UNYAMA NCHINI: KWA MUDA WA MIEZI 6 VITENDO VYA UBAKAJI VIMEFIKIA ELFU 2965, WATOTO 394 WAMELAWITIWA HUKU WATOTO 127 NAO WAKITUPWA


Picha ya mtoto aliye zikwa akiwa hai mbeya na baba yake, hapo ni baada ya kufukuliwa na polisi

Haki ya kuishi kwa watanzania imeendelea kukiukwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita kupitia matukio mbalimbali yaliyo kinyume na haki za binadamu ikiwa ni pamoja na Polisi kuua raia, polisi kuuawa mikononi mwa raia, mauaji ya alibino, mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina, wananchi kuvamia vituo vya polisi, vitendo vya ubakaji.


Hayo yameelezwa katika taarifa ya hali ya haki za binadamu nchini katika kipindi cha kuanzia January hadi June mwaka huu iliyotolewa leo na kituo cha sheria na haki za binadamu ambayo pia inaonesha kuongezeka kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vitendo ambavyo vinatokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi.


Mtafiti kutoka kituo hicho Bwana Pasience Mlowe ndiye aliyesoma taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam ambapo amesema kuwa elimu ya kutosha juu ya haki za binadamu itolewe kwa wananchi ili kuzuia vifo visivyo vya lazima hapa nchini


Katika kipindi cha January hadi june mwaka huu Jumla ya askari polisi 8 wameuawa na wananchi, raia 22 wameuawa chini ya vyombo vya ulinzi, watoto 127 wametupwa, watoto 394 wamelatiwa, vifo 597 vimetokana na raia kujichukulia sheria mkononi, vifo 303 vimetokana na imani ya kishirikina na vitendo 2965 vya ubakaji vimeripotiwa.


Katika matukio ya kubakwa huko ukerewe mwanza mwanaume wa miaka 40 aliyejulikana kwa jina la Emanuel Halala alimbaka mara mbili mtoto wa miaka 8, huku mtoto wa miaka 3 aliye bakwa na mwanaume wa miaka 30 huko mkoani Mbeya matukio ambayo yanazidi kila ripo zinavyo zidi kutolewa


Aidha kuna mtoto aliye zikwa akiwa hai na baba yake huko Mkoani Mbeya kwa madai ya kuachana na mama yake mtoto huyo alikuwa wa miaka 4, lakini katika matukio mengi hakuna hatua zozote za kisheria zilizo chukuliwa didhi ya wahusiaka wa matukio hayo. 

Shirika hili limeitaka serikali kuendesha kampeni juu ya elimu ya haki za binadamu kama ambavyo wamefaulu katika maleria na ukimwi ilikuondoa matendo ya ukatili na unyanyasaji katika jamii ya watanzania.
DR. SLAA SIMTAMBUI TENDWA, ASEMA READ BRIGADE ILIANZA TANGU 2004

DR. SLAA SIMTAMBUI TENDWA, ASEMA READ BRIGADE ILIANZA TANGU 2004



Katibu mkuu wa chama cha Democrasia na maendeleo Chadema Dr. Wibroad Slaa amesema kuwa chama hicho akimtambui msajili wa vyama vya siasa nchini Gaji John Tendwa na kwamba wamefuta kiasi kwamba hawashirikiani nae katika kazi zao.

Dr. Slaa amezidi kusema kuwa hawata shirikiana na  Tendwa mpaka atakapo ondoka madarakani lakini Dr. Slaa alisisitiza kuwa chama chake inaeshimu sana ofisis ya msajili wa vyama vya siasa na kutambua uwepo wake.

"Msajili wa vyama vya siasa anatakiwa kulea vyama vya siasa na sio kukandamiza upande mmoja, yeye hatungi sheria na taratibu zote tumefuata za kusajili chama, labda atuambie nikifungu gani atatumia kukifuta chama" Alisema Dr. Slaa.

Hayo yamekuja baada ya Dr. Slaa kufanya mahojiano na wanahabari alipokuwa kwenye ufunguzi wa kongamano la demokrasia lililo chini ya taasisi ya kimataifa ya inayojishugulisha na mambo ya kidemokrasia inayojulikana kama International Young Democrat Union IYDU.

Hivi karibuni kumekuwa na mvutano mkali kati ya CHADEMA na ofisi ya msajili ambapo ofisi ya msajili ilikitaka chama hicho kuachana na mpango wake wa kuunda vikundi vya ulinzi na endapo kitakaidi atakifutia usajili chama hicho.

Kuusiana na suala la Read Brigade Dr. Slaa amesema kuwa chama chake hakikuanza mwaka huu, tangu mwaka 2004 chama hicho kilikuwa na kikundi hicho hivyo kama kuna sheria inawafunga kufanya hivyo wangependa kudhibitishiwa.

Aidha kuusiana na swala la amani Dr. Slaa amesema kuwa kama serikali ingeweza kutatua matatizo ya ardhi na kuondoa kero hasa za ubadhirifu wa fedha kwa viongozi amesema amani ipo ila nimuhimu kwa serikali kuweka mazingira ambayo yataondoa malalamiko miongoni mwa wananchi.

Hatahivyo Mwenyekiti wa Bavicha Mhe. John Heche amesema mkutano huo wa kuangalia masuala ya Demokrasia katika nchi mbali mbali duniani umeshirikisha nchi zaidi ya 18 ndani ya Afrika na nje ya Afrika.

Heche amesema, yeye ndiye Mjumbe wa bodi ya vijana ya Dunia hivyo wataitumia fursa hii kuleta mabadiliko kwa vijana katika ushirikiano wao kwenye siasa, fursa za ajira pamoja na uwezo wa kuzalisha ili kuweza kujiwezesha kiuchumi.

"Bila vijana kukombolewa taifa halita inuka kikubwa ni kufanya mabadiliko na kuwapa ewezo zaidi vijana na sisi tuna wataka wafanye mabadiliko na washiriki kikamilifu katika kufanya mabadiliko" amesema Heche

Baadhi ya nchi zilizoshiriki katika mkunao huo ni Germany, Italy, Spain, Finland, Kenya, Uganda, Togo na nchi zingine nyingi.

Hatahivyo Heche amesema, chama chake kita wasilisha matatizo yote wanayo kumbana nayo kutoka kwa vyombo vya dola kama kuzuiliwa mikutano yao ya kisiasa, ukatili kutoka kwa polisi dhidi ya raia, vifo katika mikutano yao mfano David Mwangosi na mengine mengi.

Lengo la kuwasilisha hayo nikuuambia ulimwengu yanayojiri hapa nchini. amesema Heche.

KAMPUNI YA PROACTIVE YAJIPANGA KUWAAJIRI WAZAWA KATIKA MIRADI YA GESI LINDI NA MTWARA

Wadau mbali mbali wanao jishugulisha na shuguli za uchimbaji mafuta na gesi katika mkoa wa Lindi na Mtwara, hasa kampuni ya Proactive Solutions ambao wamejipanga kuwapa elimu vijana wa Lindi na Mtwara jinsi ya kufanya kazi katika makampuni ya kuchimba gesi


Wakazi wa Proactive Sulution akiwa kwenye banda lao. Loveness Nathan na Novatus Mango.


Akiongea na Blog hii hapo jana Mkurugenzi mtendaji wa kampuni

Proactive Solutions bwana  Nestory Phoye amesema kampuni ya 

ke itatoa elimu kwa vijana wa mtwara ili waweze kufanya kazi

katika makampuni mbalimbali kwani bila kupata elimu hiyo 

kufanya kazi itakuwa tabu.



Shughuli za uchimbaji na uzalishaji wa Gesi na mafuta katika mikoa ya Lindi na Mtwara utagharimu kiasi cha Dola 60 za kimarekani, ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 97 za kitanzania.


Wadau hao wamejadili njia za kutumia ili kuweza kuwahusisha wazawa katika miradi yao na jinsi ya kupata eneo la kufanyia shughuli zao za uchimbaji wa gesi katika mikoa hiyo.


Corporate sales manager bi Jamila Holaki akitoa maelekezo ya bidhaa zao katika mkutano wa wadau wa Gesi na Mafuta

Akiongea na waandishi wa habari katika mkutano huo, Mkurugenzi
 Mkuu wa TPDC Bwana Yona Kilaghane amesema kuwa lengo lao
 kubwa ni kuwashirikisha wazawa katika shughuli zote za uzalishaji
 na kuongeza kuwa gesi itasindikwa katika mikoa hiyo ya Lindi na 
Mtwara.


Mkutano huo ulioanza leo na kumalizika kesho jijini Dar Es Salaam utafungwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo.



BENKI YA NMB YAFADHILI MAAFISA MAENDELEO WA VIJANA NCHI NZIMA

Waziri wa Habari, Vijana, Tamaduni na Michezo Dkt. Fenera Mkandara akiongea katika semina hiyo 

Benki ya NMB imefadhili semina kubwa iliyohusisha maafisa maendeleo wa vijana kutoka nchi nzima kwa lengo la kujadili maendeleo ya vijana kuanzia ngazi ya halmashauri ilikuweza kuimarisha utendaji kazi kwa vijana wa mikoa na Wilaya



Semina hiyo ya siku mbili ilifanyika katika kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, ambapo Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Mhe. Dkt Fenera Mukangara ambaye naye aliishukuu Benki hiyo kwa ufadhili mkubwa na kujitolea ili kufanikisha semina hiyo.

Meneja mahusiano wa NMB Josephine Kulwa akiongea katika semina hiyo
 Hivi karibuni Benki ya NMB ilifungua milango kwa wenye mahitaji ya mikopo ya bei rahisi na nafuu, huku wakisisitiza kuwa wana nunua mikopo ilikuongeza uduma kwa wateja wao
JESHI LA POLISI LA KANUSHA KUMLENGA MNYIKA NA BOMU, WAKAMATA KIWANDA CHA SILAHA DAR, NA MAJAMBAZI SUGU 8

JESHI LA POLISI LA KANUSHA KUMLENGA MNYIKA NA BOMU, WAKAMATA KIWANDA CHA SILAHA DAR, NA MAJAMBAZI SUGU 8

Picha hii ahiusiani na habari hii


Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es salaam, hii leo limekanusha tuhuma kuwa Bomu lililo lipuka katika mkutano wa Chadema uliofanyika kwenye viwanja vya Sahara Mabibo siku ya Jumamosi tarehe 21/07/2013 halikuwa limemlenga Mhe. John Mnyika ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo kama taarifa za awali zilivyo eleza

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam DCP Ally Mlege amesema taarifa zimekuwa zikipotoshwa juu ya tukio hilo, lakini ukweli ni kuwa bomu hilo lililipuka kwa bahati mbaya na hakuna mtu yeyote aliye jeruhiwa

Bomu hilo lililipuka kwa bahati mbaya baada ya Askari no. E.5340 D/CPL JULIUS ambaye alikuwa ndani ya gari la Polisi lenye namba PT 1902 alipokuwa anasogeza Box lenye mabomu ya mamchozi ya kurusha kwa mkono ndipo Bomu hilo likalipuka.

Hatahivyo Chadema hawakuruhusiwa kufanya mkutano eneo hilo lakini baadae waliondoka kwa amani katika eneo hilo bila madhara yeyote kujitokeza na kuamia katika maeneo ya Ubungo na kumalizia mkutano wao. Amesema DCP Ally Mlege


KARAKANA YA KUZALISHA SILAHA MAENEO YA 

KAWE MZIMUNI, NA MAJAMBAZI 8 WANASWA NA 

RISASI 56


Majambazi 8 wamekamatwa na Polisi wa kanda maalum ya Dar es salaam, wakiwa na silaha 5 pamoja na kiwanda cha kienyeji cha kutengenezea silaha na vifaa mbalimbali vya kufanyia uhalifu maeneo ya Kawe Mzimuni, kiwanda hicho kilikuwa chini ya Charles Francis Masunzu mkazi wa eneo hilo

wengine ni Matula Rashid dereva pikipiki mkazi wa mbezi, Omary Hassan kinyozi mkazi wa Mabibo, Mardha Muhagama mkazi wa Mbezi Kibanda cha mkaa na Mwasiti Maulidi mkazi wa mbezi msumi, watuhumiwa walikuwa na SMG yenye usajili no.02704 ikiwa imekatwa kitako na risasi 20 ndani yake.

Bunduki hiyo SGM no.02704 aliporwa Askari Polisi Wilaya ya Rufiji akiwa anasindikiza magari toka ikwiriri mkoani pwani mwaka 2007, majambazi hayo wametumia silaha hiyo kwa takribani miaka 7.

Aidha baada Charles Francis Masunzu mkazi wa mzimuni baada ya kufanyiwa upekuzi alikutwa na Shortgun moja no. 2539 double bore, Reffile 3 iliyo sajiliwa kwa no. TZ CAR 42871, Reffile 3 iliyosajiliwa kwa no. CAR83744,Reffile 3 ikiwa imefutwa namba, Pistol KJW Works, pamoja na mitutu 5, pingu,risasi 36 na maganda 17 ya risasi, mkebe wa Short gun, funguo mbali mbali, misumeno ya vyuma na vielelezo zingine vingi vinavyo husiana na uhalifu

Pia katika msako mwingine maeneo ya Kijitonyama Polisi walikamata Maragi ya wizi 5 Engine 3 za magari, vipande vya magari yaliyo katwa huku wezi 5 wamagari wakitiwa nguvuni.

Wahusika katika uhalifu huo ni Godlove Damasi, Anna Kway, Sharif Ahamad, Salehe Abdala Ally, pamoja na Nassoro Mohamed

AMIRI JESHI MKUU RAIS JAKAYA KIKWETE AWAONGOZA MAMIA KUAGA MIILI YA WANAJESHI 7 WA TANZANIA WALIOUWAWA DARFUR


Rais wa Tanzania Jakaya Kiwete amewaongoza maelfu ya waombolezaji katika kutoa heshima zao za mwisho kwa wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa kwa kushambuliwa na waasi Darfur nchini Sudan walipokuwa wakilinda amani.


Rais Kikwete amesema nchi ya Sudana ifanye uchunguzi wa haraka juu ya vifo vya wanajeshi hao ili kubaini ni kina nani wamehusika katika shambulio hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa” Alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa Wanajeshi wetu walienda kuwalinda ili waweze kuwa na amani katika nchi yao na sivinginevyo. Alisema




Miili ya wanajeshi hao iliwasili jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi, na kupokelewa na mamia ya waombolezaji walioongozwa na makamu wa rais Dokta Gharib Bilal, katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya kijeshi ya Lugalo.

Zoezi la kuwaaga wanajeshi hao imefanyika katika uwanja wa makao makuu ya jeshi eneo la Upanga jijini DSM, ambapo wanajeshi wawili kati yao watasafirishwa visiwavi Zanzibar kwa mazishi


Wanajeshi hao ni pamoja na Sajenti Shaibu Shehe, Corporal Oswald Chaulo, Corporal Mohammed Ally, Corporal Mohammed Chukilizo, Private Rodney Ndunguru, Private Fortunatus Msofe na Private Peter Werema.

Rais wa Sudan Omar Al Bashir alimhakikishia Rais Jakaya Kikwete kuwa wote waliohusika katika kuwashambulia wanajeshi hao na kuwaua watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Rais Bashir alitoa ahadi hiyo wakati wa mazungumzo na Rais Kikwete na kuongeza kuwa anaamini waliohusika na mauaji hayo walikuwa wahalifu na kuwa lazima wasakwe.

SHOW LOVE “NELSON MANDELA INTERNATIONAL DAY”


Wananchi wa Afrika kusini hii leo wame sherehekea siku ya kuzaliwa kwa Raisi wao wa kwanza bwana Nelson Mandela kwa kufanya shuguli mbalimbali za kijamii.  


Siku hii ya mandela ni miongoni mwa siku kuu za kidunia mbayo watu wanahimizwa kutoa kwa kusaida jamii inayo wazunguka na kufanya mema.


Maeneo mbalimbali ya Miji mkubwa nchini Afrika Kusini imepambwa kwa mabango ya picha za raisi huyo kama ishara ya kumuenzi


Wananchi wa Afrika kusini wametumia dadika 65 kwaajili ya kusaida watu mbalimbali

MIILI 7 YA WANAJESHI WALIO UWAWA DARFUR KUWASILI NCHINI HAPO KESHO

Miili ya wanajeshi 7 waliofariki huko nchini Sudan - Darfur huenda ikawasili hapo kesho baada ya kupewa heshima za mwisho na majeshi yanayolinda amani nchini humo hii leo

Habari zilizo andikwa na mtandao wa UNAMID zinasema tayari miili hiyo imeagwa tangu majira ya mchana na kuanza safari ya kuletwa nchini kwa mazishi








Hatahivyo taarifa ambazo hazijathibitishwa na Blog hii kwani jitihada za kuwasiliana na msemaji wa jeshi ziligonga mwamba baada ya kutopewa ushirikiano wa kutosha na simu kuita bila kupokelewa

Taarifa zinasema kati ya wanajeshi 14 waliokuwa mahututi 4 tayari wamefariki Dunia....... Blog hii itakujuza zaidi kadri habari zitakavyo kuwa zinatufikia      = Picha kwa hisani ya Michuzi Blog
MNYIKA AMJIBU MGIMWA TOZO ZA SIMU, APINGA KUSEMA WABUNGE WALIPITISHA

MNYIKA AMJIBU MGIMWA TOZO ZA SIMU, APINGA KUSEMA WABUNGE WALIPITISHA

Alia na wananchi kuongezwa mzigo mkubwa wa kodi, na kutoa hatua 7 ambazo amemtaka waziri wa fedha kutolea ufafanuzi huku akieleza jinsi anavyo hamasisha wananchi kupinga tozo hizo

   > Ataka maandamano,
   > Sahihi ya wananchi wanao pinga kupandishwa kwa tozo hizo,
   > Wabunge waliopitisha sheria hiyo watajwe,
   > Wananchi wapewe taarifa kamili ilikuwaje sheria hiyo ikapitishwa.

Habari kamili

KAULI YA WAZIRI WA FEDHA KUHUSU KODI YA LINE ZA SIMU NI KIELELEZO CHA UDHAIFU WA SERIKALI NA UZEMBE WA BUNGE; NIANDIKIE SASA KUHUSU HATUA ZA KUCHUKUA JUU YA SUALA HILI KUPUNGUZA MZIGO WA GHARAMA ZA MAISHA KWA WANANCHI

Katika kipindi cha Hot Mix cha EATV muda mfupi uliopita Waziri wa Fedha amesema kwamba mawazo ya kutoza elfu moja kwa mwezi kwenye kila laini ya simu ni ya wabunge. 

Kauli inayokaribiana na hiyo imewahi kuandikwa pia na Naibu Waziri wa Wizara yenye dhamana na sekta mawasiliano kwenye mitandao ya kijamii katika siku za karibuni. Baadaye alifuata Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na sasa waziri mwenyewe. Mwaka 2012 nilitahadharisha kuhusu udhaifu wa Rais (na Serikali) na uzembe wa Bunge katika masuala yanayohusu maandalizi ya bajeti, hususan kutozingatiwa kwa mpango wa taifa wa maendeleo na ongezeko la mara kwa mara la gharama za maisha kwa wananchi. Kwa kauli hizi za Serikali udhaifu na uzembe huo unaendelea kujihidhirisha.

Kauli hizi za Serikali ni za kujivua mzigo wa lawama baada ya malalamiko ya wananchi kuhusu kodi hii na nyinginezo kwa kuhamisha mzigo huo kwa wabunge.

Ni muhimu badala ya kutoa kauli za ujumla za kulaumu wabunge, Serikali ijitokeze itaje kwa majina na wabunge gani hasa walitoa mawazo hayo. Mimi sijawahi kutoa wazo hilo wala kuliridhia. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwenye Hotuba yake juu ya Muswada wa Sheria ya Fedha ilipinga pendekezo hilo lililokuwepo katika jedwali la marekebisho lililowasilishwa na Wizara ya Fedha. Katika kuhakikisha kwamba kifungu hicho hakipitishwi, niliwasilisha jedwali la marekebisho ya sheria kutaka kifungu hicho kiondolewe katika muswada wa sheria ya fedha na marekebisho yake yaliyowasilishwa na Serikali.

Hata kama ikiwa ni ukweli kwamba wazo hilo ni la baadhi ya Wabunge (ambao ni muhimu wakatajwa kwa majina), Serikali inayokwepa kutetea maamuzi ambayo Serikali yenyewe imeyaunga mkono inadhihirisha kwamba imechoka na imepoteza uhalali kwa kimaadili kwa kushindwa kukubalika mbele ya wananchi wake yenyewe (illegitimate government) . 

Mamlaka na madaraka ya Bunge kwa mujibu wa katiba ibara ya 63 ni kuishauri na kuisimamia Serikali. Katika kutekeleza mamlaka hayo, Bunge ni chombo cha uwakilishi wa wananchi na chenye mamlaka pia ya kutunga sheria na kupitisha bajeti ya nchi. Hata hivyo, ibara ya 99 ya Katiba imeweka mipaka kwa mamlaka hayo ya Bunge inapokuja suala la kutunga sheria ya fedha kama hii iliyoongeza mzigo wa kodi kwa wananchi. Mamlaka hayo yamewekwa kwa kiwango kikubwa mikononi mwa Rais kupitia Waziri wake mwenye dhamana.

SOMA ZAIDI HAPA

KAULI YA WAZIRI WA FEDHA MHE. WILLIUM MGIMWA AMBAYO ANAPINGWA NA MNIKA
KULETWA KWA MIILI YA WANAJESHI 7 WATANZANIA WALIOFIA DARFUR BADO HAIJAJULIKANA

KULETWA KWA MIILI YA WANAJESHI 7 WATANZANIA WALIOFIA DARFUR BADO HAIJAJULIKANA


Photo: Natuma salamu za pole kwa amiri jeshi mkuu,ndg za marehemu na wanajeshi wote kwa msiba huu mkubwa uliotukuta.Wamekufa wakiwa kazini wakitekeleza majukumu yao ya kazi.Mungu awape moyo wa subira na uvumilivu wananchi,wanajeshi wote na wafiwa.R.I.P MAKAMANDA WETU.

Jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ limesema linasubiri matokeo ya uchunguzi wa Umoja wa Mataifa juu ya kikundi kilichohusika pamoja na mazingira ya mashambulizi yaliyosababisha kuuawa kwa wanajeshi 7 wa Tanzania wanaolinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Hot Mix kinachorushwa na EATV, msemaji wa jeshi hilo Kanali Kapambala Mgawe amesema jeshi linasubiri ripoti ya umoja wa mataifa ili kuamua ni lini miili ya marehemu italetwa nchini, 

Aidha amekanusha juu ya taarifa zilizo sambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jeshi hilo limetoa majina ya wale waliofariki katika shambulio hilo

"Kuna baadhi ya majina tume yaona kwenye vyombo vya habari lakini sisi hatukutoa majina ya wale walio uwawa, Jeshi lina utaratibu wake katika matukio kama haya sijui haya majina nani kawatajia, hivyo siwezi kusema ni nani ameuwawa kwani majina bado hayaja wekwa hadharani" amesema

Kanali Kapambala Mgawe amesema, utaratibu wa kijeshi nikuwa mtu anapo uwawa, nilazima ndugu wakaribu waambiwe kwanza na jinsi ya kukabiliana na hali hiyo nasio kutamka kwenye vyombo vya habari kwani inaweza kusababisha matatizo mengine.

Mtu amefiwa na mtuwake wa karibu wewe unatoa jina lake, je atajiskiaje kusikia kwenye vyomboi vya habari bila kuambiwa kwa utaratibu unao faa, Alihoji na kueleza kuwa kilicho tendeka sio utaratibu mzuri kwani wao ndio walipaswa lutoa taarifa kwa ndugu wa marehemu. Alisema Kanal Kapambala

Amesema kwa hivi sasa jeshi hilo halina mpango wowote wa kuongeza wanajeshi nchini Sudani kwani walioko wanatosha lakini endapo watatakiwa na umoja wa mataifa kufanya hivyo wataongeza.

Jumla ya wanajeshi 875 walikuwa nchini humo tangu mwezi February mwaka huu, kwa maana hiyo walio hai mpaka hivi sasa ni 868 (ukitoa 7 waliofariki) na miongoni mwa hao walio hai 14 walijeruhiwa na wapo katika hali mbaya
.Wanajeshi hao walishambuliwa wakati wakisindikiza msafara wa waangalizi wa amani wa Umoja wa Mataifa, Tangu Tanzania ianze kupeleka majeshi yake mwaka 2007 huko Darfur ni mara ya kwanza kwa Jeshi letu kupoteza watu wake. Pole Tanzania Pole kwa ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu.

CCM YA BURUZWA NA CHADEMA ARUSHA, WASHINDA KATA ZOTE VIONGOZI WA DINI NAO WAPONGEZA UTULIVU ULIOPO

CCM YA BURUZWA NA CHADEMA ARUSHA, WASHINDA KATA ZOTE VIONGOZI WA DINI NAO WAPONGEZA UTULIVU ULIOPO




Viongozi wa Madhebu ya Kidini mkoani Arusha wameeleza kuridhishwa na hali ya amani iliyotawala katika uchaguzi mdogo wa Madiwani katika kata za Jiji la Arusha na kuzisifu vyombo vya dola pamoja na wananchi kwa kudumisha amani na kuepuka vurugu zisizo za lazima.

Habari zilizo ifikia Blog hii toka mkoani humo zinasema, Viongozi wa kidini Wakizungumzia hali hiyo, kutoka katika madhehebu tofauti wamesema, amani itaendelea kuwepo kwani utulivu ulioonyeshwa na vyombo vya dola pamoja na wakazi wa Arusha unapaswa kuendelea katika chaguzi zijazo.

Naye Mkurugenzi wa kituo cha Taarifa kwa wananchi Deus Kibamba amesema watendaji wa serikali wakiweza kusimamia demokrasia kwa kiwango hicho, hakuna vurugu wala umwagaji wa damu utakaotokea hapa nchini.

Kwa upande mwingine, Wanachama wa Chama cha Mapindizi wamewataka viongozi wa Chama hicho kwa Wilaya ya Arusa kujithamini kutokana na anguko walilolipata katika Uchaguzi huo, ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeshinda katika kata zote nne.

Chama cha Chadema kimethibitisha ushindi wake baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye mkoa huo, Uchaguzi huo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na ulikuwa unachukuliwa kama kipimo cha siasa komavu mkoani humo
Chadema kimeongoza katika vituo vyote136 vya kupigia kura katika Kata za Elerai, Kaloleni, Kimandolu na Themi.
Matokeo hayo yameonyeshwa kulingana na idadi ya vituo katika kata mbali mbali ambapo Matokeo ya Uchaguzi katika kata hizo nne na vituo 136 yalikuwa kama ifuatavyo:
Kata ya Elerai CHADEMA kura 2,047  CCM kura 1,471
Kata ya Themi CHADEMA kura 674 CCM kura 326
Kata ya Kaloleni CHADEMA kura 1,470 CCM kura 330
Kata ya Kimandolu CHADEMA kura 2,761 CCM kura 1,163


Baadhi ya Kata hizo zilikuwa wazi tangu mwaka 2011 baada ya Chadema kuwatimua wanachama wake waliokuwa madiwani Estomih Mallah(Kimandolu), John Bayo (Elerai), Reuben Ngowi (Themi) na Charles Mpanda (Kaloleni

MAKAMBA AOMBA SERIKALI IAONDOWE VIKWAZO VIJANA




Serikali imetakiwa kuhakikisha vijana wanapewa ewezo wa kutumia vipaji vyao kujiajiri na kuajiri wengine kwa kuwaondolea vikwazo vinavyo wakabili bindi wanapo taka kuanzisha biashara au kupata mkopo katika mabenki hapa nchini.




Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mhe. January Makamba wakati wa uzinduzi wa tuzo za vijana chini ya miaka 30, ambapo Mhe. Makamba amesea, kujituma na kutumia fursa kwa vijana inategemeana na vikazo mbavyo kuna muda wanakumbana navyo na kuitaka serikali kuondoa vikwazo hivyo



kijana anataka kusajili biashara yake lakini kuna mlolongo mrefu sana ambao unafanya anakata tamaa, au anahitaji mkopo benki lakini wanahitaji hati ya nyumba huyu kijana anatoa wapi nyumba? Sasa kama serikali ikiangalia hivi nadhani vijana wataweza kuonyesha uwezo wao”Alisema Makamba


Aidha, alisema Mfumo wa elimu wa nchi yetu nao urekebishwe iwe elimu ambayo itawapa vijana uwezo wa kutatua matatizo yanayo mkabili, kushirikiana na wengine na sio elimu tu ambao bado itamfunga kuendana na dunia ya sasa. Alisema




Mhe. Makamba amesema katika Bunge lijalo Serikali imeandaa muswada ambao utawasilishwa juu ya kuwepo kwa Baraza la Vijana kwaajili ya kushugulikia matatizo ya vijana kama ajira, elimu na baraza hilo liwepo kisheria ili liweze kuwa na nguvu

baadhi yetu tumekuwa tukipenda bara hili lianzishwe haraka kwani litao tao majibu kwa matatizo ya vijana na serikali imejipanga vyema kuhakikisha kuwa bunge lijalo tunajadili nini cha kufanya” Alisema





Naye Mkurugenzi mkuu wa Youth for Africa bwana Awadhi Malasi amesema Taasisi yake inawakumbuka sana vijana kutokana na mchango wao katika jamii hivyo tuzo hizo zitawapa motisha vijana wengine kufanya vyema zaidi. Amesema

Awadhi amesema hii ni mara ya kwanza kwa taasisi hiyo kutoa tuzo hizo hapa nchini lakini kila mwaka kutakuwa na mabadiliko juu ya tuzo hizo kwani hata mikoani na watapewa fursa ya kushiriki




Kwa kupata washindi katika tuzo hizo unapiga kura kupitia mtandao wao ambao ni 
http://www.youthawards.or.tz  au kwa njia ya simu andika YOA acha nafasi kisha tuma kwenda 15584. Tuzo zitatolewa tarehe 17/8/2013.

A NEW CAR DESIGNED IN IRINGA TANZANIA

Keneth Mwangoka akiwa ndani ya Gari lake
Gari lenye namba za usajili T 605 ADU Toyota Actaso mali ya Keneth Joseph Mwangoka kutoka mkoa wa Iringa- Tanzania imekuwa kivutio kikubwa kutokana na Dizain yake, Gari limegarimu Millioni 8 kuikamilisha kwani inatumia baadhi ya vifaa kutoka Dukani


Gari hilo lililo lililoundwa na Vyuma chakavu pamoja na mbao na urembo mwingine wakawaida kutengeneza Bodi ya gari hiyo. Akiongea na Blog hii mmiliki wake bwana Keneth amesema kwa mtu yeyote atakaye hitaji kutengenezewa gari kama hiyo wawasiliane kwa simu no. 0754 005004 


Gari hiyo imeundwa kwa kutumia Engine ya Toyota, matairi ya kawaida huku spea zingine zikiwa ni za dukani na ameiundwa kwa muda wa miezi 6. Lengo la Keneth ni kuwataka vijana hasa ambao hawana ajira kuwa wabunifu kuliko kukaa tuu mitaani
SHILINGI BILLIONI 160 KUKUSANYWA KWA MWAKA KUPITIA TOZO ZA LAINI YA SIMU YA KILA MWEZI

SHILINGI BILLIONI 160 KUKUSANYWA KWA MWAKA KUPITIA TOZO ZA LAINI YA SIMU YA KILA MWEZI

Photo: HOTMIX (11:00 Jioni): Leo ni siku ya ongezeko la watu duniani, Je idadi kubwa ya watu inachangia vipi maendeleo ya Taifa?

Serikali yasisitiza kuanza kukata kodi ya Tshs 1000 kwa kila laini ya simu, yasema inahitaji kukusanya bilioni 160, Je hii ina athari gani kwa watumiaji wa simu?

Ndani ya studio tutakuwa mastaa wa movie na music, pia utapata nafasi ya kuliona gari lililobuniwa na watanzania na kutengenezwa na watanzania, unadhani mwendo-kasi wa gari hili utakuwa ni kilomita ngapi kwa saa?

Pamoja na story kibao za leo, studio tutakuwa na Selemani Zedi mbunge wa Bukene mkoani Tabora, mtupie swali lolote hapa naye atakujibu.


>TOZO YA LAINI KWA MWEZI WABUNGE NDIO WALIPITISHA
>YADAIWA ITAPATIA NCHI BILIONI 160
>BILIONI 231 NAZO ZATOLEWA NA SEEDEN, 
>NA ADB BANK YAIKOPEHA TANZANIA BILIONI 286

Serikali imeendelea  kusisitiza kodi ya Line za simu ambayo itakatwa kila mwezi kwa watumiaji wa simu nchini

Akijibu swali lililo ulizwa na mmoja wawaandishi wa habari katika mkutano wa kusaini mkataba na nchi ya Sweeden, Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa amesema serikali ili chukua uamuzi huo baada ya wabunge ambao ni wa wakilishi wa wananchi Bungeni kukubali kupitisha Bungeni swala hilo

“Wananchi wana lalamika lakini wawakilishi wao ambao ni wabunge ndio walipitisha aina hii ya tozo hivyo serikali inajipanga kuanza mchakato wa kupata fedha hizo ili kuweza kuongeza kipato”Alisema

Aidha Dr. Mgimwa amesema kuwa serikali itapokea shilingi Billioni 160 kwa mwaka kutokana na kukata tozo hizo”Amesema

Akitoa ufafanuzi wa matumizi ya fedha hizo Dr. Mgimwa amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika kusaidia maitaji ya jamii kama vile Hospitali, mashule na barabara”Alisema Dr. Mgimwa

Hii inamaana kama kila mwaka mmiliki wa line moja atatozwa shilingi Elfu 12 hali ni tete kwa wale wanao miliki laini zaidi ya Mbili.

Tozo hiyo itaanza kukatwa rasmi kuanzia Julai 2013 mwezi huu

Wananchi wengi wamezidi kulalamikia tozo hizo huku baadhi ya wabunge nao wakidai kuwa swala la laini za simu aikuwekwa Bungeni kujadiliwa kwa wazi 

BILLIONI 231 KUTOKA SWEEDEN KUENDELEZA MITAMBO YA UMEME NA UCHUMI

Serikali ya Tanzania imepokea shilingi bilioni 231 kutoka serikali ya Sweden kwa ajili ya kuendeleza miradi mbalimbali nchini

Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa amefafanua kuwa  mikataba miwili iliyotiwa saini leo ni kwa ajili ya matumizi tofauti ambapo mkataba wa kwanza wa shilingi bilioni 202 unalenga kuongeza nguvu katika kuhamasisha ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini

Mkataba wa pili wa jumla ya shilingi bilioni 129 utaelekezwa katika shughuli za ukarabati wa mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo Hare jijini Tanga, nakuongeza megawati 21 katika umeme wa taifa

“Hivi sasa hare inazalisha megawati zisizo zidi tisa 9, nakuwa serikali imeamua kuongeza uzalishaji wake kwani kuna upatikanaji wa maji ya kutosha katika eneo hilo” amesema.

Dr. Mgimwa amesema, Hii ni sehemu ya jitihada za serikali kufanyia kazi vipaumbele vya mwaka huu wa fedha 2013/2014 ambapo kipaumbele cha kwanza ni miundombinu ya Nishati ya umeme na barabara.

Serikali ya Sweden imekuwa mstari wa mbele miongoni mwa washirika wa maendeleo nchini kusaidia ukuaji wa sekta ya nishati hususani Umeme hapa nchini

BARABARA YA ARUSHA-HOLILI KUJENGWA AUGUST 2013 MAPAKA DEC 2018

Barabara ya Arusha-Holili mpaka Taveta na Voi nchini Kenya inatarajiwa kuanza ujenzi wa kupanua barabara hiyo baada ya Tanzania kusaini mkataba wa mkopo wa shilingi Billioni 286 kutoka Banki ya maendeleo Afrika AFDB

Akiongea na waandishi wa Habari hii leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Fedha Mhe. Willium Mgimwa amesema kuwa ujenzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 42, utaanza August mwaka huu na kumalizika December 2018.

Aidha, Mradi wa ujenzi wa barabara hiyo itasaidia usafiri wa watu zaidi ya Laki 5 na 84 kwa upande wa Tanzania ikiwa pamoja na kurahisisha usafiri kwa watalii watakao tembelea mkoa wa Arusha na Kilimanjaro

Tanzania itarudisha mkopo huo baada ya Miaka 40 lakini mda wa kuanza kulipa mkopo huo ni miaka 5 ijayo, katika kurudisha fedha hizo Tanzania itatoa Asilimia 4.7 huku Kenya ikitoa Asilimia 5.9.

WANAFUNZI EFU 33,683 KUJIUNGA KIDATO CHA TANO2013, 530 WAPELEKWA VYUO VYA UFUNDI, HUKU LAKI 397,437 WAKISOTA MTAANI



Jumla ya wanafunzi 34,213 sawa na asilimia 18.1 ya waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012 kwa madaraja ya I – IV wamechaguliwa kuingia kidato cha tano na vyuo vya ufundi pamoja na taasisi ya menejiment ya maendeleo ya maji kwa mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 2,790 sawa na asilimia 8.9 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Aidha Jumla ya wanafunzi 33,683 sawa na asilimia 18.1 ya waliofaulu wakiwemo wavulana 23,383 na wasichana 10,300 wamechaguliwa kuingia kidato cha tano kwa mwaka 2013 ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.15 ikilinganishwa na mwaka 2012.

Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe Philip Mulugo ndiye aliyetoa taarifa hiyo leo jijini DSM na kusema kuwa idadi kubwa ya wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu ni wa masomo (Tahasusi) ya Sayansi.

Mhe. Mulugo amesema wanafunzi wa some kwa bidii bila kujali aina ya masomo anayosoma, pamoja na kuwasisitiza wanafunzi wa kike kujiamini kuwa wanaweza masomo yote, Alisema

Idadi ya wanafunzi wote waliojiunga na vyuo vya ufundi imepungua kutoka 564 mwaka 2012 hadi 530 mwaka 2013 ambapo wavulana ni 416 wasichana wakiwa 114 tu. Lakini hilo niongezeko kubwa kwa upande wa wasichana ambao kwa mwaka huu wamechaguliwa 144 tofauti na mwaka jana ambao walikuwa 47 tu.

Kuhusiana na baadhi ya wanafunzi ambao tayari wame kwisha anza masomo ya kidato cha tano katika shule binafsi, Mhe Mulugo ametoa ufafanuzi kuwa shule za serikali hufunguliwa Julai ambapo waliochaguliwa watatakiwa kuripoti tarehe 29 Julai

Wanafunzi ambao tayari wameanza kusoma masomo ya kidato cha tano katika shule binafsi na wamefauli katika shule za serikali ni uamuzi wao kuamua kama waendelee na shule za binafsi au warudi kujiunga na shule za serikali ila wasiihusishe serikali” Amesema

Matokeo haya yanaonesha kuwa, shule za serikali zitakumbwa na upungufu wa wanafuzi takribani 10,097 wengi wao wakiwa ni wa masomo ya sanaa.

Kwa taarifa ya Waziri Jumla ya Wanafunzi Laki 397,437 hawacha chaguliwa kujiunga na masomo ya juu, na kati ya hawa kuna waliopata daraja la IV na 0 ambao ndio wengi kuliko waliochaguliwa

VIJANA WALILIA KUTOPEWA BARAZA LAO, KUJADILI RASIMU YA KATIBA

VIJANA WALILIA KUTOPEWA BARAZA LAO, KUJADILI RASIMU YA KATIBA

  



Vijana wote nchini wametakiwa kujiunga bila kujali itikadi zao ili kuweza kupigia kelele kuwepo kwa baraza la taifa la vijana litakalo jadili mambo ya Rasimu ya kuundwa kwa katiba mpya hapa nchini

Akiongea na waandishi wa habari hii leo jijini Dar es salaam, mwenye kiti wa jukwaa la vijana Tanzania bwana Fahami Matsawilly amesema kuwa tunaomba ibara ya 43 itamke wazi kuwa kila kijana anao wajibu wa kushiriki shuguli za kijamii na maendeleo kwa ujumla

“Vijana wote tunaombwa kuungana bila kujali itikadi zetu za kisiasa, kidini, kabila na elimu ili kuweza kutetea changa moto zinazo tukabili hapa nchini

Hayo yote yamekuja baada ya JUVITA kubaini kuwa matatizo yanayowakabili vijana kama Ukosefu wa ajira, makundi kama yale ya Machinga, dereva wa bodaboda na vijana wanao fanya kazi majumbani na makundi mengine ni lazima wawe na chombo kitakacho wa wakilisha kwenye vyombo vya maamuzi ya katiba mpya

Pia amewataka vijana kupeleka mapendekezo yao kwa wawakilishi wa mabaraza ya katiba ili ibara ya 43 iweze kufanyiwa marekebisho

“Cha ajabu baraza la taifa la vijana halimo kwenye rasimu ya katiba mpya, wakati nchi nyingi zenya mabara za ya taifa ya vijana, kwa nini Tanzania hiyo nafasio hakuna” Alisema

Baadhi ya nchi ambazo zina baraza la vijana linaloshigulikia matatizo ya vijana ni pamoja na Costasica, Slovenia, Rwanda , Uganda pamoja na Kenya na nchi zingine nyingi

Uundwaji wa Katiba mpya umefikia katika hatua za mabara ya Rasimu ya katiba mpya ambapo mabaraza hayo yataanza kukaa kuanzia Ijumaa ya wiki hii tarehe 12.

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOJIUNGA NA KIDATO CHA TANO/VYUO KUTANGAZWA LEO




Naibu Waziri wa Elimu Mhe. Filipo Mulugo Asubuhi hii anatarajia kutangaza majina ya wanafunzi walio chaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na wale watakao jiunga na vyuo vya ualimu na ufundi

Majina yakupangiwa shule pamoja na vyuo yamechelewa sana tofauti na ilivyo zoeleka, kwani kwa taratibu za awali majina hayo hutangazwa mwezi wa tano ikiwa ni miezi miwili kabla ya kufungua shule ili kutoa nafasi kwa wazazi na wanafunzi kujiandaa na kujiunga na masomo yao

Katika hali isiyo yakawaida majina hayo yata tangazwa hii leo ikiwa tayari shule zimefunguliwa huku waliingia kidato cha sita wakianza masomo yao huku kukiwa hakuna wanafunzi wa kidato cha sita

Endapo shule itakuwa imefungua ikiwa na wanafunzi wa kidato cha tano basi pia itakuwa maajabu mengi juu ya mfumo wa elimu, Ikumbukwe kwamba matokeo ya wanafunzi hawa kwa mwaka 2012 yalitikisha nchi kutokana na asilimia 80 yawanafunzi kufeli vibaya huku idadi ya wanafunzi wachache ndio walifaulu.

Kutokana na hali hiyo Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda alilazimika kuunda tume ya kuchunguza sasabu za kufeli kwa wanafunzi hao na baadae ikapatikana pendekezo la kufanya standardization ili kuweza kuoka idadi kubwa ya wanafunzi waliofeli na baadae matokeo kutangazwa upya

Hata hivyo baada ya Standardization kufanyika ilitegemewa kuwa wizara itatoa taarifa ya kutangaza ni wali na lini wanafunzi watajiunga na masomo yao ya kidato cha tano kwa wale waliofaulu kwa vyuo na kidato cha nne


Habari zinazo husiana

Bonyeza hapa chini ili kusoma zaidi juu ya matokeo ya kidato cha nne 2012 tangu kutangazwa mpaka hii leo



Habari kamili itakujia hapa hapa .....................

Kategori

Kategori