BIASHARA ZA MNADA- BUNJU ZIMEPAMBA MOTO, VITU BEI CHEE

Wakazi wa Bunju na viunga vyake Jijini Dar es salaam nje kidogo ya mji, huwa wana ifurahia sana siku ya mnada kwani mnadani pana furika sana kwa watu wakila rika huudhuria siku hiyo.

Wao wakienda Mlimani City au Home Shoping Centre sisi tunakutana hapa kwaajili ya mahitaji muhimu tena kwa bei poa... Masikini kwa masikini tunachangiana, siku ya soko ni Kila alhamisi ya wiki



Pamba zote kali zinapatikana, masista duu wa Bunju tuna tokelezea bila shaka tena hadi 1000 moja unapata Top Kali nguo za watoto usiseme

Kizuri zaidi katika siku hii vitu bei ni chee hivyo wananchi wengi wa Bunju ambao ni wakipato cha chini hupata vitu kwa bei poa kabisa




Pamoja na Neema ya punguzo la Bei linalo wawezesha wakazi zaidi ya Elfu 2000 wanaohudhuria sokoni hapo kumudu lakini Soko la Bunju B halina choo cha kuhudumia watu hao siku ya Mnada 

Serikali ingeweza iangalie utaratibu wa kujenga choo cha kulipia ilikuweza kuhudumia wakazi waeneo hilo na kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko



Kwa vitu vidogovidogo vya kupikia kama ilivyo pichani, kuanzia miambili 200/=  unapata mfuniko, 300 mwiko na Ungo 500 tu, na  mazagazaga kibao kwa wale wanaitaji mambo ya kuzawadia kwenye Kitchen Party hapa si mahali pa kukosa kila Alhamisi 

Pichani ni Josephine Joseph, akifurahia jambo mnadani hapo
 Wale mnao anza maisha msijiuliza marambili Bunju B pana kila kitu kwa ajili yenu usiangaike sana kwani masikini wote tunakutana hapa Shoping ya kufa mtu


Hapa unaweza kupata Dishi zima lenya vyombo kwa Elfu 10,000 tu, endapo ukinunua chombo kimoja kimoja itakugarimu maelfu 10 kibao lakini Mnada wa Bunju mambo ni tofauti


Mnada huo ambao hukaa mara moja kwa wiki inahudumia jumla ya Mitaa Kibao ya Bunju, ambao inakadiriwa kuhudhuriwa na wakazi wa eneo hilo zaidi ya Elfu mbili kwa kila alhamisi 

Wafanya Biashara wa maeneo haya uhama hama kutokana na ratiba za minada ya maeneo haya. Mnada wa Tegeta Kibaoni hukaa kila Ijumaa huku maeneo ya Boko ni kila Jumanee na Bunju nikila Alhamisi pia wanatoa huduma hii mpaka maeneo ya Bagamoyo.

SIKU TANO NJE YA BUNGE MHE. LEMA AANGUKIA MIKONONI MWA JESHI LA POLISI



Askari wa Jeshi la Polisi wakilivuta gari la Mbunge Huyo juzi eneo la tukio Chuo cha AIA


Baada ya Mhe. Godbelss Lema kuhusishwa na vurugu za chuo chauhasibu Arusha ( Arusha Institute of Acountancy), hatimaye akamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kibarua kizito cha kupiga kambi nyumbani kwake usiku kucha

Habari zilizo chapishwa na Tovuti ya chama hicho, zinadai kuwa Mbunge huyo hawezi kukamatwa mpaka pale Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda atakapotoa kibali cha yeye kukamatwa


Tarifa ambazo blog hii imefuatilia zina sema kuwa Lema tayari ametiwa mikononi mwa jeshi la polisi baada ya kukamatwa usiku wa manane nyumbani kawake ili kujibu tuhuma zinazo mkabili



Siku mbili zilizo pita Mhe Lema alikuwa kwenye umati wa wanafunzi wa chuo cha Uhasibu Arusha akiwatuliza hasira wakiwa na lengo la kuandamana kutokana na kifo cha mwanafunzi mwenzao Henry Koga ambaye aliuwawa kwa kuchomwa kisu na watu wasio julikana

Mbunge huyo pia anadaiwa kuchochea maandamano yaliyosababisha vurugu kiasi cha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo kuzomewa na kupopolewa mawe na wanafunzi wa chuo hicho

Mhe. Lema alikwenda chuoni hapo ambapo nikaribu kabisa na nyumbani kwake kwa lengo la kutuliza gasia hizo, kitendo ambacho jeshi la polisi ilikiita cha uchochezi

VIDEO IKIONYESHA MHE. LEMA AKIONGEA NA WANAFUNZI KATIKA CHUO HICHO


Hatahivyo, Mhe. Godbless Lema ni miongoni mwa wabunge waliozuiliwa kuingia Bungeni kwa siku 5 baada ya kuhusishwa na vurugu zilizozuka Bungeni,

Mhe. Lema alizuiwa kuingia Bungeni kwakosa la kuwakataza askari kumkamata Mhe Tundu Lissu aliamriwa kutoka nje ya Bunge na Spika wabunge Mhe. Job Ndungai kwakosa la kuingilia hoja ya Mhe. Mwigulu Nchemba Wabunge wengine waliozuiwa ni Mhe. Tundu Lisu, Joseph Mbilinyi, Ezekiel Wenje na Peter Msigwa.

Lema hivi sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Arusha akiusishwa na kuchochea vurugu za wanafunzi wa chuo hicho kuandamana, ambapo jeshi la polisi lilitumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao


MKUU WA MKOA ARUSHA NAYE ALITINGA ENEO LA TUKIO KUTULIZA GASIA , NAHALI YA EWA IKACHAFUKA BAADA YA WANAFUNZI KUMZOMEA

                                                                                                              Hivi sasa chuo hicho kimefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na matukio hayo ya uvunjifu wa amanai

MTOTO ATOROKA NYUMBANI KWAO KWA KUTESWA

Mtoto wa miaka 12 ametoroka nyumbani kwao na kuja katika vituo vya utangazaji vya ITV akiomba kupelekwa kwa mama yake mzazi baada ya kuchoshwa na manyanyaso ya mama wa kambo pamoja na baba yake

Mtoto huyo Tekla Adolf, ambaye anakaa Makuburi External na anasoma darasa la 6 katika shule ya ATLAS PRIMARY SCHOOL iliyoko External


Tekla amesema miongoni mwa mateso anayo yapata nikipigo kikali kutoka kwa mama yake wa kambo aliye mtaja kwa jina la JANET LYMO kuwa ni kung'atwa kwa meno na mama yake huyo siku zingine anamnyima chakula


Baba wa mtoto huyo anaitwa Benard Adolf, ambaye naye hushirikiana na mkwewe Janet kumtesa mtoto Tekla.

Blog hii ilimpigia mama wa mtoto huyu simu ambaye huko mkoani Tanga nakukiri kufahamu mateso anayo pata mwanaye lakini hushundwa kuchukua hatua kwani baba wa mtoto huyo hayuko tayari kuruhusu yeye kuishi na mtoto huyo.

Blog hii inafatilia zaidi juu ya tukio hilo ikiwa nipamoja na kufikisha taarifa polisi ilitaratibu za kisheria zichukue mkondo wake. habari zaidi zitakujia baadae

BAJETI YA WIZARA YA MAJI YA PIGWA CHINI, WABUNGE WAUNGANA – KILIO HAKUNA MAJI NCHINI, WAKATAA BILIONI 500 HAIWEZI KUTATUA TATIZO



KUTOKA BUNGENI



Hii itakuwa historia tangu Bunge hili kuanza, ambalo ni Bunge la 10 kikao cha13, baada ya Wabunge kuacha hitkadi za chama na kusimamia ukweli na hali alisi juu ya Tatizo la maji nchini
 

Hii leo Bungeni, Bajeti ya wizara ya Maji leo haijapitishwa na wabunge, kwakukataa kuunga mkono hoja mpaka njia madhubuti zitakapoletwa kwaajili ya tatizo hilo huku wakilalamika bajeti iliyotengwa ni ndogo kwa jinsi tatizo lilivyo

Wabunge walipaza sauti zao na kumtaka Waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Jumanne  Magembe ajipange nakuacha kuwasilisha hotuba yenye nyaraka za uongo kwao

"Wabunge wengi walisikika wakisema, takweimu hizi umetoa wapi, mara hili eneo halipo tanzania umelitoa wali.... nilazima tusimamie ukweli...siungi mkoni hoja" walimalizia

Wabunge hao ambao walikataa kuunga mkono hoja huku kila mtu akilia na kukosa maji jimboni mwake wakishangaa hotuba ya waziri ambao imeelezea miradi mingi iliyotekelezwa

Hatahivyo hoja hiyo haikupitishwa mpaka itakapo jadiliwa tena bungeni hapo na Mh-Spika wa Bunge Anne Makinda akalazimika kuahirisha bunge huku akiiagiza serikali ikae pamoja na kamati ya bajeti kutokana na kuonekana kuwa bajeti iliyotengwa mwaka huu ni ndogo na haitaweza kumaliza kelele za maji,hivyo kamati ya bajeti pamoja na serikali zikutane pamoja ili wajadili pesa hizo watazitoa wapi

Katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri mkuu Bungeni, imebainika kwamba Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuzalisha mkaa duniani kiasi ambacho kinatishia mazingira ya nchi yetu

"Waziri alijibu hali hiyo sinjema na isiendelee kwani inahatarisha rasilimali zetu, hivyo kuagiza swala hilo kushugulikiwa"

Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zinazozalisha mkaa duniani huku asilimia 3 ya mkaa unaotumika duniani ukitoka Tanzania ambapo kwa siku Tanzania huzalisha Tani 2650 sawa na Tani milioni 10 kwa mwaka ,,,na hapo hapo mkaa huliingizia taifa dola milioni 650 (zaidi ya sh-bilioni moja )vile vile biashara hiyo inategemewa na familia zaidi ya milioni 1 nchini







Prof. Ibrahim Lipumba amewataka watanzania kutunza muungano na kuachana na mawazo ya kuuvunja muungano licha ya matatizo yaliyopo.

Prof. Lipumba ame yasema hayo hii leo jijini Dar es salaam, alipokuwa akiongea na vyomba vya habari,



katika makao makuu ya chama hicho.ambapo amesema tuangalie zaidi juu ya kushugulikia matatizo ilikudumisha muungano kwa maendeleo ya wote

“Watanzania wengi wanaangalia juu ya changa moto zilizopo na badala ya kushugulikia matatizo yaliyopo ilikuweza kusonga mbele kama taifa” Alisema Lipumba

Nikweli kuna matatizo ya muungano, hata mimi ninayajua lakini hayo hayawezi kutufanya kuuvunja muungano, bali tujikite kwenye njia ambazo zitatuwezesha kuujenga muungano huo. Alisema

Kesho maadhimisho ya muungano yatafanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi wa juu watahudhuria sherehe hizo, ikiwa ni miaka 49 ya muungano

Aidha kutokana na vurugu zilizo vuka huko Liwale mkoani Lindi, Prof. Lipumba amewataka wakazi wa maeneo hayo kuachana na maandamano na kuishauri serikali kukubali kukaa chini na wakazi hao kujadili juu ya swala hilo

Hapo jana vurugu vilizuka miongoni mwa wakulima na vyama vya sushirika vya Korosho mkoani Lindi baada ya kutoafikiana juu ya bei halali ya kununulia bidhaa hizo

Prof. Lipumba ameitaka serikali kuwalipa fedha wakulima hao kama walivyo ahidiana kwenye kikao cha mauzo kilicho fanyika mwaka 2012

“Wananchi wali kabidhiwa Tsh. 200/= kwa kilo badala ya shilingi 600/= kama ilivyo ahidiwa na kukubaliwa kwenye mkataba wa mauzo, serikali nilazima iwalipe wakulima kulingana na walivyokubaliana” Alisema

Serikali ifanye utafiti juu ya swala hili, na kuunda chama cha wakulima wenyewe kuuza korosho hizo hili haya yasijirudie. Alisema

Prof. Lipumba pia aliongelea swala la matusi bungeni na kuwataka wabunge kuwa tambua watanzania walio wachagua kuwa hawa vutiwi na hali hiyo hivyo kuacha mara moja.
"HAKIELIMU" SHULE ZA KATA KUPATA UMEME

"HAKIELIMU" SHULE ZA KATA KUPATA UMEME

SERIKALI imesema itakamilisha ujenzi wa shule za Sekondari 1,200 kwa kuweka miundombinu muhimu ikiwemo umeme kupitia Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari awamu ya pili.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Dk. David  Mallole, aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme kwenye Shule za Kata hasa za Bweni.
Mhe.Majaliwa amesema kuwa kwa awamu ya kwanza Serikali imeanza kukamilisha ujenzi kwa shule 264 kwa thamani ya shilingi Bilioni 56.3 ambapo suala la umeme wa gridi ya taifa na  umeme wa jua limepewa kipaumbele.
Ameongeza kuwa Serikali kupitia mfuko wa wakala wa usambazaji umeme Vijijini (REA) imedhamiria kusambaza umeme katika zahanati, shule na visima vya maji vilivyo katika maeneo yatakayonufaika na huduma hii ya umeme Vijijini.
“Mpaka sasa, Serikali imewezesha shule za sekondari 3,385 sawa na asilimia 75 ya shule zote za sekondari nchini kuwa na huduma ya umeme” amesema Mhe. Majaliwa.
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kishirikiana na wadau na kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo kuhakikisha dhamira ya kuziwezesha shule na maeneo mengine yanayotoa huduma za jamii yanakuwa na huduma ya uhakika ya umeme.

NEW BAGAMOYO ROAD PROJECT - NDOTO KUMALIZIKA AUGUST 2013



Bango likionyesha mradi huo unakamilishwa chini ya watu gani.



Barabara ya New Bagamoyo road ambayo inajengwa na serikali kwa kusaidiana na watu wa Japan, hivi sasa ujenzi wake unasuasua licha kuwa bado miezi 4 tu barabara hiyo kukabithiwa kwa serikali

Ujenzi wa barabara hiyo unaofanywa na kampuni ya KONOIKE ina zua adha kwa watumiaji wa barabara hiyo hivi sasa kutokana na kuwekwa kwa road block kibao na ujenzi unaoendelea ambao hauna matumaini ya kumalizika kwa muda ambao uliwekwa na serikali 

Barabar hii ina madaraja 3, moja nila Lugalo jeshini karibu na mwenge maarufu kama Soza, la pili ni la Mbezi Beach maarufu kama Bondeni huku la 3 ni la tegeta kwa ndevu, katika haya madaraja ni upande mmoja tu ndio umekamilika huku upende wa pili ukisuburi neema za wakandarasi hao


Barabara hii inatokea mwenge mpaka tegeta kibaoni, hivi sasa foleni ndio kilio chetu tukisubiri rehema za KONOIKE, TANROADS,JAPAN na SERIKALI kwa ujumla kuokoa hii adha maana sasa neema imegeuka shubiri kwa wakazzi wa jiji wanao tumia barabara hii



BILLIONI 20 KUENDELEZA WAFUGAJI WAGOGO WADOGO NCHINI

BILLIONI 20 KUENDELEZA WAFUGAJI WAGOGO WADOGO NCHINI

Serikali ya Tanzania imesema itahakikisha kwamba hakuna mtanzania ambaye atakufa kwa njaa mwaka huu licha ya kuripotiwa kwa baadhi ya maeneo yaliokumbwa na ukame na njaa kali

hayo yamesemwa na Waziri wa Uvuvi na maendeleo ya Mifugo Mhe. David Mathayo David hii leo jijini Da es Salaam, alipokuwa akifanya ufunguzi wa mradi wa uwezeshaji wakulima na wafugaji vijijini

Waziri Mathayo amesema, japo kuwa kuna uhaba wa chakula katika baadhi ya maeneo lakini serikali haita acha kuwafikishia chakula watu hao, na kuwa serikali inatambua maeneo ambayo yanasumbuliwa na njaa

Waziri Mathayo amezitaka taasisi binafsi kushirikiana na serikali ma maafisa ugani ili kuweza kufikia kilele cha mafanikio katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Katika mradi huo kiasi cha Dola millioni 13.2 zimetolewa na UN ambayo ni sawa na Shilingi Billioni 20 za kitanzania ili kuwafanikisha wajasiliamali wadogowadogo kuendesha biashara zao pamoja na kutafuta masoko kwaajili ya bidhaa zao

Zaidi ya asilimia 75 ya watanzania wameajiriwa na kilimo, hivyo mradi huu utaleta maendeleo kwa watanzania kujiendeleza kiuchumi


KAMPENI UDSM NI BALAA, WAGOMBEA WANADI SERA ZAO UCHAGUZI KUFANYIKA APRIL 29


Washabiki wa Mkolwe Egidy wakimsindikiza baada ya kushuka jukwaani. Egidy anagombea urais wa DARUSO
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam, hii leo wamefungua rasmi kampeni za ugombea nafasi za uongozi wa juu chuo ni hapo

Mwanamke pekee katika kinyang'anyiro hicho Bi. Mashingia Stella
Wagombea hao wapatao wa 5, wa 3 wakigombea nafasi ya Urais huku wawili wakigombea nafasi ya Makamu wa raisi

Blog hii ilifanya mahojiano na Raisi wa DARUSO ambaye anatarajia kumaliza muda wake bwana Bokombe Itembe, ambaye alielezea kuwa kampeni hizo zitakuwa za wiki moja na juma tatu ya wiki ijayo ambayo itakuwa tarehe 29.04.2013

 

“Kampeni zimeanza rasmi leo, wagombea wameanza kunadi sera zao jukwaani kwa muda wa wiki moja kisha jumatatu uchaguzi utafanyika ilikupata viongozi wapya wa DARUSO” alisema Bokombe

Bokombe aliwataka wanafuzni wa chuo hicho kutosusia uchaguzi huo kwani kura zao ndizo zitaleta mabadiliko wanayo yataka, kususia hakuta saidia kitu. Alisema 


Aidha baadhi ya wanafunzi walilalamikia mchakato huo kuwa sio wahaki kwani kuna wagombea ambao walianguka kwenye uchaguzi wa awali lakini bado wameingia kwenye kampeni hizo kama wagombea

“Mtu ameangushwa, baada ya watu 100 kuto mcahgua lakini baadae anakuja kama mgombea nani kamchagua wakati watu 100 tayari walimkataa? Hafai kutuongoza wala hatumtaki” 

wakati mahojiano hayo yakiendelea kelele zilizuka Ndani ya hall ambako kampeni hizo zikifanyiaka kisha umati wawatu ulizuia mahojiano kuendelea kutoakana na kelele nyingi

 

Blog hii iliweza kusikia wanafuzni wakilala mika, wengine wakiendelea kuwa nadi wagombea wao

Hapo awali kulikuwa na tetesi kuwa baadhi ya wagombea hao wamepandikizwa na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini kwa maslahi yao..kitu ambacho wagombea wote wamekanusha kuwa sikweli

Upinzani mkali kati ya wagombea ulionekana waziwazi kila mtu akielezea jinsi gani atawasaidia na kuwatumikia wanafunzi wa chuo hicho na ukomavu wake katika siasa ya chuo hicho

HABARI PICHA 
thecampasvision.blogspot.com

MIKATABA FEKI YAMLIZA JAJI WEREMA, RASILIMALI KUTONUFAISHA WATANZANIA NAKO KWA MKERA, AWATAKA WANASHERIA KUPITIA MIKATABA UPYA


Jaji mkuu Frederick Werema amewataka wanasheria kuondoa malalamiko ya watanzania juu ya mikataba mibovu kwa kupitia upya mikataba ambayo imeshapitishwa ili kuokoa rasilimali za Taifa

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alipokuwa akifungua mafunzo ya sheria ya makubaliano ya kibiashara kwa wanasheria 40 wa Serikali.



Jaji Werema amesema, wanasheria nilazima waamuke na kuomba kuipitia upya mikata upya na waangalie niwapi walikosea ilikuifanya kazi yao kuwa ya weledi na tija kwa taifa.

“Kama sisi tusipo sema wanachi watasema, waandishi kupitia makala na magazeti watasema, nilazima tuseme penye mapungufu bila kumuogopa mtu” alisisitiza Jaji Werema




Jaji Werema alisisitiza kuwa mengi ya tokea yakuibiwa rasilimali zetu yanasababishwa na makosa ya sheria, hivyo tuamke kwani maendeleo ya watanzania yako mikononi mwetu. Alisema kwa msisitizo

“Tuwalinde watanzania na mikataba mibovu (FEKI)tunayo simamia kama wanasheria .. makosa kama ya IPTL, DOWANSA nanyingine yasiwepo kwani makosa mengi yakuibiwa yanasababishwa na makosa ya kisheria” alisema




Pia amewataka wanasheria kujifunza lunga mbalimbali ilikuweza kukabiliana na wawekezaji mbalimbali kwani hiyo itawasaidia kuwa na uwezo mkubwa wakuchambua sheria mbalimbali huku akisisitiza juu ya sheria ya – Tanzania Investment Act[CAP 38 R.E 2012]

Aidha amesema, watanzania wengi hawajui kuwa watungasheria ni wabunge ambao huruhusu mikataba inayo walinda wawekezaji hivyo kuwataka wanasheria kuiwasimamia.




Mafunzo kwa wanasheria hao 40 itafanyika kwa wiki moja lengo ikiwa ni kuwafundisha juu ya kuingia makubaliano ya mikataba ya kibiashara. Mpango uliofadhiliwa na UNDP. Mafunzo hayo yatafanyika shule ya sheria (Law School of Tanzania)

kwamuda mrefu sasa nchi imekuwa ikipoteza rasilimali zake kutokana na mikataba mibovu inayopitishwa na viongozi pamoja na wanasheria.

WANAWAKE NA MAENDELEO - BUNJU SISTERS GROUP TUNASONGA

Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa chama hicho. Miss Loyce Joseph ambaye pia ni CEO wa Blog hii, katikati ni Miss Lucy na mwisho ni Janet Jackson
Bunju Sister group, nikikundi cha Mabinti ambao kinalenga maendeleo zaidi na kusaidia katika mambo ya kijamii, Tunakopeshana fedha na mengine mengi. picha hizi niza kikao kilicho pita


Kikundi cha BSG kinamuda wa mwaka sasa, tayari kina wana-
chama 8, kikundi kinamipango ya kufungua biashara ya kikundi ilikutunisha mfuko wa chama


Mwenyekiti wa kikundi hichi ni Loyce Joseph, Mwenyekiti msaidizi ni Susan Nzota, Muweka hazina Wendi, wanachama wengine ni Lucy, Dianarose, Janet Jackson, Bibianna, na Susan

Wa kwanza Kushoto ni Kaimu Mwenyekiti Miss Zusan Nzota akikamilisha taarifa ya kikao hicho, katikati ni Miss Dianarose na aliye simama ni Miss Wendi

Kikao kilifanyika Dons Girl Pub ambayo iko Mbweni masaiti, marekebisho ya kalenda ya chama yalifanyika, pamoja na kuwatambua wanachama wapya walioomba kujiunga na chama chenu

Susan na Janet wakipata msosi baada ya kikao, katikati ni Muweka azina wetu Miss Wendi
Kikundi kina mkaribisha binti yeyote ambaye anatokea maeneo ya Bunju au Mbweni kujiunga na chama chetu, masharti yetu nikujitambua kwanza. 

PICHA ZIKIONYESHA MAZISHI YA BI. KIDUDE



MAZISHI YA BI. KIDUDE RAIS JK AHUDHURIA, DR. ALLY MOHAMED SHEIN, MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF NA MSANII MAARUFU WA BONGO FLEVA DIAMOND PLANTUM NA FID Q NI MIONGONI MWA MAMIA WALIO HUDHURIA MAZISHI HAYO


Kaburi la Marehemu Bi. Kidude baada ya maziko

Mamia waliohudhuria mazishi hayo yaliyo fanyika hapo jana Zanzibar maeneo ya Kitumba Wilaya ya kati unguja

UHOLANZI YATOA BILLIONI 275 UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE, MWAKYEMBE NAYE AWAPIGA MKWARA WAKANDARASI


Picha ikionyesha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere

Waziri wa uchukuzi Mhe. Harison Mwakyembe ametoa onyo kwa makandarasi wa babaishaji, wasidhani kuwa Tanzania ni kichaka cha kuja kuzolea fedha na kuondoka

Waziri Mwakyembe ame yasema hayo hii leo jijini Dar es salaam wakati wa utiaji saini mkataba wa ujenzi wa jengo jipya la abiria (TB III) katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere

“natoa onyo kwa makandarasi wa bababishaji. Wasidhani Tanzania ni kichaka cha kuja kuzolea fedha na kuondoka, katika ujenzi huu makandarasi watakao simamia nilazima wahakikishe kazi ina malizika kwa muda wa makubalianao yetu kwani kinyume na hapo sheria ya mkataba utafuatwa” Alisema Waziri

Utiaji saini ukiendelea kati ya Tanzania na Uholanzi

Ujenzi wa Jengo hilo unafanywa kwa msaada wa nchi ya Uholanzi, ambapo nchi hiyo imetoa kiasi cha Billioni 275 kukamilisha jengo hilo ambalo litajengwa kwa muda wa miaka 3 kuanzia hivi sasa, Aidha ujenzi wa Jengo hilo utawavutia wawekezaji na mashirika makubwa ya ndege kuleta huduma yako katika Viwanja vya Tanzania

“Mara baada ya mradi huu kukamilika, tunatarajia makampuni makubwa kuleta ndege zao hapa nchini, kuongeza pato la taifa na kuifanya Tanzania kuwavutia watalii wengi zaidi kuliko ilivyo sasa” Alisema Mwakyembe

Naye Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) amesema, Jengo jipya linalo tarajiwa kujengwa litajengwa kwa awamu mbili, ambapo utausisha maegesho ya ndege (APRON) barabara za viungio (TAXIWAYS) maegesho ya magari na barabara ya kuingia kiwanjani

Balozi wa Uholanzi akiongea kwenye utiaji saini huo

Bwana, Suleiman amesema kuwa, Ujenzi wa awamu ya kwanza utakuwa na ukubwa wa mita za mraba 35,00 Elfu wenye uwezo wa kuhudumia abiria Millioni tatu kwa mwaka, huku ujenzi wa awamu ya pili utakuwa na ukubwa wa mita za mraba 25,00 Elfu ukuwa na uwezo wa kuhudumia abiria Millioni Mbili na nusu kwa mwaka.

“Jengo jipya litakuwa na uwezo wa kubeba abiria Millionmi 6 kwa mwaka , pindi ujenzi wa wamu zote mbili kukamilika, lakini mradi uliosainiwa leo utagarimu kiasi cha EURO 133,228,145.45 sawa na pesa za kitanzania Billioni 275” alisema Suleiman

Kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa TAA bwana Suleiman Suleiman akitia saini hapo jana, Nyuma kabisa yupo Waziri wa Uchukuzi Mhe. Mwakyembe

Hivi sasa kiwanja cha kimataifa cha Julius Nyerere kina uwezo wa kuhudumia abiria Milioni 1.2 hadi 4.7 kwa mwaka

Aidha baada ya mradi huo kukamilika kutaiwezesha TAA, kuwatenganisha abiria wanaosafiri ndani ya nchi (Domestic Passengers) ambapo abiria wanaosafiri nje ya nchi (International passengers) watatumia jengo jipya (TB III) na abiria wandani watatumia (TB II)

OUR BELOVED BI. KIDUDE HAS GONE...


Photo: HOTMIX (11:00 Jioni): Nguli wa muziki Bi. Kidude (Fatuma Binti Baraka) afariki dunia. Jiunge nasi SASA katika kutoa pole na upate ripoti kamili kuhusu maisha yake mpaka mauti yalipomfika... Pia, pata kujua yaliyojiri ndani ya BUNGE...

--->> COMMENTS
Mwananziki mkongwe zaidi Tanzania na Duniani Hayati Fatuma Binti Baraka amefariki Dunia hii leo huko Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na uvimbe tumboni

Bi. Kidude anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 100 au 102, kwani hakuna mtu aliye weka kumbukumbu za siku yake ya kuzaliwa lakini marehemu anasema alizaliwa enzi za matumizi ya Rupi huko Zanzibar



Blog hii inaungana na Watanzania wote katika maombolezo ya shujaa wa muziki wa Taarabu nchini

MBUNGE MWINGINE WA CCM ATUKANA BUNGENI LICHA YA MKWARA WA POLISI KUTANGAZWA

MBUNGE MWINGINE WA CCM ATUKANA BUNGENI LICHA YA MKWARA WA POLISI KUTANGAZWA


 Wakati Bunge linamalizia kikao chache cha Asubuhi hii leo (Mkutano wa 11, Kikao cha 6) bila hiyana,
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia tiketi ya CCM Peter Serukamba ametoa tusi Bungeni 




alipopewa nafasi yakuongea baada ya kambi yaupinzani kumaliza kutoa sababu za kisheria kwanini wazungumzie mambo ya Usalama wa Taifa Bunge

Tusihilo ambalo limewalenga watanzania ambao na mwingine ambaye mbunge huyo anamjua yeye

“tusi lenyewe nitaliandika kama alivyo tamka mheshimiwa wetu 'came one FUCK YOU', miongoni mwa tusi kubwa kuliko yote Bungeni” Mbaya zaidi watoto na wanajua kingereza siku hizi

.... angalizo Mhe. Mbunge akuogopa kutaja tusi mbele ya Bunge Tukufu na Kwenye Television ya Taifa huku akiwa na uhakika kwamba watanzania wengi wanatazama Blo hii ijaona haya pia kusema

Ikiwa ni siku moja tu baada ya Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda kupiga mkwara na kusema Polisi watatinga Bungeni kumkamata mbunge yeyote atakaye tukana

****
>Matusi yenu yanafanya tunasahau yote ya msingi mliotangulia kuongea
>Pia hii inaonyesha udhaifu wa uongozi wa Bunge
>Madhara ya Kupendelea upande mmoja
>Bunge limegeuka Pango la wahuni

Kama kanuni za Bunge sio kitu, Spika sio kitu na watanzania sio kitu mbele ya mnayo yafanya kwao basi hata viliovyetu sio shida kwenu …. matusi yenu sio ya njaa tulizo nazo na ugumu wa maisha bado mnatutusi hadi kwa maneno

SERIKALI YAJIPANGA KUONGEZA MAPATO YA MADINI


Great Rift Valley Mining Summit (GRV) hii leo wamekutana nchini Tanzania kwa siku mbili kuangalia njia za kuongeza mapato kupitia vivutio vya madini

Mkutano huo umehusisha nchi zilizoko kwenye nchi za Bonde la ufa, miongoni mwa nchi hizo ni Uganda, Malawi, Zambia, Ethiopia, Mozambique, na Kenya

Akiongea kwenye mkutano huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Stephen Masele amesema Lengo kubwa la mkutano huo ni kuinua mapato yanayopatikana kwenye madini, pamoja na kuweka mazingira mazuri ya watanzania kuwekeza katika madini” alisema Masele

“Lengo kubwa ni kuainisha vivutio vya uwekezaji kwenye madini ilikuongeza mapato ya serikali” Alesema Masele


Aidha Masele amesema, tayari wameanzisha mfuko maalum wa kuudumia mazingira na watu wanao zunguka maeneo ya migodi ambayo inasaidia katika ujenzi wa mashule, barabara na Hospitali ikiwa pamoja na kutunza mazingira ya maeneo husika. Alisema

Naye Mtendaji mkuu wa mamlaka ya ukaguzi wa madini nchini (TMMA)
Bwana Paul Masanja amesema jumla ya shilingi Billioni 480 zimekusanywa na mamlaka hiyo kwa muda wa miaka 3 toka kwa makampuni makubwa ya madini nchini

“Jumla ya Billioni 480 zimekusanywa kwa miaka 3 toka makampuni makubwa nchini ambayo yanafanya biashara ya madini, kiasi hiki ni faida kwa taifa” na kuongeza kuwa kiasi hicho ni sawa na nusu ya faida ya asilimia 15.51% ya faida ambayo taifa inapata kulinganisha na wawekezaji.

Bwana Paul Masanja alisema kuwa, Tangu mwaka 1998 mpaka 2012 serikali imepata faida ya jumla ya shilingi Trillioni 12.6 ambayo nayo imekusanywa kwenye mapato ya migodi yote hapa nchini

Aliongeza kuwa, Kwa muda wa mwaka mmoja serikali inakusanya kiasi cha Billioni 1.4 kama makusanyo yatokananayo na madini ya ujenzi tofauti na ilivyo kuwa hapo awali, ambapo serikali ilikuwa inakusanya Millioni 3 tu kutoka kwenye madini hayo

Kamishna wa madini nchini bwana Ally Samaje amesema fursa za kumiliki hisa kwa watanzania ninyingi kuliko wageni kwani mtanzania anapaswa kuwa na hisa ya kiasi cha asilimia 25% zaidi ya wageni ili kuwawezesha kunufaika na madini hayo
WANAHARAKATI WALIA NA WALEMAVU, WATAKA UCHAGUZI WA MABARAZA YA KATIBA URUDIWE

WANAHARAKATI WALIA NA WALEMAVU, WATAKA UCHAGUZI WA MABARAZA YA KATIBA URUDIWE

Washirika wa jukwaa la wazi la semina za jinsia na maendeleo GDSS linalo ratibiwa na TGNP, hii leo wameitaka serikali kurudia uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba ya wilaya, kata na mitaa

Tamko hilo limekuja baada ya taasisi hiyo kueleza kuwa mchakato huo uligubikwa na Ubaguzi wa kijinsia, Rushwa, Udini, na siasa huku miongoni mwa watu 7 watakao wakilisha mitaa hakuna nafasi ya walemavu

Akitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari hii leo TGNP, katibu wa GDSS bwana Badi Darusi amesema kuwa nilazima Serikali kurudia mchakato huo ilimakundi yaliyo achwa pembezoni kama walemavu na wanahabari wapewe nafasi

“Hakuna anaye wakilisha walemavu, watu 7 ambao ni wanawake 2 wasichana 2, wanaume 2 na wengine 1 hakuna mlemavu...walemavu hawana mwakilishi mabaraza ya katiba” alisema Darus

Darus amesema, katika swala la Siasa kuchukua nafasi kubwa. Vyama vya siasa vilikuwa zinatumia fursa ya kufanya kampeni chafu kinyume nataratibu zilizo wekwa na Tume ya taifa ya mabadiliko ya katiba.

Aidha wameelezea kuwa mchakato huo pia uligubikwa na vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji uliofanywa na baadhi ya viongozi wa mitaa na vyama vya siasa hali iliyopelekea kutoa tamko lao hivyo kuitaka serikali kurudia tena zoezi la uchaguzi wa mabaraza ya katiba.

SIKU YA WAJASIRIAMAMLI DUNIANI- WASHAURIWA KUKOPA

SIKU YA WAJASIRIAMAMLI DUNIANI- WASHAURIWA KUKOPA




Wajasiriamali wameshauriwa kutoogopa kukopa na kutumia taasisi za mikopo katika kuendeleza biashara zao

Hayo yamesemwa na Gershom Mpangala ambaye ni Meneja Masoko wa FINCA 



(FINCA Tanzania Limited) alipokuwa akifanya mahojiano na Blog hii. FINCA imekuwa ikitoa mikopo kwa wajasiriamali zaidi ya Elfu 70 hapa Tanzania

Mpangala amesema, swala la wajasiriamali wengi kuogopa kukopa ni moja ya kikwazo cha kutoendelea kwa biashara nyingi.

Aidha amewataka wajasiriamali kutambua kuwa hata wafanya biashara wakubwa au ambao wanamiliki biashara tofauti tofauti wamefanikiwa zaidi kwa kutumia mikopo kwenye biashara zao

“ Wajasiriamali wakubwa, mfano wanaofungua ma Benk na huduma nyingine kubwa katika jamii wame fanikiwa kutokana na kukopa, wakope au wahudhurie semina zinazo fundisha jinsi ya kuendeleza biashara kwakutumia mkopo, watafanikiwa zaidi” Alisema

Nidhamu ya Pesa, pia ni msingi wa kuendeleza biashara yako, ujue jinsi gani ya kupata Faida na kuokoa hela ya mtaji wako... hichi pia ni kikwazo kwani wengi hutumia faida anayo pata na mtaji bila kujua atumie pesa hipi katiya hizo ilikuendeleza biashara yake.

Ikiwa leo ni siku ya wajasiriamali Duniani, kwa Tanzania siku hii imeachwa kwenye mitandao kwani wajasiriamali wengi hawajui siku hii

UMEME VIJIJINI - NEEMA YAJA, EU KUISAIDIA TANZANIA



Wizara ya Nishati na Madini imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada kutoka NORWAY kwaajili ya umeme vijijini, ambayo nikiasi cha Kr 700 ambayo ni karibu USD 140 sawa na Billioni 200 za Kitanzania




Uhakika wa kukamilisha miradi ya umeme kwenye wilaya mpya 13 ambayo itagarimu kiasi cha Billioni 70 hasa vijijni itaenda kwa wakati, Aidha bado maongezi na wafadhili wengine juu ya miradi ya umeme nchini inaendelea huko Brussels.

Viongozi wa  juu wa Wizara ya Nishati na Madini hapo jana, walifanya kikao cha majadilianao na EU ilikukamilisha makubaliano ya kukamilisha miradi ya umeme ambapo Mei 3,2013  EU mishion itakuwa Dar ilikufanikisha miradi hiyo

Kikao hicho kilicho mhusisha kaimu Mkurugenzi wa wizara hiyo na Balozi wa EU pamoja na wadau wengine wa sekat hiyo, lengo ni kuondoa tatizo la umeme.

Aidha EU itatoa Grants kwenye miradi ya Transmission, Distribution, Energy, Efficiency, Renewerbale energy pamoja na Capacity building kwa wizara hiyo

EU imeamua kuifanya Tanzania nchi muhimu sana kwa ushirikiano wake na Afrika, hivyo kuamua kukamilisha miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Hatahivyo, Bwawa la mtera limeweza kufikisha kiasi cha chini cha uendeshaji wake(Minimum Level) cha 690 M.A.S.I kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini.

Taarifa kutoka ndani ya Wizara hiyo zinasema kuwa wanatarajia kiwango hicho kuongezeka ili kuweza kufikia hatua nzuri ya uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo ambalo hivi karibuni lili punguza kiwango chake cha uzalishaji kutokana na kina cha maji kupungua.
MBWA AHAMIA BUNGENI, MHAKAMA NAYO YAKANA KUWANYIKA HAKI WANANCHI

MBWA AHAMIA BUNGENI, MHAKAMA NAYO YAKANA KUWANYIKA HAKI WANANCHI

KUTOKA BUNGENI

Mbunge wa Kondoa Kusini Mhe. Juma Nkamia hii leo ameshangaza jamii alipomuita Mbunge mwenzake Mhe. Joseph Mbilinyi Mbunge wa Mbeya Mjini kuwa ni “MBWA” alipokuwa akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi wa Waziri Mkuu inayoendelea hizi sasa Bungeni

Bila hiyana Mhe. Nkamia alitamka neno hilo zaidi ya mara moja kuwa Mhe. Mbilinyi ni Mbwa licha kuambiwa kutofanya hivyo na Naibu spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai

“Sugu naomba uwena eshima, mimi sizungumzi na Mbwa nazungumza na Mwenye Mbwa” wkati mabishano yakiendelea Mhe. David Machali aliingilia na kusema.... kwakuwa umesema sugu ni mbwa inamaana spika ni Mbwa na wabunge nao ni Mbwa.”

“Nkamia naye Alijibu tena aliye toa hoja sio makini kwani swezi kuongea na watu wasiokuwa makini, … Spika aliingilia baada ya mjadla kuendelea sana hali inayoonyesha upendeleo wa waziwazi alioufanya Spika...

“Nkamia baada ya kuambiwa aombe radhi kwa kauli hiyo alisema.... Kilicho nifanya nikosema maneno hayo ni maneno ya chini chini ya aka Sugu....akadai alicho maanisha ni Kuwa anaongea na baba na sio mtoto nakuongeza kuwa nyimbo za Sugu ataendelea kuzisikiliza”

MAHAKAMA YAKANA KUWANYIMA HAKI WANANCHI

Jaji mkuu Fredrick Werema amepinga vikali swla la serikali kutumia mahakama kama chombo cha kuwapiga wanyonge baada ya kujibu swali aliloulizwa na mbunge wa viti maalum Magdalena Sakaya ambaye alitakja kujua kwanini serikali inafanya hivyo huku akisema juu ya swala la mgomo na madai ya walimu

“Serikali nimhajiri kama waajiri wengine swala la kwenda mahakamani ni lakisheria na sikweli kwamba mahakama inatumiwa kuzuia haki za wanyonge alisema JAJI mkuu.

Hoja inayoendelea kujadiliwa hivi sasa bungeni ni Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na wizara zote zilizopo chini yake.

WANAFUNZI 35 VETA WALA SHAVU, KUTUMIWA NA NHC UJENZI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU


Mashine ya hydraform kuzalisha matofali ya bei rahisi
Wanafunzi 35 kutoka chuo cha Fundi Stadi (VETA) wamechaguliwa kuendesha mashine ya Hydroform inayo fyatua matofali ya bei rahisi yatakayo tumiwa na shirika la nyumba la Taifa (NHC) katika ujenzi wa nyumba zaidi ya Elfu 5000 nchini 

wanafunzi 35 watakao hudhuria mafunzo hayo
Akiongea katika makubalianao na VETA yautoaji mafunzo kwa wanafunzi hao, Mkurugenzi mkuu wa NHC bwana Nehemia Kyando Mchechu amesema shirika hilo liko kwenye utekelezaji wa ujenzi wa nyumba Elfu 5000 za garama nafuu

“ MASHINE ya Hydroform itazalisha tofali nyingi kwa garama ndogo, pia aiharibu mazingira. Tutakamilisha ujenzi wa nyumba 5000 ambazo tutaziuza kwa garama za chini hivyo kila mtu ataweza kununua ”Alisema

Mkurugenzi mkuu wa NHC na Mkurugenzi mkuu wa VETA wakisaini makubaliano hayo

Mchechu amesema , NHC imejenga nyumba za Garama ya Millioni 35 tu lakini hizi sasa wanaitaji kupunguza garama hiyo, japo kuwa bei ya ujenzi wa nyumba inatofautiana mikoa hadi mkoa kulingana na upatikanaji wa maitaji ya ujenzi

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha VETA bwana Zebedia Moshi amesema. Chuo hicho kimeanzisha mikakati ya kuwapatia ajira wanafunzi wanao soma chuo ni hapo ilikukabiliana na uhaba wa soko la ajira nchini kwani lengo lao nikufikisha asilimia 95% yawanafunzi wanao pata ajira ndani ya miaka 5
  
“ Ndai ya miaka 5 tunataka vijana wapate ajira kwa kiwango cha asilimia 95%, kwani hivi sasa ni asilimia 66% yawanafunzi wanaojiajiri kutoka vyuo vya VETA kote nchini huku Asilimia 43% wanahajiriwa, kwakushirikiana na wadau tutaongeza kiwango kilichopo hivi sasa” Aliseam

Jumla ya wanafunzi 35 ambao wamechaguliwa na NHC watapewa mafunzo ya wiki mbili baadae watagawanywa kwenye mikoa mbalimbali nchini ikiwemo GEITA, KIGOMA,SONGEA ,KATAVI TANGA na Dar es Salaam (Kigamboni)


Kategori

Kategori