Archive for December 2015
Kundi la kwanza ni ~ Wanandoa ambao tayari ni mume na mke au wanaishi pamoja kama wanafamilia.
Kundi la Pili ni ~ Walio kwenye Uchumba ambao hawaishi pamoja au hawaja oana lakini wanatarajia kuingia katika ndoa.
Swali langu katiya makundi hayo mawili ni kundi lipi linauhalali wa kuwa huru na simu ya mkononi ya mpenzi wake, bila kujali kama ni mwana mke au mwanaume.
Swala la simu miongoni mwa wapenzi huwa lina utata na matatizo mengi, Campasvision imefanya utafiti katiya makundi hayo mawili kwa kuuliza maswali baada ya kubaini kuwa kuna kundi moja linaamini lina uhalali wa kuwa huru na simu ya mpenzi wake, huku kundi lingine likidai akuna uhalali wakuwa huru na simu ya mpenzi wako kwa sababu tofauti tofauti ambazo walizitaja
Tukianza na kundi la kwanza ambalo kila mtu anamtegemea mwenzake, yani mume na mke kwani nikama familia au umoja wenye mambo mengi yanayo fanyika kwa pamoja na kuwa jumuisha pamoja, tusema nifamilia pengine yaweza kuwa na watoto au lah.
Wengi wa watu niliofanya nao mahojiano katika kundi hili ambao wote walikuwa walio oa na kuolewa, kundi hili walisisitiza juu ya kuwa huru na simu ya mwenza wako kwa sababu nyingi na zilizo kuwa na msingi kabisaa,
Hakuna aliye kuwa na sababu ya kwa nini mke wake au mume wake asishike simu yake, aidha kwa idhini au bila idhini kutokana na kuwa tayari wao nifamilia moja mipaka kama hiyo aijengi familia. Na endapo kutakuwa na mtu anamkatazia mke au mume wake kushika simu yake ya mkononi basi siyo mwaminifu katika mapenzi yake na kwakuwa simu ndio mficha siri zetu basi wengi wanahofia kuumbuka, ilikuji ficha basi anaamua kuwa mkali kwenye simu yake.
Kundi la Pili ni la wale wachumba ambao wanatarajia kuingia katika ndoa, ila bado kila mtu anakaa peke yake au anakaa na wazazi wake. majibu niliyo pata toka kwenye kundi hili kwa wasichana na wavulana halikuwa la moja kwa moja, kwamba ninani mwenye uhalali wa kushika simu ya mwenza wake kati ya kundi la kwanza au kundi la pili
Wengi wa kundi hili waliwajibia waliokwenye ndoa kuwa ndio wanastahili kushika simu ya mwenziwake. Lakini miongoni mwao hawakuwa tayari kusema kama wanaona uhalali wa kushika simu za wapenzi wao, na hawa walikuwa wasichana kwa wavulana ambao bado wako kwenye uchumba
Nilicho kibaini ambao ni utofauti wa makundi haya mawili nikwamba, Kundi la kwanza tayari limeshajiwekea malengo na uhakika wa mahusiano yao lakini kundi la Pili bado hawana msimamo na malengo kwenye mahusiaono yao ndio maana wakashindwa kutoa jibu la moja kwa moja, na swala la kushika simu za wapenzi wao au mpenzi kushika simu yake ilikuwa kasumba kubwa naamini bado hawajawa waaminifu na msimamo wa mahusiano yao
Kitu cha msingi ambacho kila mtu anatakiwa kujua anapokuwa katika mahusiano, nijukumu la kulinda penzi na kuwajibika kwa mwenza wake bila kujali wewe ni mume/mke au wewe ni mchumba tu, kwani hakuna anaye ingia katika maisha ya ndoa bila kuanzia katika uchumba.
Kwa mtu ambaye ni mwaminifu hakuna sababu ya wewe kuficha simu au kuzima simu hata kuweka password na vikwazo vingine ambavyo vinapelekea kuweka mipaka kati ya wapenzi wetu, kumbuka kwamba kuwa muwazi katika mambo yako hujenga mahusianao na kuleta uaminifu kati yenu.
kulingana na mada yetu hakuna asiye kuwa na uhalali wakushika simu ya mwenzi wake kama tayari umeamua kuwa huyu ni wangu wa maisha, hasa kwa wale walioko kwenye ndoa. si vyema kumkataza mwenza wako kushika simu yako na kama hili nitatizo ambalo unahisi linakukera sana pale mpenzi wako anaposhika simu yako au pale anapokukataza kushika simu yake. kila kitu kina sababu na maana yake ni bora kuzungumza ilikuweka mambo sawa
Kikubwa cha kufanya nikupunguza mabavu na maamuzi ambayo yanaegemea upande wako bila kujali mwenzako anajisikiaje au atanielewaje katika hili swala... kuwajibika katika kulinda mahusiano kwa kila namna ni jukumu la kila mmoja wenu. Tuwe watu wakuweka vitu wazi na kusisitiza uhaminifu miongoni mwenu