Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Tolly Mbwete amesema shahada hiyo ya Obama imetokana na kutambua mchango wake katika fani ya maendeleo ya kiuchumi ya jamii ( Community Economic Development).
"Shahada hii sio ya kwanza kuitoa, na hii itakuwa ya 7 kutoa hapo hawali tuliwahi kupata msaada kutoka katika serikali yake ilikuweza kuanzisha shahada hii hapa nchini hivyo itakuwa vyema kama akifahamu maendeleo ya chuo hicho" Alisema
Akitaja waliowahi kupewa tuzo na Chuo hicho kuwa ni Rais mstaafu wa Afrika Kusini Bwana Nelson Mandela, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Benjamini Mkapa, Alli Hassan Mwinyi
Wengine ni Dr. Jane Goodall ambaye ni mtafiti wa mambo ya Sokwe mtu huko Afrika Mashariki na Profesa wa mawasiliano wa Uingereza Bwana David Mellor, chuo hicho kikiwa cha kwanza kufundisha masomo ya uzamili ya maendeleo ya kiuchumi ya jamii huku kikidahili wanafunzi wa shahada ya uzamili ya sayansi ya maendeleo ya kiuchumi ya jamii
Prof. Mbwete amesema kwa mwaka ujao wa masomo yaani 2013/2014 chuo hicho kitaanza kutoa Vyeti, Shahada ya kwanza na Stashahada ya uzamili ya maendeleo ya kiuchumi ya jamii kutokana na umaarufu wa mafunzo hayo. Alisema
"Kuanzisha shahada hii itawezesha wananchi kujua elimu ya kutafuta fursa za kiuchumi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja katika jamii yetu"Alisema Prof. Mbwete