MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-

Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.

Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.

Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.

MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).

Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).


Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

BEI ZA UMEME JUUU...... TANESCO YAZIDI KULEMEWA NA MADENI SASA YAFIKIA BILIONI 456.8 MIZIGO WABEBESHWA WANANCHI.

Mamlaka wa udhibiti wa nishati na maji EWURA hii leo jijini Dar es salaam wametangaza kupanda kwa bei za umeme ifikapo Januari 1. 2014 kutoka asilimia 67.87 kutoka asilimia 40.29 bei inayotumika hadi hivi sasa.


 Akitangaza ongezeko la bei hizo Mkurugenzi wa udhibiti uchumi wa EWURA Bwana Felix M.Mngamlagosi amesema wamepandisha bei hizo kutokana na Tanesco kuelemewa nakuwa shirika hilo lina hali mbaya kifedha.



"EWURA imebaini kwamba hali ya kifedha ya shirika la umeme sio nzuri kwani limeendelea kupata hasara ya shilingi Bilioni 47.3 katika mwaka 2010 mpaka kufikia Bilioni 223.4 mwishoni mwa mwaka 2012, hivyo kuinusuru shirika hilo tumekubaliana kuongeza bei za umeme"amesema Felix

RIPOTI YA TOKOMEZA UJANGILI YA THIBITISHA SERIKALI KUUSIKA NA VITENDO VYA MAUAJI, UBAKAJI, UDHALILISHAJI NA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

JK APEWA RUNGU KUAMUA,
PINDA NAYE MAJI YA SHINGO,
MAWAZIRI WA 4 MATUMBO JOTO BUNGE LATAKA WAVULIWE MADARAKA,WAMTAKA KAMANDA ALIYE SIMAMIA ZOEZI HILO..........


Kutoka Bungeni Dodoma




Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hii leo wameungana na kukemea matendo ya kikatili yaliyofanya kipindi cha zoezi la “TOKOMEZA UJANGILI ” na kumtaka Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda kujiuzulu wadhifa wake kwa kushindwa kuwa simamia Mawaziri ambao zoezi hilo lilifanywa chini ya Wizara zao.


Mawaziri hao ni Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ambaye ni Waziri wa Ulinzi, Mhe Emmanuel Nchimbi ambaye ni Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Hamis Kagasheki ambaye ni Waziri wa Maliasili na utalii na Mhe. Mathayo David Mathayo ambaye ni Waziri wa Uvuvi na Maendeleo ya Mifugo

SERIKALI YASEMA ITAHAKIKISHA FEDHA ZA MAENDELEO ZINAWAFIKIA WALENGWA

Serikali ya Tanzania inajipanga kuchukua hatua endelevu katika kuhakikisha fedha kwa ajili ya maendeleo zinazotengwa kwa kila sekta zinafikia walengwa kwa wakati.

HONGERA KENYA KWA MIAKA 50 YA UHURU

Rais Uhuru Kenyatta jana amewaongoza wananchi wa Kenya kusherehekea miaka 50 ya uhuru, na kuwataka kudumisha umoja na moyo wa uzalendo ulionyeshwa na wapigania uhuru wa Kenya, kwa kudumisha amani na mshikamano katika taifa hilo.

WANAOSEMA TUME YA UCHAGUZI SIO HURU, NI WAONGO !

Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania imesema ina uhuru wa kutosha kuendesha chaguzi mbali mbali ikiwamo kura ya maoni ya katiba mpya, tofauti na ambavyo wadau wengi wamekuwa wakidai kuwa tume hiyo sio huru.

TANZANIA BADO INAIDAI UGANDA FIDIA YA VITA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inategemea kulipwa na serikali ya Uganda kiasi cha dola za Marekani  milioni nane laki nane na alfu 24, ikiwa ni fedha za fidia ya vita ambayo Tanzania ilipigana nchini Uganda Miaka ya 1977/78.

WEMA ALIPA FAINI YA LAKI MOJA NA KUENDELEA KUPETA MTAANI


Ile kesi ya kumpiga na kumtukana matusi ya nguoni Meneja wa Hoteli ya Mediteranian iliyopo Kawe Beach, Dar, Godlucky Kayombo iliyokuwa ikimkabili Wema Sepetu imetolewa hukumu yake baada ya Wema kuomba iharakishwe kwakuwa alikuwa anasafari.

TANZANIA KUOMBOLEZA KIFO CHA MANDELA KWA SIKU 3

Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
ONDOA VIKWAZO FUNGUA MILANGO YA KUJENGA JAMII JUMUISHI KWA WOTE

ONDOA VIKWAZO FUNGUA MILANGO YA KUJENGA JAMII JUMUISHI KWA WOTE


Watu wenye ulemavu wametakiwa kutokuwa wanyonge na badala yake wajitokeze na kujishugulisha na shuguli mbali mbali katika jamii

Hayo yamesemwa na Mratibu wa kitengo cha walemavu kutoka hosptali ya CCBRT bwana Fredrick Msigana wakati akiongea na Blog hii mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam.

Bwana Fredrick amesema walemavu wamekuwa wanyonge kila mara hivyo wanakosa fursa zingine ambazo wangeweza kujitokeza kuzifanyia kazi na kusema kuwa siku ya walemavu duniani itakuwa fursa kubwa kwao

Kategori

Kategori