CD ZISIZO NA CHATA YA TRA KUPIGWA STOP JULY MOSI

Baraza la sanaa Tanzania kwa kushirikiana na Baraza la hatimiliki nchini zimejipanga kuzuia mauzo ya CD za wasanii wa bongo ambazo hazina chata ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), ili kuongeza kipato cha wasanii na Taifa kwa ujumla.

Wakiongea na Blog hii leo Dar es salaam, Kaimu katibu mtendaji wa BASATA bwana Godfrey Lebejo na Mtaalamu wa Tehama kutoka COSOTA wamesema zoezi hilo litaanza rasmi July 1 mwaka huu.

Kwa muda sasa wasanii wa bongo wamekuwa wakilalamika kuibiwa kazi zao, hivyo mamlaka hizi zimeamua kutumia mbinu mpya ya kudhibiti kazi hizo kwa lengo la kuinua maslahi ya wasanii.

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR (ZEC) IMEFUTA MATOKEO YA UCHAGUZI

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi zanzibar salim jecha salim ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo kwa madai kuwa kumekuwepo kwa kura nyingi kuliko idadi iliyopo kwenye daftari la wapiga kura.
Akitangaza suala hilo mwenyekiti wa zec amesema kumetokea kuwepo kwa dosari nyingi kwenye upigaji kura jambo ambalo amelitaja kuwa sio wa haki.
"Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika." amesema salim jecha
Amesema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukuwa vitambulisho vyao vya kupigia kura".

WATU WANNE WAKAMATWA KWA KUNUNUA KADI YA MPIGA KURA MOROGORO



Ikiwa imebaki siku chache kuelekea uchaguzi mkuu katika hali isiyo ya kawaida watu wanne wasiofahamika itikadi zao za kisiasa  wamekamatwa na wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) kwa madai ya kupita katika kata za manispaa ya morogoro na kudai shahada za wapiga kura kwa nguvu na kuanza kuorodhesha majina ya wananchi na namba zao za simu




kwa upande  wananchi mashuhududa   waliokumbana na watu hao  katika harakati za  kuwaandikisha  wapiga kura majina  wameeleza jinsi watu hao walivyokuwa wakifanya zoezi hilo  kwa kudai kwa lazima shahada za kupigia kura ambapo baadhi ya watu  walikubali na wengine wafikisha  jambo hilo kwa afisa mtendaji wakata na wananchi waliamua kuungana na kuwakamata na kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi cha mji wa morogoro.

MHE. DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA NDEGE



Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la ludewa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi ccm mhe. deo filikunjombe na wengine watatu wamefariki dunia katika ajali ya chopa iliyotokea eneo la hifadhi ya selous

Akidhibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi poul chagonja amesema ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria wanne wakitokea dar es salaam kuelekea njombe na waliotambuliwa mpaka sasa ni rubani wa ndege hiyo capten willium silaa na deo filikunjombe

Kamishna chagonja amesema jeshio la polisi limaendelea na uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y DKK unaendelea na kuwa abiria wengine wawili bado hawajatambuliwa kwa majina yao.
sauti ya kamishna chagonja akielezea zaidi

Kategori

Kategori