Majeshi
Maalum (Special
Forces)
ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yanayolinda amani Mashariki mwa
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa vikosi bora 35
vya majeshi ya nchi mbali duniani vinavyokubali kuwa na ufanisi wa
hali ya juu, uwezo mkubwa wa kupigana na vilivyofundishwa vizuri.
Kwa
mujibu wa Mtandao wa Imgur Via Distractify, Tanzania na jeshi lake
ni nchi pekee ya Afrika kuweza kuwa na majeshi yake miongoni mwa
majeshi bora duniani.
Chini
ya kichwa cha habari “35
Most Badass Elite Fighting Units from Around the World”
mwandishi, Micky Wren anaandika kuwa hayo ndiyo majeshi bora duniani,
yamefundishwa kwa kiwango cha juu kabisa, yana silaha za kisasa
kabisa, yameandaliwa vizuri kwa ajili ya operesheni ngumu za kijeshi
na yenye uwezo kukabiliana na adui katika mazingira yoyote kuanzia
kumaliza uhuni wa utekaji hadi kuwasambaratisha magaidi wenye uwezo
mkubwa.