Ngoma ya Feza Kessy ambaye ni mwakilishi wa Tanzania ndani ya Big Brother Africa. Fezza ameendelea kufanya vizuri katika jumba hilo na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri
Msanii aliyejulikana kama KASHI kwajina kamili ni Jaji Hamisi ambaye amefariki jana baada ya kuugua kwa siku tatu, amezikwa katika makaburi ya Anansif Kinondoni hii leo maajira ya alasiri
Kashi ameacha watoto wawili pamoja mume, kwamujibu wa mama mzazi wa marehemu arehemu alizaliwa mwaka 1976 huko mkoani Lindi
Pichani ni Mama wa marehemu Kanumba, mama yake Lulu akiteta jambo na mama yake Monalisa |
***************************************************
CD ZISIZO NA CHATA YA TRA KUPIGWA STOP JULY MOSI
Baraza la sanaa
Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la hatimiliki nchini zimejipanga
kuzuia mauzo ya CD za wasanii wa bongo ambazo hazina chata ya Mamlaka
ya mapato Tanzania (TRA), ili kuongeza kipato cha wasanii na Taifa
kwa ujumla.
Wakiongea na Blog
hii leo Dar es salaam, Kaimu katibu mtendaji wa BASATA bwana Godfrey
Lebejo na Mtaalamu wa Tehama kutoka COSOTA wamesema zoezi hilo
litaanza rasmi July 1 mwaka huu.
Kwa muda sasa
wasanii wa bongo wamekuwa wakilalamika kuibiwa kazi zao, hivyo
mamlaka hizi zimeamua kutumia mbinu mpya ya kudhibiti kazi hizo kwa
lengo la kuinua maslahi ya wasanii.
*******************************************************************
BAHATI BUKUKU AHAMIA KENYA, NA NGOMA YAKE MPYA - NAKUTEGEMEA
Katika hali ya kushangaza msanii nguli wa nyimbo za injili nchini Bahati Bukuku ameandika katika mtandao wa ou tube wimbo wake mpya kuwa ni muimbaji wa Kenya
Ngoma hiyo mpya ambayo imesambazwa kwenye mtandao wa You Tube inamtambulisha kama mkenya
****************************************************************************
NGOMA KALI KUTOKA KWA DESIRE LUZINDA, UNAITWA NSUBIZA
MSANII WA UGANGA
*************************************************************************
SIKILIZA HAPA***HAKI YETU- NGOMA MPYA YA KIDUMU
Mwanamuziki
Jean Pierre Nimbona Alias a.k.a KIDUMU ametoa wimbo mpya unao kwenda
kwajina la HAKI YETU, ambao unaongelea zaidi maswala ya haki na
usalama ujumbe kwa jamii yote kujali HAKI.
Kidumu
ni raia wa Burundi ambaye aliamia nchini Kenya wakati wa vita ya
wenyewe kwa wenyewe mwaka 1994, lakini yeye aliingia nchini Kenya
1995. mwaka 2001 alitoa Album yake ya kwanza inayoitwa Yaramenje,
amekuwa akiimba kwa lunga yakirundi Kiswahili na Kingereza kidogo
Kidumu
ameimba nyimbo 18 zikiwemo alizo imba mwenyewe na za kushirikishwa. Wimbo huu mpya Kidum amemshirikisha Nemless
Haki yetu umeandikwa na Kelvin Swamwel, Thiorry de Oliviera na Nimbona Jean Piere aka Kidum, Ngoma imetengenezwa na Robert "rkay" Kamanzi na Steven Waweru na Producer wake ni Robert"rkay" studio ya MingiLove Studios.
Posted: April 05.2013
*********************************************************************************
MERCY JOHNSON AMUANIKA MTOTO WAKE
Msanii maarufu wa maigizo barani Afrika ambayea anatokea
pande za Nigeria, bibie Mercy Johnson amemuanika mtoto wake, Mtoto huyo anaitwa
Baby Purity Ozioma Okojie’s anatarajiwa kufanyiwa sherehe wiki ya kwanza ya
mwezi wa tatu huko Lagos Nigeria
WIZ KHALIFA NA AMBER ROSE WAPATA MTOTO WA KIUME.
Rapper Wiz Khalifa na Mchumba wake Amber Rose wamemkaribisha duniani mtoto wao wa kwanza leo asubuhi. Mtoto Huyo wa Kiume amepewa Jina la Sebastian Taylor Thomaz Aka "The Bash." Baada Ya Mtoto Kuzaliwa Wiz Khalifa Ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter "Daddy time," "Happy Birthday Sebastian "The Bash" Taylor Thomaz!!! ` Everyone welcome this perfect young man into the world.
**************************************************
LINEX KUMUANIKA MCHUMBAWAKE, SIKUYAKE YAKUZALIWA HUKO ARUSHA
Msani Linex leo anatarajia kumuanika
mpenzi wake kwenye siku yke yakuzaliwa ambayo itafanyika huko mkoani
harusha, Leo katika sherehe aliyo andaa nimoja yakitu ambaho
kinasubiriwa na wengi ilikumjua mridhi wa mama halima
Hatahivyo kunatetesi kuwa mrembo atakaye wekwa wazi ni mchumba wake wa kizungu ambaye amekuwa akionekana naye kwa karibu sana na ambaye amewahikukiri kutoka naye
Linex anasherekea siku yake ya kuzaliwa
hii leo ikiwa alizaliwa tarehe 15. 2 lakinimiaka yake ameweka kapuni,
na itafanyika huko Arachuga
Linex ambaye anafanya vizuri sana ndani
ya game ya bongo fleva huku akiwa na style yake ya kuweka manjonjo ya
kiluga chake kwenye nyimbo. Pia Linex Yumo ndani ya kundi la
Lekalutigite ambao ni muunganikano wawasanii kutoka Kigoma
Posted on. 15.02.2013
***********************************************
MABAYA KUMKUTA DIAMOND,MGANGA WAKE AFUNGUKA
Msanii maarufu nchini Diamond Plantnum ameingia katika
kashfa nyingine baada ya mtu anaye dai kuwa ni mganga wake kujitokeza na kumpa
makavu kwenye vyombo vya habari
Akiongea Katika kipindi kilichorushwa na kituocha TV cha EATV kipindi
cha Hotmix, mganga huyo aliye julikana kwajina la Ustadhi Yahaya wa Kigogo jijini
Dar es salaam, amesema jinsi anavyosikitishwa na msanii huyo kusema kuwa
hajawai kwenda kwa mganga wala kufanya ushirikina waaina yoyote ilikujiinua
kisanii
Mganga huyo amesema, anashangazwa na kitendo cha Diamond
kusemekana kuwa ni freemason wakati yeye ndiye
aliyemuinua kisanii pka akufikia hapo
Aidha mganga huyo alipoulizwa niya yakufanya kama
anamchafulia msanii huyo, alidai kuwa yeye hana nia hiyo ila kitendo cha
Diamond kujidai anampotezea na kutopokea simu yake kwa muda mrefu sasa baada ya
kupata umaarufu nakung’ara kimuziki
Mganga huyo aliweza kusoma SMS ambayo alimtumia mwaka jana
msanii huyo kumweleza kuwa anacho kifanya sio poa kwani yeye ndiye aliyemtoa
kisanii na kuzidi kulalamika kuwa hata simu zake hapokei
Mganga huyo kudhibitisha kuwa anamfahamu zaidi Diamond
alisema kuwa miaka ya nyuma kidogo aliwahi kukutana hata na mama wa msanii huyo
kwani familiya zao zinafahamiana
Hatahivyo Mganga huyo akueleza wazi kama kweli anamdai
Diamond pesa yoyote ambayo anahitaji kupewa na msanii huyo, na kueleza kuwa
maagano aliyoweka naye ndiyo chanzo cha kila kitu mpaka yeye kufikia hatua ya
kusema habari hizo
Mganga huyo alitoa maneno ya kumlaani Msanii msanii huyo,
kwakusisitiza kuwa kitakacho mtokea msanii huyo kitaonekana
Kwamuda wa mwaka hivi kumekuwa na lawama akitupiwa msanii
Diamond kuwa anamtesa na kumroga msanii mwenzake ambaye alikuja kwa swaga kama
zake msanii Tanzanite ambaye naye Alisha muomba msamaa msanii huyo iliasimroge
na Diamond kukana matukio hayo nakusema kuwa amemsamee msanii huyo
Kama haitoshi kumekuwa na kashfa ya yakumwambia msanii huyo
ni Mshiriki wa Dini ya kimashetani ya Freemason, tuhuma ambazo Diamond
amezikana kuwa sio za kweli nahata Blog hii iliwahi kuandiika habari isemayo
DIAMOND AUKANA U FREEMASON
Diamond mwenyewe kupitia vyombo mbalimbali vya habari
amekuwa akikana kumjua mtuhuyu ambaye anadai kuwa alikuwa ni mganga wake
*********************************************************
SERIKALI YASIKIA KILIO CHA WASANII WA MAIGIZO
Serikali imekubali kukaa na Wasanii wa
Filamu ilikusikiliza madai yao juu ya maswala ya kanuni za Tozo
zilizopendekezwa wakati wa kupitia kazi za wasanii (Filamu) kabla ya
kufika Sokoni
Mike Sangu, Mwenyekiti wa Chama cha
Wasanii maigizo nchini, amesema kuwa Tayari wameanza mazungumzo na
Serikali juu ya kanuni hizo, iliwaweze kuangalia njia mbada ya
kufanya juu ya Kanuni hizo ambazo zilikuwa zinawakandamiza sana
upande wa mapato
Mike Sangu- M/Kiti wa chama cha w |
“ Tayari tumeanza mazungumzo na
Serikali juu ya Kanuni hizi mpya na tunaamini kuwa mambo yataenda
sawa kama tunavyo tarajia, Alisema Mike
Aidha kulikuwa na mgogoro juu ya kanuni
mpya katiya TAFF, COSOTA na Chama cha Waigizaji nchini, ambapo
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Tamaduni na Michezo.
Hatahivyo, Mike Sangu ameongelea hali
ya Msanii mwenzao Matumaini ambaye anahali mbaya huko nchini Msumbiji
alikoenda kwa shuguli za kikazi, nakuongeza kuwa Wanaomba watu wenye
nianjema watoa mchango wa hali na mali ilikuweza kumasafurisha kuja
Nchini kwa matibabu zaidi. Alisema Mike
Msanii wa maigizo Matumaini anaye umwa hivi sasa |
Mike Saangu, ametoa nomba yake ya Simu
kwaajili ya watu wanaoitaji kutoa mchango wao na kiasi kinacho
hitajika ni Shilingi Milioni Moja. 1,000,000 kama nauli ya
kumsafirisha msanii huyo
“ Matumaini kazimba sana miguu na
hali yake nimbaya, msamaria yeyote anaweza kumchangia ni 0718951355
kwaajili ya kukata tiketi ya kumsafirisha arudi nchini” Alisema
Mike
******************************************
HUYU HAPA MTOTO WA BOB JUNIOR
******************************************
MSANII WA BONGO FLEVA ASHANGAZA MSIBANI KWA SAJUKI
Msanii mkongwe na maarufu wa Bongo Fleva leo katika msiba wa Sajuki amekataa kuhojiwa na waandishi wa habari kwa madai ya kutotaka kuonekana kiherehere anapohuzuria misiba.
Msanii huyo ambaye jina lake nalihifadhi, alisema "Sipendi kuonekana kiherehere kwa sananii wenzangu kwani mimi naonekana sana kwenye kila msiba wa wasanii wengine"
Kituambacho nimekiona mimi nikuwa wasanii wa Bongo Fleva wanabagua wasanii wengine hasa kutokana na kitendo cha msanii nguli na mkubwa kukataa kuhojiwa juu ya msiba kwa kuhofia kuona anaki herehere miongoni mwa wasanii wengine.
Msanii huyu wa Bongo Fleva alijitokeza sana katika mazishi na msiba wa sharomilionealakini katika mazishi ya sajuki alijificha na kukataa kuhojiwa iliasijulikane kama alihudhuria mazishi ya sharo Milionea
**********************************************
AKILI THE BRAIN ARUDI TENA NA NGOMA MPYA YA MY DEAR
Msanii wa bongo fleva na muandaaji wa Muziki nchini ambaye alitamba na kibao cha Regina, arudi tena
Akili the brain, ambaye kwa muda kidogo alikuwa kimya sana baada ya kutoa ngoma ya Regina,
hivi sasa anakujia na wimbo wa My Dear
Katika wimbo huo wenye miondoko kama ya kiindi amem..
hirikisha msanii sa-raha
Akili, amejikita zaidi kwenye uproducer licha ya kuwa na uwezo wakutunga mistari na kuimba.
..............................................................
RAY, WOLPER NA IRENE UWOYA WAJINYAKULIA NAFASI ZA JUU UONGOZI WA BONGO MOVIE
Vicent Kigosi maarufu kama Ray ameibuka kidedea na kuwa Mwenyekiti wa Bongo Movie, baada ya uchaguzi uliodumu kwa miezi miwili hivi sasa, na kumbwaga JB aliyekuwa Mwenyekiti katika uongozi uliopita.
katika Uchaguzi huo, Irene Uwoya aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Mpya, huku Jackline Wolper akiibuka kuwa Makamu mtunza Fedha.
Nchiki Mchoma awa katibu Mkuu wa Bongo Movie, Uchaguzi huo ulichelewa kutokana na Tasnia ya Filamu kupatwa na Misiba mfululizo. Ambapo kwa wiki moja walimpoteza Sharo Milionea, John Steven Maganga na Mropero.
.
.............................................................................
PRESIDENT OF CRAZY ATOA NGOMA MPYA
katika Uchaguzi huo, Irene Uwoya aliteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti Mpya, huku Jackline Wolper akiibuka kuwa Makamu mtunza Fedha.
Nchiki Mchoma awa katibu Mkuu wa Bongo Movie, Uchaguzi huo ulichelewa kutokana na Tasnia ya Filamu kupatwa na Misiba mfululizo. Ambapo kwa wiki moja walimpoteza Sharo Milionea, John Steven Maganga na Mropero.
.
.............................................................................
PRESIDENT OF CRAZY ATOA NGOMA MPYA
president of crazy- Mkono wa Mkonole,
Awachana wasanii kupenda kazi za wasanii wenzao, huku akiachia ngoma
kali ya Bayoyo yenye miondoko ya serious comedy.
Ukiongelea sanaa ya vichekesho nchini
nilazima umtaje Mkono wa Mkonole, mabye tangu enzi za Kaole sanaa
Group anakamua vizuri sana kwenye vichekesho.na hivi sasa ameibukia
muziki
Mkonole tayari ametoa ngoma mbili, iliyopo sokono kwa sasa inakwenda
kwa jina la BAYOYO. ngoma ambayo inamiondoko ya serious Comedy.
Mkonole amewashukuru sana watanzania
kwa kupokea kaziyake ya Bayoyo pia kwa kuendelea kuipenda kazi yake
ya sanaa ya maigizo.
Amekemea kitendo cha Wasanii wenzake
kutafuta mbinu za kuupotezea muziki wake ili usivume kuwa sio cha
kiungwana na kuwataka kutokufanya hivyo, zaidi amewataka wasanii
kupenda kazi za wenzao.
....................................................................................................................................
JACKLINE CLIF VIDEO QUEEN VIDEO YA DIOMOND, NATAKA KULEWA
Msanii wenye viwango vya juu Bongo, Nasibu Abdul a.k.a Diamond Plantum au Asali ya Warembo ametoa Video yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki wake.inayokwenda kwa jinala Nataka kulewa, huku mrembo Jacquline Clif akikamua poa msana ndani ya Video hiyo
katika Video hiyo ambayo Diamond kaonyesha uwezo wa juu kwa ubunifu wake nakumtumia mrembo kadhaa kukamilisha dhana ya kuchoshwa na mapenz so anataka kulewa, na swagga za mkali wa HipHop mareemu Michael Jackson zimo ndani.
Tayari ngoma hiyo iko kwenye mitandao na kwenye vyombo vya habari hapa nchini.
................................................................................................................
WASANII KUTOZWA ELFU 20 NA NSSF
Wasanii wa Filamu nchini Wamekubali kujiunga na NSSF
Wasanii wa Filamu wamekubali kujiunga na mfuko wa hifadhi wa jamii NSSF ilikuweza kuwasaidia pale wanapo kutwa na majanga mbalimbali kama msiba na majanga mengine ya kijamii,
akiongea kwa niaba ya Wasanii wenzake, Miss Tanzania wa zamani na Muingizaji wa Filamu nchi Wema Sepetu, amesema wakotayari kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ilikuweza kunufaika na mafao mbalimbali kama Fao la Mazishi na mengineyo.
Naye Msanii Maarufu Odama, alielezea furaa yake juuya uamuzi ambao NSSF umeufanya wakuweza kuwashawishi kujiunga na mifuko ya mafao kwani faida zake ninzuri na kuongeza kuwa Kiwango ambacho kitatozwa cha shilingi elfu 20,000 nichachini kiasi cha wasanii wote wenye uwezo na wasio na uwezo watamudu kutoa garama hizo.
Kwa upande wake Yusuf Mlela, alisema kuwa swala la kujiunga na mfuko wa hifadhi za jamii nimuhimu kwakila mtu na aumbagui mtu, nakuwataka wasanii wote waione fursa hio kuwa ya kipekee kwao
........................................................................................................................................................................
Msanii wa Muziki na Maigizo nchini Shilole, ameshindwa kuimba wimbo uliotungwa kwaajili ya kumuenzi mareemu Sharo Milione, aliyepoteza maisha taree 26 majira ya saa 2 usiku, baada ya kufika Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga.
Wasanii mbali mbali wa Bongo Fleva wametoa ngoma inayo itwa KAZAMOYO ya kumuenzi msanii mwenzao marehemu Sharo Milionea, wimbo ulioimbwa na kurekodiwa katika studio ya Kiri Records chini ya Producer C9
Miongoni mwa wasanii walioshiriki katika nyimbo hiyo, ni Shilole, Barnaba, Sheta, Richimavoko, Dayna Nyange, Suma Mnazaleti, Kanali Top na wengine wengi
Hatahivyo kundilake la zamani la Watanashati nao kwa upande wao walitoa Ngoma ya kumuenzi Mareemu Sharo Milionea
2 comments
inapendeza sana blog yako. hongera kwa kuweka habari nzuri.
Asante sana endelea kutembelea ukurasa hu
EmoticonEmoticon