi data ya utambulisho wa Taifa ambapombo zoezi hilo
litaendeshwa na mamlatka ya vimbulishi vya taifa na kwamba zoezi hilo
litaanza Octoba 3.2016.
“Tuna watumishi wa
serikali Laki 5 na elfu 61 lakini uhakiki huu utatupa fursa ya
kuwatambua zaidi watumishi wetu na zoezi hili litausisha watumishi
waote wakiwepo Polisi lakini upande wa Majeshi (JWTZ) wao
wataandaliwa utaratibu wao wakati mwingine” , amesema
Aidha Mhe Kairuki
amewataka Watumishi kote nchini katika Wizara mbalimbali, Idara za
serikali zinazojitegemea, Tawala za Mikoa na mamlaka za serikali za
mitaa, Wakala za Serikali, Taasisi na mashirika ya Umma ambapo zoezi
zitahusisha na watrumishi wa serikali kwa upende wa Zanzibar.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa
TEHAMA kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Bwana Mohamed
Hamisi amesema tayari wameandaa watumishi 400 kwaajili ya zoezi hilo
kwa nchi nzima ambapo BVR zaidi ya 5000 zitatumika.