KINANA, CCM WANAPANGA NJAMA ZA KUMVUA LISSU UBUNGE MAHAKAMANI



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani vikali njama za Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana kufufua kesi ya uchaguzi dhidi ya Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Mh. Tundu Lissu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbroad Slaa amedai kwamba CHADEMA imekamata nyaraka zinazoonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Kinana amewaelekeza waliowakuwa mawakili wa makada wa CCM waliomfungulia Mh. Lissu kesi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Singida Mashariki mwaka 2010 wafungue rufaa katika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ili kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma iliyotupilia mbali kesi ya makada hao wa CCM dhidi ya Lissu. Kesi ya Mahakama Kuu ilitupiliwa mbali tarehe 27 Aprili mwaka jana.

Dr. Slaa alisema kwamba lengo la njama za Kinana na CCM ni kuhakikisha kwamba Mh. Lissu anafutiwa Ubunge ili asiweze kushiriki katika mchakato wa Katiba Mpya kama mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba litakalojadili na kupitisha rasimu ya Katiba Mpya baadaye mwaka huu. Dr. Slaa alisema: “Kwa kipindi kifupi ambacho amekuwa Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge, Mheshimiwa Lissu amekuwa mwiba mkali kwa CCM na Serikali yake ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano.


BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI HABARI HII
KUELEKEA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WALIMU WAPAZA SAUTI, WALIA SERIKALI KUZIDI KUWAPUUZA

KUELEKEA BAJETI YA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI WALIMU WAPAZA SAUTI, WALIA SERIKALI KUZIDI KUWAPUUZA


Chama cha walimu Tanzania kimeitaka jamii kutambua kuwa mgogoro kati ya walimu na serikali bado upo palepale kutokana na serikali kutokubali kutekeleza madai ya walimu kwa kiwango wanachohitaji.

Akiongea leo jijini Dar es salaam, Rais wa chama cha walimu Tanzania Bw. Gratian Mukoba amesema wabunge watakapokuwa wakijadili bajeti ya wizara ya elimu wiki ijayo watambue kuwa mgoggoro huo bado upo.

Serikali itambue bado hatuja kubaliana juu ya madai yetu, hivyo mgogoro bado hupo pia wabunge watambue hilo ili serikali ijadiliane juu ya maslahi ya walimu” Alisema Mukoba

Aidha CWT iliamua kukubaliana na serikali kufanya majadiliano kwa faida ya walimu na ustawi wa elimu katika kikao cha baraza la majadiliano ambacho kilifanyika Mjini Morogoro tarehe 09 mpaka 10/12013 na tukakubaliana kufanya kikao kingine Februari 2013

Katika kikao hicho tulitaka ongezeko la mishahara,posho kuongezeka kwa asilimia 30 na asilimia 50 kwa walimu wa sanaa na walimu wa sayansi asilimia 50 tu, lakini serikli haikutimiza hayo” alisema

CWT ilipeleka mchanganuo unaopelekea uhalali wa madai yake, serikali ilitakiwa kushugulikia madai hayo haraka kabla ya kuitishwa kwa kikao kingine cha majadiliano na baadae CWT ilitimiza jukumu lake kwa kukubidhi serikali Justification yake tarehe 06/02/2013 lakini serikali ilikaa kimya. Alisema Mukoba

Tulikaa tena tarehe 21/03/2013 hukohuko Morogoro lakini serikali haikuja na yale tuliyo hitaji nabadala yake iliripoti kuwa mchakato wa ufuatiliaji offer bado unaendelea jambo ambalo halikuturidhisha” Alisema Mukoba
CWT waliomba fursa ya kumwona waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi kupitia, mwenyekiti, makamu mwenyekiti na katibu wa baraza ambapo tarehe 24 mpaka 25/05/2013 majadilihao hayo yalifanyika jijini Dar es salaam. Alisema Mukoba

katika kikao hicho, walihitaji Ongezeko mishahara kwa asilimi 100, posho ya kuundishia (Teachers allowance) 55% kwa walimu wa sayansi na 50% kwa walimu wa sanaa, posho ya 30% kwa walimu wanaofanyakazi katika mazingira magumu. Mambo ambayo walitaka wabunge watambue kuwa bado hayajatatuliwa

Hivyo CWT imeitaka serikali kuwa na nia njema na ikubali kurudisha mioyo ya walimu iliyokufa kwa kukata tamaa ilikufufua utendaji wao na kuboresha elimu ya Tanzania.

Bajeti ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2013/2014 kwa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi inatarajiwa kusomwa mapema wiki ijayo huko Bungeni Dodoma
MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, ASILIMIA 93 WAFAULU

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, ASILIMIA 93 WAFAULU



Baraza la mitihani Tanzania, leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwezi February mwaka huu, huku asilimia 93.9 ya watahiniwa wamefaulu mtihani huo

Akitangaza matokeo hayo katika ofisi za baraza hilo Mikocheni jijini DSM, Naibu katibu mtendaji wa baraza hilo Dr Charles Msonde amesema Jumla ya watahiniwa 40,242 kati ya watahiniwa 42,952 wa shule, sawa na asilimia 93.92 wamefaulu kwa daraja la I hadi la IV

Matokeo haya yanaonesha kuwa kwa mwaka huu ufaulu kwa watahiniwa wa shule umeongezeka kwa takribani asilimia 1.6. wakati kwa matokeo ya jumla matokeo yamepanda kwa takriban asilimia 0.2. hapo mwaka 2012 watahiniwa Elfu 40,775 sawa na asilimia 92.30 ya watahiniwa walifaulu mitihani hiyo.

Aidha Dr msonde ametaja shule 10 bora, zilizoongozwa na Marian Girls ya Pwani katika kundi la watahiniwa zaidi ya 30, ikifuatiwa na Mzumbe sekondary school iliyopo Morogoro. Shule zilizo fanya vibaya Pia ametaja watahiniwa waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali, 

Kwa upande wa Sayansi aliyeongoza ni Erasmi Inyanse aliyekuwa akisoma PCM kutoka shule ya Ilboru Arusha, kwa masomo ya biashara wa kwanza ni Erick Robert Mulogo kutoka Tusiime ya DSM kombi ya ECA, na kwa masomo ya lugha na sayansi ya Jamii kwa kwanza ni Asia Idd Mti kutoka Barbro-Johansson ya DSM alikuwa akisoma HGE

Aidha, Watahiniwa watano wa kiume bora kwa somo la Sayansi kuwa ni, Erasmi Inyanse kutoka Ilboru, Maige R Majuto kutoka shule ya Kisimiro, Gasper Singfrid mungongo wa Feza boys, wanafunzi wa kike walio fanya vizuri kwa somo la Sayansi ni Lucylight E Mallya wa Marian Girls, Edna Baraka Kibango wa Msalato na Sara Severin Kimario wa St. Marys mazinde juu.

Hatahiyo baraza la mitihani ilmezuia kutoa matokeo ya mitihani wa kidato cha sita kwa wanafunzi 89 kwa sababu za kutomaliza ada ya mitihani na matokeo yao yatatoka mpaka hapo watakapo lipia mitihani hiyo, 27 walipata matatizo ya kiafya hivyo watapewa fursa ya kurudia mitihani yao mwaka 2014


FUNGUA HAPA KUANGALIA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2013

ASILIMIA 43 WAFAULU, ZIRO ZAPUNGUA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE 2012

ASILIMIA 43 WAFAULU, ZIRO ZAPUNGUA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE 2012

Matokeo mapya yaliyo subiriwa kwa hamu sana hatimaye yametoka hii leo, huku kiwango cha waliofaulu kikiongezeka na kuwa asilimia 43 hivi sasa kutoka asilimia 9.55 kwa yale matokeo ya kwanza yaliyo tangazwa tarehe 18 februari mwaka huu.

Jumla ya watahiniwa Laki 397, 138 wamefaulu, wasichana wakiwa ni Elfu 60,751 na wavulana wakiwa ni Elfu 98,858 ikiwa ni jumla ya watahiniwa wa shule Laki 159,609.

Ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa, inaonyesha kuwa jumla ya watahiniwa Elfu 35,349 wamefaulu katika daraja I – III ambapo kati yao wasichana ni Elfu 10,924 na wavulana ni Elfu 24,425 ambao hawa ndio wataweza kujiunga na kidato cha sita mwaka huu kutoka idadi ya wanafunzi Elfu 35,349 ambao walifaulu hapo awali na kuacha idadi kubwa ya wanafunzi

Waliofaulu kwa daraja la IV ni wavulana ni Elfu 74,433, wasichana ni Elfu 49,827 ambao kwa ujumla wanafikia Laki 124,260 sawa na asilimia 33.54, Walipata sifuri kwa sasa ni Laki 210,846 sawa na asilimia 56.92. Matokeo ya wali jumla ya wanafunzi Laki 210, 846 walipata sifuri ambao ni sawa na silimia 56.92

Akitangaza matokeo hayo hii leo jijini Dar es salaam, Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Shukuru kawambwa amesema maandalizi ya matokeo yaliyo tangazwa sasa yamechakatwa kwa utaratibu wa Fixed Grade Ranges lakini yakafanyiwa standalization.

“Matokeo yaliyofutwa yalikuwa yamechakatwa kwa kutumia utaratibu wa fixed grade ranges utaratibu uliotumika kwa matokeo haya mapya lakini kwa hawamu hii tumefanya standalization ilikuweza kupata matokeo haya kama ambavyo tume maalum ilivyo pendekeza” alisema

Dr, Kawambwa alielezea Fixed Grade Ranges kuwa hutumia viwango vya aina moja kuchakata matokeo kwa masomo yote bila kujali kiwango cha kufaulu kwa somo husika, viwango hivyo hubadilika kila mwaka kulingana na ufaulu wa watahiniwa kwa kila somo husika

Aidha, katika mfumo wa Fixed Grade Ranges viwango vya aina moja hutumika kuchakata matokeo kwa masomo yote bila kujali kiwango cha ufaulu kwa somo husika. Viwango vya kuchakata matokeo hutumika hivyo hivyo kila mwaka bila mabadiliko . Alisema Dr. Kawambwa

kuanzia sasa na kuendelea baraza la mitihani litaandaa matokeo ya kidato cha nne na sita kwa kutumia mfumo wa fixed grade ranges na standardisation. Alisema waziri


KUANGALIA MATOKEO MAPYA KIDATO CHA NNE INGIA HAPA



WASANII WAKUTANA LEADERS CLUB KUJADILI MAZISHI YA MANGWAIR


Marehemu Ngwair akiwa na msanii M2 the P huko Afrika kusini kabla ya kufikwa na umauti

Baadhi ya wasanii wamekutana jioni hii ilikujadili jinsi ya kumpumzisha msanii mwenzao nguli Albert Mangwair, wasanii hao wako katika viwanja vya leaders club
Tayari kamati ya wakongwe wa muziki wamepanga kamati ya mazishi ambayo itaongozwa na Lady Jay Dee, Prof Jay, Mchizi mox, Nura, Pre Funk majani na
NURA AKANA MANGWAIR KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA
Msanii Nura alipohojiwa na kituo cha EATV kuusu arehemu kutumia madawa ya kulevya amekana kujua swala hilo na kuwa hajawahi kumshuhudia marehemu akitumia madawa hayo
“Sijawahi kumshuhudia ngwair akitumia madawa licha ya kusikia watu wakisema sana kuusu hilo, kama unavyo jua wabongo wanaongea sana hivyo kujua kitu cha ukweli au uongo nivigumu” Alisema Nura na kutoa masikitiko yake juu ya kifo hicho

HISTORIA YA MAREHEMU, MANGWAIR
Jina lake kamili ni Albert Keneth Mangwair, ni mzaliwa wa Ruvuma kwa kabila ni Mngoni wa kutoka Songea. Mangwair alizaliwa mkoani Mbeya mnamo tarehe 16 Novemba mwaka 1982 akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto 10, lakini katika uzao wa mama yake mzazi yeye ni motto wa 6.
Baada ya kufikisha miaka 5, Mangwair alihamia mkoani morogoro kwaajili ya kuanza shule ya msingi ya Bungo iliyopo hukohuko Morogoro, lakini baadae walihamia mkoani Dodoma ambako alimalizia masomo yake ya helium ya msingi.
Baadae alifanikiwa kujiunga na shule ya sekondari Mazengo kasha kuendelea na elimu ya chuo katika chuo cha ufundi Mazengo, Kwaufupi alianza kuimba tangu akiwa mdogo mpaka hapo nyota yake ilipo gara kwa watanzania.

MAZISHI KUFANYIKA MKOANI MOROGORO
Wapendwa wa karibu na mashabiki wote wakiwa wanasubiri kuwasili kwa mwili wa mpendwa wetu kutoka huko Afrika kusini aliko patwa na umauti
Kwa mujibu wa baba mdogo wa marehemu, mzee Mangwair ambaye yuko mbinga songea amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yani baba mkubwa wa Mangwair David Ngwair, kuwa watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam.
Mazishi yatafanyika mkoani Morogoro mahali alipozikwa baba mzazi wa msanii Mangwair.

MSANII ALIYEKUWA NAYE YUKO MAHUTUTI
Msanii aliyeongozana na mangwair ambaye anafahamika kwa jina la M to the P, Naye aliyake haiku zivuri na taarifa zinasema kuwa anapumulia mashine na manesi wanasema amelishwa kitu kinacho sadikiwa kuwa ni sumu nab ado anapat matibabu hukohuko Afrika ya kusini

MANGWAIR AFARIKI DUNIA AFRIKA KUSINI,



Msanii wa Bongo Fleva Albert Mangwair amefariki dunia akiwa Afrika kusini ambapo alikuwa akifanya shoo za muziki akiwa na msanii mwenzake Bushoke

Habari ambazo Blog hii imezipata, kutoka kwa kijana mmoja aliye jitambulisha kwa jina la Erick Mwakasila akiwa huko Afrika kusini ambaye ndiye ametoa taarifa za kifo hicho 

Erick amesema kuwa Ngwea alifanya shoo jana usiku huko Johenesbug, lakini tangu alipolala hakuamka mpaka saa 9 mchama walipoambiwa kuwa amefariki Dunia katika Hospitali ya St. Hellen huko Afrika Kusini

Blog hii inajaribu kutafuta ndugu wa karibu wa msanii huyo pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Afrika kusini ili kupata uhakika zaidi wa tukio hilo kwani chanzo cha kifo chake bado hakija julikana
SERIKALI YATAKIWA KUWAKUMBUKA WAFANYA KAZI WA MAJUMBANI

SERIKALI YATAKIWA KUWAKUMBUKA WAFANYA KAZI WA MAJUMBANI




Serikali imetakiwa kutekeleza mkataba wa kimataifa wa shirika la kazi Duniani ILO mbayo iliahidi huko Geneva mwaka 2011, ili kutekeleza maslahi ya wafanyakazi wa majumbani, ambapo Tanzania ni nchi ya Pili kwa kuwa na wafanyakazi wengi wa majumbani barani Afrika.

Mwaka 2011 tarehe 15 June huko Geneva, siku moja kabla ya kupitisha mkataba wa kimataifa wa shirika la kazi sheria no 189, Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DR. Jakaya Kikwete aliahidi kutekeleza mkataba huo na kuuridhia, hivyo serikali imeombwa kutekeleza ahadi hiyo.

Akiongea katika mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali kutoka barani Afrika na kufunguliwa na Waziri wa Kazi na ajira nchini Mhe. Gaudencia Kabaka , Mratibu wa mtandao wa wafanyakazi wa majumbani kanda ya Afika Bi. Vicky Kanyoka amesema wengi wa waafanyakazi wa majumbani wanakumbwa na changa moto nyingi hivyo kuitaka serikali kushugulikia changamoto hizo

“Serikali nyingi za Afrika zilipigia kura kutaka kuwepo kwa mkataba wa kimataifa ambao utatetea maslahi ya wafanyakazi wa majumbani, Tanzania ikiwepo lakini ni nchi chache sana zimeanza kutekeleza yale yaliyo takiwa kushugulikiwa” Alisema

Afrika inajumla ya vyama 19 vya kutetea maslahi ya wafanya kazi, lakini tuliafikiana kushugulikia haki ya kupewa ajira, muda wa kazi, mikataba, kima cha mishahara na jinsi ya kuwaendeleza kielemu wafanyakazi wa majumbani. Alisema Kanyoka

Naye Katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanya kazi Zanzibar bwana Khamis Mwinyi Mohamed, amesema kuwa wana jitahidi kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa majumbani na kutaja haki zinazotakiwa kufuatwa juu ya wafanyakazi hao.

“Tuli pendekeza mishahara ya wafanyakazi wa majumbani kiwe Elfu 60 kwa Zanzibar na Elfu 65 kwa Tanzania bara mpaka sasa hakuna anaye tekeleza haya, nasisi bado tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunatekeleza” Alisema Mohamed

Aidha Tanzania ina jumla ya wafanyakazi wa majumbani Zaidi ya milioni moja huku wengi wao wakiwa ni wanawake. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kazi Duniani Tanzania ni nchi ya Pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hao kwa asilimia 80.5, ikiongozwa na Mali yenye asilimia 86.8.

Nchi zilizo fanikiwa kufanikiwa katika kushugulikia tatizo hili kikamilifu ni nchi ya Afrika Kusini na Mouritius.

Mkutano huo wa siku tatu, ambao umeanza hii leo May 29 mpaka 30, unafanyika jijini Dar es salaam, umeshirikisha jumla ya wawakilishi 75 kutoka nchi za barabi Afrika, vyama mbalimbali vya kutetea maslahi ya wafanyakazi.
SERIKALI YA KIRI, UHABA WA VIFAA VYA MATIBABU NI TATIZO

SERIKALI YA KIRI, UHABA WA VIFAA VYA MATIBABU NI TATIZO

Serikali imekiri kuwa uhaba wa vifaa vya tiba ni tatizo hasa kwa hospitali kubwa hapa nchini, hali ambayo ilipelekea madaktari kufanya mgomo katika siku za nyuma

Akiongea leo Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu, Naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii Mhe. Seif Rashid amekiri kuwepo kwa tatizo hilo lipokuwa akijibu swali la Mhe. Magdalena Sakaya ambaye alitaka kujua nilini serikali itatatua tatizo la uhaba wa vifaa katika Hosptali za hapa nchini ili kukomesha mgomo wa madaktari usijirudie tena.

***********

Serikali imepiga marufuku biashara za vioski ambavyo viko kwenye makazi ya watu pamoja na vile ambavyo hufanya biashara hiyo maeneo ya shule kuacha mara moja kwani vioski vingi kufanya biashara bila ya kuzingatia sheria.

Hayo yamesemwa na waziri wa Tamisemi Mhe. Agrey Mwanry alipokuwa akijibu swali la Mhe Suzan Lymo ambaye alitaka ufafanuzi juu ya biashara zinazo endelea mashuleni.

BUNGE LA HAIRISHWA, WANAJESHI WA 5 NAO WAFARIKI DUNIA WAKIELEKEA MTWARA



Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania lime ahirishwa kutokana na vurugu zinazoendelea mkoani Twarahapo ambapo Serikali inatakiwa kuja kueleze juu ya kilicho tokea huko Mtwara hapo kesho

Hii le Bungeni Mjadala wa hotuba ya Wazari ya madini ili ikiendelea kujadiliwa, mpaka tena hapo kesho 

Habari zaidi zilizo ifikia Blog hii, Jumla ya wanajeshi Wa 5 wamekufa kwenye ajali wakielekea Mtwara wakitokea nachingwea.
MTWARA WAUKANA UZALENDO, MTU MMOJA AUWAWA, GARI YA JWTZ NAYO YAPATA AJALI

MTWARA WAUKANA UZALENDO, MTU MMOJA AUWAWA, GARI YA JWTZ NAYO YAPATA AJALI




Vurugu kati ya Jeshi la Polisi na baadhi ya wakazi wa Mtwara zinaendelea hivi sasa, ambapo Mahakama, Kituo cha Jeshi la Polisi na Taraja pamoja na nyumba ya Mbunge vimeharibiwa kutokana na maandamano vurugu hizo, maeneo yaliyo adhirika zaidi ni Mtwara mjini na Mkindani

Maandamano hayo yametokana na kupinga Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini ambayo imewasilishwa hii leo Bungeni

Habari zilizo ifikia Blog hii zinasema kuwa mpaka sasa, Maafa yanaendelea katika mkoa huo huku mabomu na risasi zikirindima kila kona watu wakikimbia hovyo huku polisi nao wakijitahidi kutuliza gasia hizo

Daraja la mkindani limevunjwa, mahakama ya mwanzo ya Mitenga imechomwa moto, kituo cha polisi, pamoja na maeneo ambapo kuna makapuni ya kuchimba gesi navyo vimechomwa moto.

Tayari mtu mmoja amekufa, huku wengine wakihofiwa kufa kutokana na ali hiyo. Nyumba ya Mbunge na ya mtangazaji wa TBC nayo imechomwa moto katika vurugu hizo

Habari zaidi zinasema kuwa Gari ya JWTZ nalo imepata ajali ikiwa njiani kuelekea Mwara ikitokea Nachingwea, na msaada wa kitabibu unahitajika kwa Askari hao

Hatahivyo, Waziri wa nishati namadini Mhe. Sospetre Muhongo amesema serikali imeendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Lindi na Mtwara kujua faida ya jinsi watakavyo faidika na Gesi hiyo pia ameeleza kuwa wakazi wa mtwara waachane na fujo na maandamano kwani sio njia sahihi ya kutatua mgogoro huo

Naye Waziri wa madini kivuli ambaye Mwakilishi wa kambi ya Upinzani Mhe. John Mnyika ameitaka serikali kuweka wazi mikataba yote ya madini ilikuondoa migogoro miongoni mwa wananchi 

WAZIRI WA HABARI AWAKANA WANAHABARI,WAPONDWA NA WABUNGE NA HOJA YA MAUAJI YA MWANGOSI YA ZIMWA

Waziri wa Habari Mhe. Fenera Mkandara


 Hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya habari, vijana tamaduni na michezo imeendelea kujadiliwa Bungenu huku Wabunge wengi wakiwaponda wana habari kwa kukiuka kanuni za taaluma huku wachache wakitetea wana taaluma hiyo kwa kuachwa bila kujadiliwa kwa matatizo yanayo wakabili






Wizara ya habari imeomba kiasi cha shilingi Billioni 20 na ushee ili kuweza kutimiza mambo mbalimbali katika wizara hiyo, ambayo iko chini ya Waziri Fenela Mkandara ambaye hii leo amesifiwa kwa staili ya ya nywele

Katika hotuba hiyo waziri hakuweza kuzungumzia hali ya usalama ya wana habari wana mateso na mauaji ambayo yamewakumba wanahabari kama kifo cha David Mwangozi, Absolom Kibanda na hata kufungiwa kwa gazeti la Mwanahalisi ambalo mpaka sasa aijulikani itafunguliwa lini

Hali hiyo ili mshangaza Mbunge wa viti maalum kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na maendeleo Bi. Rebeka Mgodo ambaye alishangazwa na hotuba ya Mhe. Fenera Mkandara kwa kuwasahau waandishi wa habari pamoja na matatizo yao ambayo yako wazi kwa jamii yote

“Nashangaa kutoona hata sehemu moja katika hii hotuba  ya waziri wa Habari juu ya mazingira magumu yanayo wakabili waandishi wa habari, wala mauaji ya David Mwangosi aliye uwawa na polisi huko Iringa”Alisema Rebeka Mgodo

Aidha, Bi Rebeka amewataka viongozi kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapofuata au kuitaji ufafanuzi wowote kutoka kwao ili kuweza kurahisisha ufanyaji kazi wa waandishi wa habari. Alisema Rebeka

Naye Mhe. John Mnyika pamoja na kupanga hoja yake kwa point nyingi wakati akiomba hoja yake kuungwa mkono na Bunge ili waweze kujadili swala la mauaji ya David Mwangosi 


Mnyika aliitaka Bunge kutengua kanuni ya 64 – 1c inayo zungumzia mbunge kuto zungumzia swala linalo subiri maamuzi ya chombo kungine hasa mahakamani, ambapo John Mnyika litaka wabunge wamuunge mkono ili waweze kuchangia na kutekeleza Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC iliyoongelea juu ya mauaji ya David Mwangosi ambaye aliuwawa na askari polisi September 2 mwaka jana huko mkoani Iringa

Kabla wabunge hawaja simama kuunga mkono hoja, Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda aliingilia na kupinga hoja hiyo ambayo ilizimwa zyyy kama Analogia ndani ya Bunge hilo

REJEA HAPO JANA

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda aliunga mkono hoja Mhe.Godfrey Zambi ambaye alitaka Spika kukataa kusomwa kwa hotuba ya kambi rasmi ya upinzani ambayo ili wasilishwa na Mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ambayo ni bajeti kivuli ya Wazara habari.

MADIMBWI YA VINYESI, ZAHANATI HII IFUNGWE AU MPAKA TUPATE MSAADA KUTOKA- WHO ?



Viongozi wetu wamekuwa na vipaumbele vyao kuliko maisha yetu, wakumwambia haonekani na anaye ambiwa hasikii kwani msaada kutoka World Health Organisation hawaja toa msaada au ushauri juu ya madimbwi ya vinyesi mpaka hali hii ishugulikiwe


Mbele ya Zahanati ya Mwenge kuna dimbwi la kinyesi linalo pelekea wagonjwa kutohudhuria hospitali hiyo kutokana na maji ya kinyesi yaliyotapakaa mbele ya Hospitali hiyo yakitokea kwenye Dimbwi linalo vuja masaa 24 katika eneo hilo


Kama ilivyo pichani hali hiyo imekuwa usumbufu kwa wagonjwa na wapita njia wa maeneo hayo huku pakitawaliwa na harufu mbaya, mamlaka husika azinambinu mpya kwani tatizo nila miaka sasa... pengine WHO watoe msaada juu ya Afya ya wkazi na wanao tumia maeneo hayo kila mara


Hakuna anaye jali kwani njia inayotumika mpaka sasa kuzuia hali hiyo ni matairi yaliyo pangwa na mawe  ,kama amna jinsi nibora Zahanati hii ya Mwenge ifungwe mpaka hapo njia itakapo patikana ya kudhibiti kinyesi kwa kuwa huu sio mradi wa Afya tena bali ni mradi wa Maradhi kwa watumiaji wanao pumua

***********************************************************************************

AFYA BORA KWA KILA MTANZANIA, WAFANYA BIASHARA WA MAJI SAFI NAO WAMETUTEGA NA MAJI YA KINYESI HAPA

Mbele ni magari ya maji safi rangi ya Blue katika eneo hilo lililotapakaa harufu ya kinyesi kama uonavyo pichani
Hili ni dimbwi lingine mbele kabisa ya hofisi za Tume ya Sayansi na Teknologia, nyuma kidogo ya kituo cha Sayansi kijitonyama ambapo Wauza maji hupaki magari yao.


Maji hayo ya Chooni yanaendelea kutiririka kwa wiki zisizo pungua sita, katika eneo hilo huwezi kukaa zaidi ya dakika 30 bila kusikia kizunguzungu, lakini wauza maji safi wao wanaendelea mbele na biashara yao ya kuuza maji huku akihofia afya zao


Kwa hali hii ambayo haiwatii mashaka viongozi husika kutokana na jitihada zao kuto onekana wakidhibiti hali hiyo, endapo magonjwa kama kipindupindu yatalipuka ni dhairi viongozi wataonyesha kujali hali hiyo

MASHINE ZA KUKATIA RISISTI ZITAKAZO TUMIWA NA WAFANYABIASHARA HIZI HAPA

Mashine za kukatia risiti zilizo zinduliwa na Mamlaka ya mapato Tanzania TRA wiki hii, ambazo zitatumiwa na wafanya biashara wenye kuingiza kipato cha Shilingi Billioni 14 kwa mwaka ikiwa na lengo la kuongeza kipato na kutunza kumbukumbu.

Kwenye uzinduzi huo TRA ilisisitiza sana juu ya wanunuaji kujenga tabia ya kudai risisti pindi wanapo nunua bidhaa yoyote ili kuweza kutimiza lengo la kukusanya kodi kisha kuweza kuboresha shuguli za kijamii

Mashine hizo zinapatikana kwa bei ya shilingi laki 8, natayari makampuni mbalimbali yapatayo 11 yamekuwa wakala wa TRA wa kusambaza mashine hizo kwa nchi nzima

Mashine hizo zinauwezo wa kutumia lugha ya kiingereza na kiswahili kulingana na uhitaji wa mfanya biashara au mteja, Pia itawasaidia wafanya biashara kuwa na rekodi ya mauzo ya bidhaa zake hivyo kuepuka hasara.


Adha TRA itaweza kutuma ujumbe wa maneno kupitia risisti zitakazo katwa kwenda kwa mtumiaji au kutuma taarifa ya maelezo yoyote kwa mfanya biashara, ambapo hali hiyo itarahisisha mawasiliano kati ya TRA mnunuzi na mfanya biashara

SHULE ZA MANISPAA YA ILALA ZINA UPUNGUFU WA MADAWATI ELFU 88,

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg6zHitwBvRvqBU3G07NZKJjlKwOdotV0nso8y5I_BKcC2T_U-LN0Zb5Cu9Pgq4tf5KT3EyTHkUTs-sFayJPhOcjAhPDEL_6qr1ugFdAGDdEjXu9C7uZ5G29iPLaSwIrrEz0tCN0FNvTmmu/s1600/UHABA+WA+MADAWATI+SHULE+YA+MSINGI+MWERE+B+PIX+NO+0000000000000.jpg

Kutokana na tatizo la upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari katika manispaa ya Ilala, imemlazimu meya wa manispaa hiyo bwana Jerry Slaa kuanzisha kampeni ya kuchangia madawati ili kuondokana na tatizo hilo



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg32kYHgZ-qCRKHGe-EKbaMfsmy_MiCWvkvCK4wN0Emd6V1POZ2IzWollpmxS1H5qnKcZ7mDukOmVNc6LcT4w1V02PCaINYa3RPfM3jr8j6rYrCOzbZUtTSNpd-63A3QrQ62zGBKh_0fIQ/s1600/1Wanafunzi+wa+shule+ya+Msingi+Mvumi++%25288%2529.JPG


Manispaa hiyo inaupungufu wa madawati Elfu 44,151 kwa shule za msingi zipatazo 105, huku shule za sekondary 49 zikiwa na upungufu wa madawati Elfu 14,354 jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu katila manispaa hiyo



http://farm9.staticflickr.com/8142/7412822258_64cdf5a4b5_z.jpg


Aidha wingi wa wanafunzi umeelezwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazo hatarisha maendeleo ya elimu kwani wanafunzi wengi katika manispaa hiyo hukaa chini wakati wakiwa darasani. 



JUKWAA LA KATIBA LASUBIRI HAKI MAHAKAMANI, WATAKA MCHAKATO WA KATIBA USIMAMISHWE. NCHIMBI NAYE APEWA KIBARUA KIZITO

JUKWAA LA KATIBA LASUBIRI HAKI MAHAKAMANI, WATAKA MCHAKATO WA KATIBA USIMAMISHWE. NCHIMBI NAYE APEWA KIBARUA KIZITO


Jukwaa la Katiba Tanzania limeamua kwenda mahakamani kupinga mwenendo wa uundwaji wa katiba mpya kwa madai kuwa mchakato unaotumika siyo wa kidemokrasia.

Akiongea na Wana habari leo Jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Bw. Deus Kibamba amesema kuwa, Tume ya katiba inapeleka mchakato kwa haraka hivyo kuwanyima fursa wananchi kutoa maoni yao na kwamba wanaiomba mahakama  kusitisha zoezi la kukusanya maoni.

 “Tumeamua kwenda mahakamani kutafuta haki ya watanzania, kwani tumejaribu kufanya kila jitihada na kutoa matamko lakini hayakuzaa matunda hivyo Mahakama itatusaidia kuleta haki” Amesema Kibamba

Kibamba amesema, Tumejaribu kutoa tarifa kwa ngazi za Kibunge kwa kuonana na spika, kuonana na waziri wa sheria na katiba pamoja na kujaribu kwa ngazi za juu kwa kuomba kukutana na rais lakini haya yote hayaja zaa matunda hivyo tunaenda mahakani ambako haki ya watanzania inapatikana huko.

Bwana Kibamba aliendelea kusema, Tume ya katiba imeshindwa kutekeleza misingi 5 ya uundwaji wa katiba hivyo kuwanyima wananchi fursa ya kuleta mabadiliko kikatiba.

“Mwenendo wa mchakato wa katiba mpya hauto zaa katiba mpya Tanzania, nasema hivi kwakuwa wananchi hawajui kitu kabisa mchakato unaharakishwa bila hamasa yoyote hii haraka niyanini.” Alisema

Alitaja misingi hiyo 5 kuwa ni, Ushirikishwaji wawana siasa, kutokuwepo kwa mahakama ya kikatiba nchini kiasi kwamba wanalazimika kwenda mahaka zilizopo kufikisha madai yao. Tayari jukwaa hilo limeandaa mawakili 10 kusimamia kesi hiyo wakiongozwa na Rugemeleza Nshulla.

Aidha Bwana Kibamba ameongeza kuwa, Mchakato wa katiba mpya si vyema kuendeshwa kisiasa hivyo Wabunge wasihusishwe katika mchakato huo na kuwa wananchi wapewe nafasi kubwa ya kutoa maoni yao ili kuepusha msukumo wa chama kimoja.

Katika hatua nyingine Jukwaa la katiba limeitaka Tume ya katiba kueleza wananchi ni lini watatoa rasimu ya katiba kwani muda waliotoa tayari umepita na kwamba Mabilioni wanayotengewa na serikali yanaenda wapi.

Wakati huohuo, Jukwaa la katiba limemtakaWaziri wa Mambo ya ndani Dr. Emanuel Nchimbi asikiuke katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ibara ya 19, kwani wizara yake imepanga kukiuka ibara hiyo,

Dr. Nchimbi akisoma bajeti ya wizara yake mapema Bungeni amesema serikali inapanga kupeleka muswada Bungeni wakuzuia mihadhara na maandamano yote nchini kwani wanaofanya hivyo wanasababisha uvunjifu wa amani

“Kuzuia mihadhara ndio itakuwa kama kuchohea kwani kila mtu anahaki ya kusema na kutoa maoni yake” alisema Kibamba.
VIJANA LAKI 7 NA 60 ELFU HAWANA AJIRA, NEEC WAJIKITA KUTAFUTA MBINU MPYA

VIJANA LAKI 7 NA 60 ELFU HAWANA AJIRA, NEEC WAJIKITA KUTAFUTA MBINU MPYA

Kutokana na swala la ukosefu wa Ajira nchini, Baraza la uwezeshaji wananchi kiuchumi NEEC limeamua kuwapa elimu ya kujiajiri vijana 40 ambao ni wahitimu wa vyuo vikuu ili kuendeleza biashara zao na kuajiri wengine.

Akiongea hii leo katika kituo cha Ujasiriamali cha chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Katibu mtendaji wa Baraza hilo bwana Anecleti Kashuliza amesema wameamua kutoa elimu hiyo ili kuweza kutoa ajira kwa kundi kubwa la vijana kwa lengo la kupata ajira na kisha kuajiri wengine

Njia ya kukabiliana na tatizo la ajira nikuwapa elimu ya mitaji pamoja na kuenedeleza biashara zao, ambapo vijana 40 tuliowapata baada ya mchujo watasaidiwa kukuza biashara zao” Alisema


Vijana wengi wa kitanzania hawana ujuzi wa biashara wa vitendo, kwani wamezoeya njia ya nadharia zaidi kuliko vitendo hivyo kushindwa kujiajiri hata pindi wanapo hitimu masomo yao. Alisema Bwana Kashuliza


Hatapindi vijana wanapo jaribu kujiajiri, ukosefu wa kuendeleza mitaji huwaangusha, pia ujuzi wa kinachohitajika sokoni pia nimdogo


Uwezo wa biashara ya kushirikiana (Net-Working) inawashinda vijana waliohitimu vyuoni kuweza kufanikisha kujiajiri wenyewe, hivyo tutawawezesha vijana hawa kujiajiri ikiwa pamoja na kukuza mitaji yao iliwaweze kuajiri na wengine” Alisema


zaidi ya vijana Laki 8 ambao huingia katika soko la ajira kila mwaka nchini, laki wakiwa ni wahitimu wa vyuo vikuu, vijana Elfu 4 tu kati yao ndio huajiriwa kila mwaka hapa nchini, hii umaanisha kwamba idadi ya vijana Laki 7 na 60 Elfu hujikuta bila ajira.

MALENGO YA MILENIA 2015 KUTOTIMIA BILA MAJI KUWAFIKIA WANANCHI KWA MASAA 24 NCHINI

Swala la uharibifu wa mazingira umetajwa kuwa chanzo cha kukauka kwa vyanzo vya maji nchini, na kuchangia kwa tatizo la uhaba wa maji



Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Waziri wa maji na Umwagiliaji Prof. Jumanne Maghembe alipokuwa akifungua mkutano wa wiki moja wa kujadili tatizo la maji kwa nchi za Afrika ambapo amewataka watanzania kutunza vyanzo vya maji




“Watu wengi huaribu vyanzo vya maji katika maeneo yanayo wavunguka hii pia ni changamoto kwetu, matumizi ya mkaa na kuni ndio huchangia”

Prof. Jumanne alisema kuwa hivi sasa mchakato wa kufikisha maji kwa vijiji 682 nchi nzima umeanza, hivyo kufikia mwaka 2015 mradi huo wakufikisha maji utakamilika.




Mkutano huo unalenga kuahinisha njia za kupunguza upotevu wa maji kabla ya kumfikia mteja ili kufanikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa ukanda wa Afrika ifikapo mwaka 2015

“Watu Millioni 65 barani Afrika wana uhitaji mkubwa wa maji, huku nchini Tanzania ni Asilimia 63 ya watu wanahitaji maji. Hivyo wadau wa maji wanaangalia ni njia gani za kuwafikia watu hawa “Alisema Prof. Jumanne Magembe



Hatahivyo, Dawasa kupitia mpango wake maalum wa kuboresha maji katika jiji la Dar es salaam imepanga kuongeza uzalishaji wa maji kutoka lita Millioni 300 hadi Lita Millioni 756 kwa siku



Dawasa pia imedhamiria kuongeza idadi ya waliounganishiwa maji kutoka kaya 110,000 kwa sasa mpaka 590,000, ambapo huduma ya maji itakuwa kwa masaa 24 tofauti na hivi sasa maji hupatikana kwa masaa 8 tu.

Katika hatua mbalimbali za kuwafikishia wananchi maji kwa asilimia kubwa nimoja ya malengo ya millenia kwa mwaka 2015, ambapo mapato ya Dawasa yatafikia Shilingi Bilioni 9 kwa mwezi tofauti na ilivyo sasa, wana kusanya shilingi bilioni 3 tu kwa mwezi

TO ALL MOTHERS



Nawatakia kila heri na furaha kina mama wote wa Tanzania katika siku ya maadhimisho ya wanawake Duniani, ambayo hufanyika mara moja kil mwaka.

Wanawake wa Tanzania tuna changamoto nyingi sana ila MUNGU atulinde atupe moyo wa kusonga mbele.


Kwaniaba ya Bunju Ladies Group Nawatakia kila lakheri Wanawake wote Tanzania........

Pole ziende kwa mama yangu mpenzi Bi. Josephine Ogalo ambaye yuko msibani Musoma lakini na mpenda sana 

                         HAPPY MOTHERS DAY
WAUGUZI - TUTAWEKA MWANASHERIA WETU, UKOSEFU WA VITENDEA KAZI NA WAGONJWA WENGI HUSABABISHA TUONEKANE HATUFAI

WAUGUZI - TUTAWEKA MWANASHERIA WETU, UKOSEFU WA VITENDEA KAZI NA WAGONJWA WENGI HUSABABISHA TUONEKANE HATUFAI

CHAMA cha wauguzi nchini kitaweka wanasheria wao ilikuweza kuwatetea pindi wanapopatwa na matatizo katika kazi yao

Akiongea na waandishi wa habari jijini Da es salaam, Mweyekiti wa chama cha Wauguzi mkoani Da es salaam, Bi Joan Bigirwa amesema chama hicho kinahitaji mwanasheria ilikubaini kosa likowapi pindi muuguzi anapoangukia mikononi mwa sheria

Wauguzi wengi wana huhukumiwa na kila mtu pale kosa linapotokea kama kufariki mgonjwa akiwa hospitali na kulaumiwa kuwa ni uzembe wao bila kuangalika kama hakukuwa na vitenda kazi au ni kosa la Daktari, lakini jamii yote ulaumu Wauguzi” Alisema

Hali hiyo imepelekea dhamira ya kuweka wanasheria ilikusaidia wauguzi pindi kunapotokea makosa kwani tupo kwaajili ya kutetea wauguzi pamoja na haki ya wagonjwa ya kupata huduma. Alisema Bi. Joan

Hatua hiyo imetangazwa ikiwa ni siku chache kuelekea siku ya wauguzi Duniani ambapo kitaifa siku hiyo itahadhimishwa mkoani Lindi

Naye, Bi. Wilielmina Niwabigira ambaye ni Afisa Muuguzi (DUCE) na mwenyekiti wa Tanzania Nursers Association (TANNA) amesema kuwa mishahara midogo, wagonjwa wengi kuliko idadi ya wauguzi, mazingira yakazi yasiyo rafiki ya kazi husababisha wauguzi wengi kuonekana hawafanyi kazi ipasavyo na kutojali wagonjwa

Hakuna vitendea kazi, wagonjwa ni wengi kuliko idadi ya wagonjwa pamoja na mishahara kidogo husababisha wauguzi tuonekane kama hatujali wagonjwa kitu ambacho sio kweli” alisema Bi. Niwabigira

Kama huduma zikiboreshwa na kuwepo kwa vitendea kazi vya kutosha kulingana na idadi ya wagonjwa tunao wahudumia, whakutakuwa na malalamiko kwa wateja juu ya huduma zetu lakini kuna muda tunashindwa kulingana na mazingira yasiyo rafiki kwetu tuwapo kazini

Mgonjwa anaweza kuja hospitali dakika za mwisho lakini akifariki hulaumu wauguzi, kumbe angewahi hayoyote yasinge tokea. Kuna muda wagonjwa nao waelewe hilo”Alisema

Hatahivyo chama hicho kimeeleza kuwa hakuna Hospitali hata moja nchini ilikidhi vigezo vya kuweka wauguzi wa kutosha kama ambavyo sheria ua Huduma za Afya inasema, kwani mpaka sasa idadi ya wagonjwa ni huwa kubwa kuliko ya wauguzi na madaktari

Kaulimbiu ya maadhimisho ya wauguzi kitaifa kwa mwaka 2013 inasema kutekeleza mpango wa millenium ifikapo 2015. ambapo wanalenga kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, kuboresha afya ya mama, kudhibiti maambukizi ya virusi vya ukimwi, malaria na magonjwa mengine ya kuambukiza kam kifua kikuu

TBS YAJA NA VIWANGO VIPYA KUDHIBITI VIWANDA, MAKAMPUNI KUTUNZA MAZINGIRA



Tanzania imeanza kutekeleza kiwango cha kimataifa cha uzalishaji kitakacho tekelezwa na viwanda pamoja na makampuni mbalimbali nchini kwa lengo la kunufaisha jamii

Kiwango hicho kilicho tolewa na shirika la viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Shirika la viwango la kimataifa (ISO) linalenga makampuni kuzalisha bidhaa kulingana na kiwango cha jamii inayo izunguka na bila kuadhiri mazigira

Akiongea na Waaandishi wa Habari hii leo katika uzindushi wa kiwango hicho mapema leo jijini Dar es salaa, Mkurugenzi wa TBS bwana Leandri S. Kinabo amesema kiwango hicho kitatumika na nchi zote za ukanda wa Afrika mashariki na Tanzania ndio walipewa nafasi ya kuandaa kiwango hicho

“Kiwango kimezinduliwa Tanzania lakini kitatumika na nchi zote za Ukanda wa Afrika mashariki kwa maana Kenya, Uganda watatumia kiwango hichi” Alisema Bwana Kinabo

Kinabo aliongeza kuwa, Lengo la kiwango hicho nikuzitaka kampuni na viwanda vinavyo zalisha bidhaa katika ukanda huu kuzalisha bidhaa zao huku zilikila mazingira na rasilimali watu katika maeneo yanayo wazunguka hatimaye kunufaisha jamii hiyo

“Makampuni yatatakiwa kutosababisha maafa, kulinda mazingira, rasilimali watu pamoja na njia ambazo zitaleta maendeleo katika eneo husika kama barabar”alisema

Naye mwakilishi wa Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ambaye ni bwana Odilo Majengo amesema kuwa kiwango hicho kinajulikana kama TZS 1323 ndicho kitatumika kwa makampuni yote ukanda wa Afrika Mahsriki kwa ajili ya viwanda na makampuni.
ASIYE TOA RISITI KUTOZWA MILLIONI 3

ASIYE TOA RISITI KUTOZWA MILLIONI 3




Wafanyabiashara ambao hawatatoa risiti pindi wauzapo bidhaa zao watatozwa faini ya shilingi Millioni 3, ikiwa pamoja na wale watakao nunua bidhaa bila kudai risiti kutozwa Milioni 1 kwa kosa hilo





Hayo yamesemwa na Bi. Alvera K. Ndabagaye ambaye ni Afisa Elimu mwandamizi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) alipokuwa akitoa mafunzo kwa wafanya biashara wa vifaa vya ujenzi na vipuri vya magari katika manispaa ya Kinondoni ya jinsi ya kutumia kifaa kipya cha kielctronic kwaajili ya kukatia risiti

“ Nihaki ya kisheria kudai risiti, pia nikosa kisheria kutotoa risiti baada ya kuuza bidhaa, faini kwa asiye toa ni Millioni 3 na kwa yule asiye dai ni Millioni 1” alisema Bi. Alvera

Aidha Bi. Alivera amewataka Watanzania kutambua kwamba utozwaji wa kodi ndio pato la taifa hivyo kuwa mstari wa mbele kudhibiti upotevu wa kodi, nakuacha kulalamika pale ambapo wanakosa huduma za jamii kwani kodi ndio hukamilisha hayo yote

“Tunalalamika serikali isipo kamilisha huduma za kijamii lakini hatujui kuwa kodi zetu ndio hufanya haya yote.. tuwe wazalendo tuzuie mianya ya kupotea kwa kodi ilikuleta maendeleo”

Kwamuda sasa TRA ikokwenye zoezi la kutoa Elimu kwa wafanyabiashara wa ngazi mbalimbali nchini ya jinsi ya kutumia mashine ya kielectroniki kwaajili ya kutolea risiti wakati wa mauzo ya bidhaa zao

Hatahivyo kifaa hicho hakitakuwa na ongezeko la kodi iliyopo sasa bali itashugulikia utoaji wa risiti tu. 

Kategori

Kategori