Waziri
wa ujenzi nchini Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kipindi cha
mwezi mmoja kwa watumishi wa umma waliokopeshwa nyumba za serikali,
kulipa madeni yao vinginevyo watanyang'anywa nyumba hizo na kupewa
watumishi wengine.
Waziri
Magufuli ametoa agizo hilo leo muda mfupi baada ya kuzindua ujenzi wa
nyumba 851 zinazojengwa eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar
es Salaam, nyumba zitakazopokeshwa kwa watumishi wa umma.
Katika
maelezo yake, waziri Magufuli amesema takribani wafanyakazi 2500 bado
hawajalipa madeni wanayodaiwa, ambapo amemuomba makamu wa rais Dkt.
Mohammed Gharib Bilal kuunga mkono hatua hiyo ya kutoa mwezi mmoja au
kuwanyang'anya nyumba wadaiwa hao.
Wakati
huohuo, makamu wa rais Dkt Mohammed Gharib Bilal, amesema muungano wa
Tanganyika na Zanzibar utaendelea kudumu licha ya njama za watu
wachache wanaotaka muungano huo uvunjike.